Zitto Kabwe Anajenga Hoteli ya Kifahari! [Zitto kafafanua]

Status
Not open for further replies.
Kwa sasa hoteli hii imefikia ghorofa ya 3, na inakwenda kwa kasi!....
Tunaandaa picha kamili za nyumba hiyo ili wabishi muone!
N asiku moja tutamphotoa akiwa ameenda kuangalia maendeleo!
Labda amsusie nduguye!

Acha usanii mkuu. Jiheshimu angalao kidogo basi. Kwa vile nyumba imefikia ghorofa ya 3 na inakwenda kwa kasi basi automatically ni ya Zitto? Tokea lini picha za nyumba zikadhibitisha mmiliki wa nyumba? Halafu hii habari is completely hearsay. Unadai umepigiwa simu na ndugu yako anayeshi Dodoma. Bila hata kutumia ubongo wako uka-login JF na kuandika this hearsay bila hata kufanya utafiti wa aina yoyote. Respect yourself brother. Vitu kama hivi vinahitaji evidence na sio kupayuka tuu. Hata kama hiyo nyumba ni ya Zitto, huoni kama umeshaharibu hata kupata ushahidi? Watu wengine mnakera yaani basi tuu.
 
haka bana kajanja sana..kako kama sungura analala jicho moja kafumba linhine wazi..toka awe mjumbe kwene kamati ya madini kapoteza makali kabisaaaaaa
 
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!

Naona Zitto ameshakujibu, na wewe mpigie simu ndugu yako umpe majibu akupe facts kama anazo.

Ukitaka kiwanja dodoma sema na wewe, nipo hapa CDA. Kilahali kabisa unapata!

Wabongo bwana, maisha mafupi. Tumieni hela iwazoeee!!
 
Mimi sina tatizo na zitto kujenga hotel dodoma ya 5* la hasha

Kuna siri kubwa sana hapa town viongozi na vigogo hawatumii majina yao kwenye vitega uchumi vyao,wanatumia majina ya watu wa huko vijijin ambao hata hawajulikani sema tu ndugu zao wanafahamishwa mchongo mzima

Mnakumbuka rizmoko alisema yeye ana shamba heka moja tu bagamoyo na kikolola cha kutembelea,je ni kweli? Nani asijua utajiri wa rizmoko?

Kama zitto unajenga kwa fedha yako big up ila kama milungula ya madini haijakaa njema
 
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!

Kwani ni dhambi kwa yeye kujenga?
kwani hizi hotel nyingi zilizoko nchini unajua wamiliki wake?
Labda utuambue kuwa kuna UFISADI Mh.zitto amefanya sehemu iliyompelekea akajenga hiyo hotel ambayo bado tungehitaji utuletee ushahidi.
WanaJF tufike sehemu tuachane na unafiki tufikirie namna ya kulisaidia TAIFA.Kwa sasa Taifa linakabiliwa ba changamoto nyingi mojawapo likiwa ni UKOSEFU WA AJIRA.Ninaposikia mtu anajenga Hotel kubwa kama hiyo ninaona kama ni miongoni wa wakombozi wa taifa letu kwani lazima kuna watu wengi watapata ajira kuanzia ujenzi wa JENGO lenyewe hadi uendeshaji wa hoteli yenyewe.
Hakuna sehemu yoyote iliyoandikwa kwenye sheria zetu za nchi kwamba watu aina ya Mh.Zitto hatakiwi kumiliki hotel ya nyota 5 (labda wanaofahamu sheria zaidi watuambie).
Watu wengine wanahoji eti hizo pesa ametoa wapi,mimi ninaamini kuna njia nyingi za kihalali ambazo angeweza kuzitumia kujipatia pesa na kujenga hiyo hoteli.
Pamoja na kwamba Mh.Zitto amekanusha taarifa hii lakini binafsi ningesema kuwa ANASTAHILI kufanya hivyo maadamu fedha atakazotumia ni za kwake kihali na wala hazihusiani na UFISADI.Jamani tuacheni kuwaogopesha watu hasa vijana aina ya akina Zitto wasifikirie kuwa na maendeleo ya binafsi jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa maisha yake ya baadaye.
 
Kwa sasa hoteli hii imefikia ghorofa ya 3, na inakwenda kwa kasi!....
Tunaandaa picha kamili za nyumba hiyo ili wabishi muone!
N asiku moja tutamphotoa akiwa ameenda kuangalia maendeleo!
Labda amsusie nduguye!


una uhakika na haya usemayo?
 
Kama ukithibitisha kwamba si tu Nina ghorofa Bali kiwanja huko Mbezi Kimara nitakupa wewe. Ninashangazwa sana na uwezo wa kudanganya wa Watanzania.
kaka kama unajenga we jenga....mi mwenyewe na biashara yangu ya mkaa nilipoanza kujenga watu walinisema sana kuwa nimeiba mahali....mjengo ukakamilika na nimehamia....sijawasikia tena....na ni wao hao hao kila siku wanakuja kununua gunia za mkaa hapa....sasa ntashiindwa kujenga kagorofa!!!
 
halafu pale dodoma kuna ndugu yangu pale anaitwa zitto Alphonce..anajenga pale dodoma kigorofa....msichanganye majina nyie....
 
Watanzania tukubali tukatae tuna wivu ..sana.mkapa hakukosea kusema watu wana wivu sana!!.....

Hivi kuna jinai gani kwa Zitto kuchuma mali yake halali ...isitoshe ni kijana ......,nyie ndio kesho na keshokutwa akishuka kisiasa [if that will happen at all] ndio mtaanza kumcheka ....akianza kutembelea feroza au mark two..za milioni 4.......,yaani wabongo mnataka mfanane fanane tu..!! hata vidole havifanani....kwenu ni raha akiwekeza Manji ...ila akiwekeza Zitto ..au hata kudhaniwa basi kosa......tujiangalieni tukiwa na roho za aina hii tukizeeka tutakuwa wachawi....

Mimi namshauri Zitto kuwa kama akipata kipato chake ...asiogope kujiandalia maisha yake kwa ajili maneno ya watu........ni muhimu awe na nyumba Dar,Kigoma Na Dodoma ....na pia ni muhimu kuwa na miradi miwili mitatu tena ya wazi ie Kilimo,usindikaji wa mazao...,stocks etc...kipato cha mbunge si kikubwa au kidogo ..lakini kinatosha kujiandalia maisha......TENA SIKU UKIJALIWA KUWA NA NYUMBA..USIWEKE SIRI PIGA PICHA TUWEKEE HAPA......BAADAYE HAWA NDIO WATAKAOKUCHEKA KUWA ULICHEZEA MAISHA


MSIMAMO WA KIUCHUMI NI MSINGI WA MWANASIASA BORA NA ASIYEYUMBISHWA!!!!
 
halafu pale dodoma kuna ndugu yangu pale anaitwa zitto Alphonce..anajenga pale dodoma kigorofa....msichanganye majina nyie....
Kuna mkakati wa kumchafua Zitto kupitia hulka yake! Kuna muelekeo wa Viongozi wa CDM kushikamana kunako wakosesha usingizi CCM na njia ya pekee ni kumfrastruate Zitto! Walitegemea kumtumia Zitto kirahisi lakini dogo ameshtuka kiaina! Watamchafua sana humu.uzuri Zitto ni mtumiaji mzuri wa mitandao na anaweza kuwakabili humu humu! Kazi kwenu Magamba!
 
Acheni majungu hiyo inayoitwa hoteli ya zitto hata nyota tatu haifikii ni hotel ya kawaida tu ambayo mtu yoyote aliyewekeza kidogo anaweza kupata hizo hela za kujenga.
 
Duh huyu jamaa kakomalia maendeleo ya Zitto, kwani yeye kujenga hotel ni dhambi? mbona mnakomalia isssues zisizokuwa na kichwa wala miguu? una ugomvi na zitto ama? hatuhitaji picha sisi, kama anajenga hayo ni maisha yake binafsi, amekanusha hajengi bado mnakomaa. na amekwambia hana hata kiwanja huko dodoma nenda CDA, na hilo ghorofa la kimara nalo ni nyumba ya kukutisha we Kupeng`e? Mbona kibanda cha kawaida sana ukifananisha na jumba langu, wabongo bwana.mumeiharibu JF, HAIPO KAMA ZAMANI
Kwa sasa hoteli hii imefikia ghorofa ya 3, na inakwenda kwa kasi!....
Tunaandaa picha kamili za nyumba hiyo ili wabishi muone!
N asiku moja tutamphotoa akiwa ameenda kuangalia maendeleo!
Labda amsusie nduguye!
 
i am looking for a joint venture to develop serviced apartments /apart hotel in one of the most prime/plot area in arusha city, all arch drawings are in place
 
ZITTO + JUSSA=ROSTAM...........(1)

if the above formula is correct then why not??

but we ALSO know that ROSTAM=FRAUD..........(2),

HENCE IF WE SUBSTITUTE ROSTAM FROM EQN 1 ABOVE WE GET,

ZITTO + JUSSA=?????????????
 
Zitto mm naamini kabisa atakuwa anajenga, yule ni fisadi mkubwa sana sema watu hawajashtukia kwa kuwa yupo cdm. cku za mbele mambo yote yatakuwa wazi watu mtashangaa

ukiwa mnafiki ujanan,uzeen utakuwa mchawi..Songe mbele Zitto achana na malofa wanayotaka ndoa.Wazush wakubwa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom