JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Nimeona mjadala kuhusu mihula anayoruhusiwa kugombea makamu aliyeshika madaraka ya Urais kutokana na kuchukua kiti katikati ya muhula baada ya Rais aliyekuwepo madarakani kushindwa kuendelea aidha kwa kufariki akiwa madarakani, kujiudhuru au sababu za kiafya. Mjadala umechagizwa na kauli ya Sophia Mjema aliyesema Rais Samia ni hadi 2035, huku wanaharakati wakipinga vikali kuwa hana sifa ya kugombea mihula miwili tena. Je, ukweli ni upi?
Kuna magonjwa mengi yanayosababisha upungufu wa Kinga mwilini ikiwemo maambukizi ya VVU. Kumekuwa na mijadala mingi pamoja na tetesi zinazohitaji majibu ya kina kuhusu uwezekano wa kupata VVU/UKIMWI kutoka kwa mtu aliye athirika hasa ikihusisha ushiriki wa tendo la ndoa pasipo kutumia kinga hata kama ni mara moja tu. Ukweli upoje na majibu ya kisayansi yanatoa picha gani? Baadhi hudai hauwezi kupata VVU/UKIMWI kwa kufanya tendo moja tu la ngono na muathirika pasipo kutumia kinga kwa kuwa maambukizi hayaji kirahisi hivyo kama tunavyodhani.
Habari wakuu, nimeshangaa sana kuona WASAFI TV ikitumia lugha ya kihuni tena yenye maudhi katika uwasilishaji wa taarifa. Chombo mahili hakiwezi kutumia neno 'usela mavi' katika kufikisha ujumbe wake kwa hadhira,binafsi siyo mtaalamu wa teknolojia labda nyie wajuvi wa mambo hayo tazameni hii video chini kisha mniambie kama ni editing au laa. Kama ni Wasafi kweli lazima tujiulize maswali yafuatayo: Je hii jeuri wanaipata wapi ya kutudhihaki sisi juu ya msiba mkubwa kama huo? Je wao wanatumika katika kuchochea maovu ya utekaji au wao wanajikuta akina nani labda na chombo chao? Je wamezingatia nini katika uwasilishaji wao wa hiyo habari na je wameelewa kweli nini maana ya kupinga na kupaza sauti kwa vitendo juu ya mauaji? Pia soma...
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…