Je, biblia ni copy & paste ya hadithi za kale za kipagani na sio UHALISIA?

zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
19,081
28,742
Habari za kazi wanajukwaa, bila ya kupoteza muda niende kwenye mada.... Je biblia iliiga simulizi zake kutoka dini za kipagani na kuhadaa watu kuwa ni stori za ukweli???

Kwenye biblia kuna hadithi kadhaa za watu muhim ambazo nyingi zilishakuwa zimesimuliwa hata kabla ya biblia kuandikwa tuangalie mifano michache hapo chini

1.Story ya Hawa/Eve wa biblia Vs Story ya pandora box
. Story hizi zinafanana kwa kiasi kikubwa sababu zote zinaelezea uumbaji wa mwanadamu wa kwanza ulikuwaje na kivipi mwanamke alipelekea anguko la dunia hii. Story ya pandora inaelezea kuwa mwanadamu wa kwanza aliumbwa na miungu ya kipagani kutumia udongo, akapuliziwa uhai na miungu akapelekwa kuishi duniani, pia anapata mwanaume anaitwa epimethius, aanapewa BOX na anaambiwa asifungue ila siku moja anashawishiwa kupitia mungu anaitwa HERA kufungua bila kujua lina kila aina ya ubaya kuanzia tamaa,uchoyo,kifo,mauaji,visasi na dhambi zingine nyingi na hivyo kupelekea dhambi kuingia duniani!! ukiangalia kwa umakini story hii inafanana kabisa na kisa cha adam na eva ambao nao waliumbwa kwa udongo,waliwekwa duniani, walipewa pumzi na Mungu pia walipewa masharti wasile tunda flani ila mwisho wa siku eva anashawishiwa na nyoka na kula hivyo kupelekea anguko la mwanadamu . Kinachoshangaza hadithi hii ya pandora ilishaanza kusimuliwa miaka zaidi ya 800-1000 kabla ya kristo ila story ya adam na hawa kwa mara ya kwanza inaandikwa kwenye biblia miaka 400 kabla ya kristo je iliigwa au kila mtu aliandika kivyake???

2. Nuhu na gharika Vs utnapishtim na gharika. Kwenye biblia Nuhu aliagizwa na Mungu ajenge boti kubwa achukue wanyama wote na kuingia humo maana kuna mvua kubwa inaletwa na Mungu ambayo itafuta uzao wote wa mwanadamu na baada ya gharika anatoa sadaka kumshukuru Mungu. Stori hii inafanana na kisa cha EPIC OF GILGAMESH kilichoandikwa takribani miaka 2700 kabla ya kristo ilihali kuendana na biblia gharika na Nuhu limetokea takribani miaka 2147-2500 kabla ya kristo. Sasa basi kwenye kisa cha Epic of gilgamesh tunaona kuna mtu anaitwa utnapishtim huyu naye anaambiwa na mungu EA kwamba ajenge boti (yenye vipimo sawasawa na Nuhu),anachukua wanyama wote, mvua kubwa inanyesha na uzao wote unakufa, baada ya gharika utnapishtim anatuma ndege wawili kupima kma mafuriko yameisha na kma vile Nuhu na yye anatoa sadaka kwa miungu iliomponya na gharika. Kisa hiki kimesimuliwa hata kabla story ya Nuhu wa biblia hajazaliwa!!!! Je imenakiliwa ama ni matukio mawili tofauti??

3. Story ya Musa kwenye Biblia Vs Story ya Sargon wa Akkadia
. Visa vya watu hawa wawili vinafanana kabisa kuanzia kuzaliwa mpaka utawala wao. Wote wanazaliwa kwa siri, wote wanawekwa kwenye kikapu kinachoelea kwenye mto, wote wanaokotwa na malkia/binti mflame wa nchi husika na wote wanatunzwa kwenye kasri huku mwishoni kabisa wote wanaongoza jamii zao kwenye ukombozi!!! Zingatia kwamba Sargon aliishi miaka 2279 Kabla ya kristo ilihali Musa amezaliwa miaka 1391 kabla ya kristo?? Je hi nayo ni copy and paste ama ni matukio mawili tofauti

4. Amri kumi za Mungu Vs amri za Hammurabi. Hapa sina mengi ya kusema ila takribani mfumo na amri za Mungu alizopewa Musa zinafanana na Amri za mungu SHAMASH alizompatia mfalme Hammurabi wa mesopotamia zingatia kitabu cha kutoka kimeandikwa takriban miaka 500 kabla ya kristo na Musa aliishi takriban miaka 1300 kabla ya kristo huku Hammurabi alishakufa miaka 1750 kabla ya kristo yaani amekufa miaka zaidi ya 400 kabla musa hajazaliwa wala amri 10 za Mungu hazijaandikwa je mfanano huu ni coincidence au ni copy and paste na kuhadaa watu

Mifano ni mingi takribani 100 ya simulizi za biblia zinazofanana kwa 90% ya simulizi za hadithi za kipagani hasa za sumeria na kigiriki ambazo zimesimuliwa miaka mingi hata kabla Biblia haijaandikwa wala watu wanaotajwa kwenye biblia hawajazaliwa bado

NB: Mada hii nimeweka ili mjadala huu upate hitimisho kama ni kweli biblia ni copy and paste ama ni halisi ila tuujadili kwa ushahidi wa kihistoria na sio kwa misingi ya kidini hivyo sitegemei kashfa za kidini humu ila tujadiliane kwa kuelimishana nategemea wengi tutajifunza mengi katika uzi huu wa kufikirisha

Naomba kuwasilisha
 
NB: MODS NAOMBA MSIUNGANISHE UZI HUU ULE WA PROJECT UNAONGELEA QURAN NA BIBLIA KUWA NI PROJECT ZA WATU ILA YANGU INAONGELEA BIBLIA PEKEE NA INAONGELEA KAMA NI COPY AND PASTE HIVYO NI HOJA MBILI TOFAUTI NAWAOMBA MSIUNGANISHE PLEASE

Naomba kuwasilisha

Tujadili nini ndugu yangu. Ukianza kuiweka Biblia sambamba na hizo simulizi tayari unakuwa umeweka msingi mbaya.
 
1.Story ya Hawa/Eve wa biblia Vs Story ya pandora box
. Story hizi zinafanana kwa kiasi kikubwa sababu zote zinaelezea uumbaji wa mwanadamu wa kwanza ulikuwaje na kivipi mwanamke alipelekea anguko la dunia hii. Story ya pandora inaelezea kuwa mwanadamu wa kwanza aliumbwa na miungu ya kipagani kutumia udongo, akapuliziwa uhai na miungu akapelekwa kuishi duniani, pia anapata mwanaume anaitwa epimethius, aanapewa BOX na anaambiwa asifungue ila siku moja anashawishiwa kupitia mungu anaitwa HERA kufungua bila kujua lina kila aina ya ubaya kuanzia tamaa,uchoyo,kifo,mauaji,visasi na dhambi zingine nyingi na hivyo kupelekea dhambi kuingia duniani!! ukiangalia kwa umakini story hii inafanana kabisa na kisa cha adam na eva ambao nao waliumbwa kwa udongo,waliwekwa duniani, walipewa pumzi na Mungu pia walipewa masharti wasile tunda flani ila mwisho wa siku eva anashawishiwa na nyoka na kula hivyo kupelekea anguko la mwanadamu . Kinachoshangaza hadithi hii ya pandora ilishaanza kusimuliwa miaka zaidi ya 800-1000 kabla ya kristo ila story ya adam na hawa kwa mara ya kwanza inaandikwa kwenye biblia miaka 400 kabla ya kristo je iliigwa au kila mtu aliandika kivyake???.
Mkuu naomba nikusahihishe hapa:
Pandora hakuwahi kuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa na miungu.

Kabla ya miungu na binadamu kulikuwa na kitu kinaitwa void of Chaos ambapo kupitia hiyo void wakatokea miungu Chronos na Ananke ambao hawa walizaa miungu mingi sana lakini mikubwa ikiwa ni Gaia (earth), Tartarus (hell), Eros (desire), Erebus (darkness) na Nyx (Night).

Kupitia Gaia ambaye alikuja akamzaa Uranus (Sky) then akamfanya mumewe wakazaliwa miungu iitwayo Titans hawa walikuwa Cronus na Rhea ambao ndio wakazaa miungu ingine

Miungu iliyozaliwa na Cronus+Rhea ilikuwa Zeus (sky & thunder god), Poseidon (sea & ocean god), Hades (god of underworld), Hestia (hearth/soil god), Hera (women, marriage, family na childbirth god) na Demeter (harvest and agriculture god).

Ambayo baadae kwa ushawishi wa Zeus ambaye alikuwa mungu mdogo zaidi lakini aliyekuwa anaheshimika iliwaangusha wazazi wao na yenyewe ikawa miungu mikuu, kumbuka wakati wote huo inakaa Mlima Olympus

Sasa tukirudi kwa huyu Pandora yeye hakuwa mwanamke wa kwanza kuumbwa na hii miungu, ni kwamba kuliumbwa binadamu wengi kabla yake lakini hawakuwa civilized yani wao ilikuwa kazi ni kuiabudu miungu tu. Baadae kidogo mungu mmoja ulioitwa Prometheus uliiba Moto na kuwapa binadamu ambapo kupitia moto ndipo binadamu tukaanza kuwa civilized!.

Zeus baada ya kujua Prometheus kawapelekea binadamu moto akakasirika sana, akawaamuru miungu yote itoe kitu cha thamani kusaidia kutengeneza kiumbe mwanamke (Pandora) na kama adhabu alimuumba toka kwenye udongo!.. Na ili kumkomoa Peometheus ndipo huyo mwanamke akakabidhiwa Epimitheus kaka yake na Prometheus.

Ina maana tunaweza jiuliza hao binadamu waliopelekewa moto na Promotheus walikuwa wameumbwa na nini!?.. Na kama Pandora alikuwa kaumbwa kwa udongo pamoja na uzuri wote kama adhabu je wengine walikuw wameumbwa na nini?.

Kuna mada nilijaribu muelezea Pandora kupitia wick ya kwanini baby hua napenda muita pandora
 
Nyie mnaosemaga Mungu hayupo.wapuuuuuuzi nyie
Mkuu jikite kwenye mada hakuna aliyesema Mungu hayupo nmeuliza tu sasa matusi yanasaidia kujibu hoja?? Kma unaona sielewi nieleweshe sio matusi tusiweke mahaba ya dini mbele ndio maana nimeomba tujadili kwa kutumia ushahidi wa kihistoria kuliko kiimani
 
Mkuu naomba nikusahihishe hapa:
Pandora hakuwahi kuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa na miungu.

Kabla ya miungu na binadamu kulikuwa na kitu kinaitwa void of Chaos ambapo kupitia hiyo void wakatokea miungu Chronos na Ananke ambao hawa walizaa miungu mingi sana lakini mikubwa ikiwa ni Gaia (earth), Tartarus (hell), Eros (desire), Erebus (darkness) na Nyx (Night).

Kupitia Gaia ambaye alikuja akamzaa Uranus (Sky) then akamfanya mumewe wakazaliwa miungu iitwayo Titans hawa walikuwa Cronus na Rhea ambao ndio wakazaa miungu ingine

Miungu iliyozaliwa na Cronus+Rhea ilikuwa Zeus (sky & thunder god), Poseidon (sea & ocean god), Hades (god of underworld), Hestia (hearth/soil god), Hera (women, marriage, family na childbirth god) na Demeter (harvest and agriculture god).

Ambayo baadae kwa ushawishi wa Zeus ambaye alikuwa mungu mdogo zaidi lakini aliyekuwa anaheshimika iliwaangusha wazazi wao na yenyewe ikawa miungu mikuu, kumbuka wakati wote huo inakaa Mlima Olympus

Sasa tukirudi kwa huyu Pandora yeye hakuwa mwanamke wa kwanza kuumbwa na hii miungu, ni kwamba kuliumbwa binadamu wengi kabla yake lakini hawakuwa civilized yani wao ilikuwa kazi ni kuiabudu miungu tu. Baadae kidogo mungu mmoja ulioitwa Prometheus uliiba kuiba Moto na kuwapa binadamu ambapo kupitia moto ndipo binadamu tukaanza kuwa civilized!.

Zeus baada ya kujua Prometheus kawapelekea binadamu moto akakasirika sana, akawaamuru miungu yote itoe kitu cha thamani kusaidia kutengeneza na kama adhabu alimuumba toka kwenye udongo!.

Ina maana tunaweza jiuliza hao binadamu waliopelekewa moto na Promotheus walikuwa wameumbwa na nini!?.. Na kama Pandora alikuwa kaumbwa kwa udongo pamoja na uzuri wote kama adhabu je wengine walikuw wameumbwa na nini?.

Kuna mada nilijaribu muelezea Pandora kupitia wick ya kwanini baby hua napenda muita pandora
Ok nimekusoma mkuu naona umeshiba sana kuhusu greek mythology ulipomtaja Prometheus nilishtuka!!! Big up

je tukirudi kwenye mada kuna ukweli kuhusu hizi propaganda kwamba baadhi ya simulizi kwenye biblia ni copy and paste ya mythology za jamii mbalimbali
 
Mkuu jikite kwenye mada hakuna aliyesema Mungu hayupo nmeuliza tu sasa matusi yanasaidia kujibu hoja?? Kma unaona sielewi nieleweshe sio matusi tusiweke mahaba ya dini mbele ndio maana nimeomba tujadili kwa kutumia ushahidi wa kihistoria kuliko kiimani
Kuambiwa upuuuzi sio tusi, I la fikiria unapost nini.maada uliyoanzisha imekaa kidini dini
 
Mkuu hapa kuna majadiliano ya kawaida tu kuelimishana sasa kuanza kutukana bila kujibu hoja mnakuwa hamsaidii hizi hoja zimeibuliwa sana na watu ndio maana nikaona nianzishe uzi ili majibu yapatikane sasa kuanza kuniita mpuuzi ndio ustaarabu gani kama huna cha kujibu basi unapita tu ila wanaotaka kuelimishana ndio wanachangia

Narudia tena tusiingize mahaba ya dini kwenye hii mada ni simple tu unasema ndio au hapana with facts hizi kuitana wapuuzi sioni kama ni ustaarabu

Samahani kama nimekuwaza lakini

Karibu uchangie maoni yako
 
Duuuuu! Wacha nipite hivi
 
Mkuu naomba nikusahihishe hapa:
Pandora hakuwahi kuwa mwanadamu wa kwanza kuumbwa na miungu.

Kabla ya miungu na binadamu kulikuwa na kitu kinaitwa void of Chaos ambapo kupitia hiyo void wakatokea miungu Chronos na Ananke ambao hawa walizaa miungu mingi sana lakini mikubwa ikiwa ni Gaia (earth), Tartarus (hell), Eros (desire), Erebus (darkness) na Nyx (Night).

Kupitia Gaia ambaye alikuja akamzaa Uranus (Sky) then akamfanya mumewe wakazaliwa miungu iitwayo Titans hawa walikuwa Cronus na Rhea ambao ndio wakazaa miungu ingine

Miungu iliyozaliwa na Cronus+Rhea ilikuwa Zeus (sky & thunder god), Poseidon (sea & ocean god), Hades (god of underworld), Hestia (hearth/soil god), Hera (women, marriage, family na childbirth god) na Demeter (harvest and agriculture god).

Ambayo baadae kwa ushawishi wa Zeus ambaye alikuwa mungu mdogo zaidi lakini aliyekuwa anaheshimika iliwaangusha wazazi wao na yenyewe ikawa miungu mikuu, kumbuka wakati wote huo inakaa Mlima Olympus

Sasa tukirudi kwa huyu Pandora yeye hakuwa mwanamke wa kwanza kuumbwa na hii miungu, ni kwamba kuliumbwa binadamu wengi kabla yake lakini hawakuwa civilized yani wao ilikuwa kazi ni kuiabudu miungu tu. Baadae kidogo mungu mmoja ulioitwa Prometheus uliiba kuiba Moto na kuwapa binadamu ambapo kupitia moto ndipo binadamu tukaanza kuwa civilized!.

Zeus baada ya kujua Prometheus kawapelekea binadamu moto akakasirika sana, akawaamuru miungu yote itoe kitu cha thamani kusaidia kutengeneza na kama adhabu alimuumba toka kwenye udongo!.

Ina maana tunaweza jiuliza hao binadamu waliopelekewa moto na Promotheus walikuwa wameumbwa na nini!?.. Na kama Pandora alikuwa kaumbwa kwa udongo pamoja na uzuri wote kama adhabu je wengine walikuw wameumbwa na nini?.

Kuna mada nilijaribu muelezea Pandora kupitia wick ya kwanini baby hua napenda muita pandora
hizi hekaya mnazitoa wapi jameni?. wekeni vyanzo basi.
 
Story nyingi za kwenye bible zina uthibitisho wa kihistoria, je hao wengine wanao huo uthibitisho.

May wao ndio wamecopy na ku paste ili kui discredit bible na kuwapotosha watu, na ndio wakarudisha nyuma hizo story zao, kama walivyofanya waarabu.
Okay ila kuna tablet kwa mfano hizo za gilgamesh zina miaka zaidi ya elfu 2 kabla ya kristo alafu unakuta story hiyo hiyo ipo kwenye biblia miaka kadhaa baadae je hiyo ni kwa bahati tu au ndio kama unavyosema walirudisha miaka nyuma??
 
Back
Top Bottom