JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

On JF:

Wakuu nimekutana na video inayosambaa kwa kasi sana mtandaoni ambapo wanaonekana John Mrema na John Mnyika, na Mrema akisikika kuwa atatoa maoni juu ya usafiri huo mara baada ya safari kukamilika lakini kinachonipa utata ni sauti inayosikika katika video hiyo baada ya Mrema ikisema viongozi hao wamesifia huduma za usafiri wa treni ya mwendokasi (SGR) na filamu ya royal tour wakati Mnyika na Mrema hawaonekani wakitoa maoni hayo, Je kuna ukweli wowote hapa?
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kikitangaza kufanya Maandamano ya amani leo Jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amechapisha mtandaoni mwake akisema anazo taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe yupo Arusha na hivyo kumualika ofisini kwake Jijini Arusha. Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka" Ikumbukwe kuwa saa chache zilizopita, nyumba ya Freeman Mbowe iliyopo Mikocheni ilizingirwa na Jeshi La Polisi huku mkewe Dr Lilian Mtei akiripotiwa kuzuia kutoka nyumbani kwake. Source: Jambo TV
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu, amesema Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amemzuia kwenda katika ofisi kutokana na yeye kueleza ubadhirifu unaofanywa ndani ya chama. Pia Lissu amesema sababu nyingine ya kuzuiwa kwenda katika ofisi hizo ni kutokana na kutoa siri za vikao ndani ya chama, na kumueleza ukweli kuhusu kitendo cha kuanzisha taasisi nyingine ndani ya CHADEMA. Aidha Mwanahalisi ina nakala rasmi ya barua ya siri ambayo Mbowe amemwandikia Lissu kwa kumpiga zuio la kwenda ofisini.
Back
Top Bottom