Zitto Kabwe Anajenga Hoteli ya Kifahari! [Zitto kafafanua]

Status
Not open for further replies.
Sasa hivi mimi nawaunga mkono mafisadi wote wanaoliibia taifa hili na kuwekeza hapahapa nchini ili ile ahadi ya JK ya ajira kwa vijana itimie!
 
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!
Mi nadhani ujenge hoja ili achunguzwe kama una wasiwasi naye.
 
Kwani Zitto akijenga hotel kuna ubaya gani? Zitto ndo kwanza anajenga, hao mafisadi waliokwishajenga na wameandika majina ya watoto wao mbona hamsemi, kuna watu wana vituo vya mafuta na masemi trela nchi nzima mbona hamsemi? Leo Zitto kujenga imekuwa nongwa,Zitto hapaswi kuwa na maendeleo? Zito ni mtu kama mimi na wewe tunaosaka maendeleo.

Jenga Zitto, ukimaliza hiyo ya Dodoma kajenge ya nyota 3 Kigoma
 
Umbea mwingine bana.. Zitto wewe kaza buti kuna mahali unaelekea utafika tu hapo ulipo bado achana na kelele za mtaani..
 
inakuhusu nini mbona mimi ninazo mbili za nyota Tano wacha nae ajenge umeshindwa kufight maisha kivyako unaanza kuingilia maisha ya Zito.....Nyambafu yako
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wakuu, taarifa hizi ni za Uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa Zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!

Tatizo hapo ni nini hasa?
 
Hii hoja nilileta mwaka jana mod wakainyofoa

ilikuwa lile ghorofa lake la mbezi ya kimara nitaweka picha soon
 
Kwani nae anapesa haramu kama mafisadi? Kama hana pesa haramu basi hongera zake.
 
Kwani Zito haruhusiwi kujiendeleza? Sidhani kama kuna anayekatazwa kumiliki mali au kuendeleza nchi yake kwa vitega uchumi. Sie tunakataa fedha haramu. Zito kama mtanzania na kijana mwenye nguvu, akili, maarifa na mchapakazi anaweza kujipatia fedha halali na kujiendeleza. Natumaini ni fedha halali hivyo mwenye mada kama anajingine atuambie ila kama ni kujenga tu hoteli sio habari.
 
Hii ni ya mbezi kimara

images
 
inakuhusu nini mbona mimi ninazo mbili za nyota Tano wacha nae ajenge umeshindwa kufight maisha kivyako unaanza kuingilia maisha ya Zito.....Nyambafu yako

Yanini kuandikia mate...?? tupe majina tukupe tenda fasta...
 
Ushahidi uweke basi ili mjadala uende vizuri..
Sioni tatizo lolote la Zitto kujenga hiyo hotel, huenda kakopa benki..
Kizuri zaidi ni kuwa yeye katofautiana na kina mkaa hapa wanaokwenda kuwekeza aka kuficha hela zao ughaibuni kisha kuwaomba hao wa ughaibuni waje kuwekeza huku hahaaaaaaa ila usikute mleta mada ndiye zito mwenyewe anapima upepo manake hiyo heading nzito kuliko habari yenyewe
 
Wakati mwingine uongo na uzushi wa kipuuzi Kama huu ukiachwa kuna watakaoamini. Sio tu kujenga Hotel, sina hata kiwanja Dodoma. Sitegemei kuwa na kiwanja Dodoma wala kujenga Dodoma.

Nimezushiwa mengi sana

1. Nina nyumba Masaki

2. Nina 900m StanBic

3. Nina kiwanda cha kokotoNa mengine mengi sana.

Yote hayo sio ya kweli na kuna watu wanayaamini.

1. Sina biashara yeyote hapa Tanzania

2. Sina nyumba yeyote Dar. Nina shamba la Ekari tatu tu Mbutu na halijaendelezwa toka mwaka 2004.

3. Ninaishi flats za kupanga Tabata

4. Sina na wala sijwahi kuwa na tamaa ya utajiri katika maisha yangu. Property isn't my thing kabisa.JFMtu akileta accusations dhidi ya mtu mwingine tafadhali aje na ushahidi wa mfano picha ya nyumba, ushahidi wa umiliki ambao ni rahisi sana kupata CDA kwa DODOMA au Wizara ya Ardhi.

Tuache umbeya tuseme kweli. Sikatai Kusemwa kwa ya kweli. Ninajifunza sana kwa critics za ukweli. Lakini uzushi Kama huu unaumiza

Kila la kheri
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom