Siasa za wastani za Zitto Kabwe, ni tishio kwa ustawi wa ACT Wazalendo

El Roi

JF-Expert Member
May 29, 2020
263
502
Kuna usemi usemao" usilizunguke bomu, bali pita katikati yake mapema ili lilipuke mapema wakati huo, kukusaidia lisije kuangamiza watu wengi zaidi baadae ambao hawataliona iwapo litalipuka"

Maana ya usemi huo ni katika kusaidia kujenga dhana tu kwamba" usikwepe kushughulikia tatizo unaloliona wakati fulani, ukaliacha kwa sababu yoyote ile, maana baadae litakuwa tatizo kubwa zaidi.

Zitto zuberi kabwe, ni kiongozi na kijana mwenye uelewa wa mambo ( namuita kijana kwa sababu ni mdogo kwangu kwa umri), amesheheni exposure ya vitu vingi na kweli ni born politician. Kuna tatizo ambalo zitto alilikwepa na nionavyo litaangamiza chama chake na hata yeye mwenyewe kisiasa.

Tabia ya kukwepa kuusema ukweli na kutoungana na wanaousema ukweli Ili aonekane he is politically right, Sasa unamgharimu yeye na chama chake.

Katika harakati za kutaka kuleta usawa wa kidemokrasia na chaguzi huru nchini, wengine tusio wanasiasa za majukwaani (non active politicians) tulitegemea Zitto kabwe kama mmoja wa wanasiasa ambao ni figure head angeungana na wenzake wa vyama makini kama Chadema kupinga michakato iliyoanzishwa na serikali ambayo kiuhalisia ilikuwa na mambo ya wazi kabisa yaliyopaswa kupingwa at the word go kabla ya hatua yoyote.

Ajabu Zitto Zuberi Kabwe, katika maoni yake alionekana kupingana kabisa na wanamageuzi wenzake na akakubali michakato ambayo ilikuwa inawanyonga hadharani na akajinasibisha na waleta mabadiliko yasiyo hasa. ( Superficial change).

Nakumbuka nikimsikia akisema" Kila watu Wana namna yao ya kufanya siasa, " siyo lazima upate Kila kitu" yeye amechagua siasa za majadiliano " nk. Hizi ni lugha za mtu niliyemsikia ambaye alitaka kuonekana he was politically right".

Hilo ni kosa ambao analifahamu na analizunguka. Kwa vyama vya kiafrika ambavyo vimeshalewa madaraka na kuishi kwao ni madaraka, ni vyema kujifunza kuwa mkweli hata kama utaoneka uko irrevant na wengine.

Zitto pamoja na umahiri wako, political relevancy ndo Ina wagharimu muda huu.

Kwa upande wa Zanzibar, nimewasikia wanataka kujitoa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa. Madai yao yakiwa hawatendewi haki na makubaliano yao ya awali yamekiukwa!

Swali ni " hivi kweli ACT hawakuelewa kwamba CCM ni very tricky na isingeweza kuwapa nafasi sawa na maridhiano yao?

Ina maana miaka hii yote hawaijui CCM na mbinu zake za kukaa madarakani daima dumu? . Kutaka kuonekana waungwana hata pale kusikotakiwa ndo kunawagharimu Sasa hivi.

Walikuwa na haki ya kukataa kuwa kwenye serikali hiyo kwa sababu za kiuchaguzi zilizokuwa zimepita. Kupigwa watu, kuvunjwa kwa kina Jussa, nk. Lakini kwa kupenda kuonekana politically civilized walikubali serikali ya mseto na mmoja wa wahanga wakubwa wa mateso na vipigo ni waziri kwenye serikali hiyo. Some body mazurui.

Unapata wapi gutts za kulalamika wakati wewe ndo huwa wa kwanza kuendeleza mambo yasiyo sawa badala ya kuyapinga kwa sababu tu wanaopinga huwapendi hata kama wako sahihi?

Inawezekana Zitto anakwepa kuwaunga mkono Chadema katika mambo mengi kwa sababu ya uadui wa asili uliopo kati yao, lakini akumbuke ukweli ni ukweli tu hata kama unatoka kwa mtu usiyempenda.
" Injustice somewhere is injustice everywhere". Hakuna sababu ya ku compromise na watu ambao unajua kwa hakika ni marafiki bandia, bora ungesimama na adui anaeujua ukweli.

Nimesikia malalamiko ya ACT baada ya kushindwa vibaya na CCM kwenye viti vya marudio ya udiwani. Wamechinjiwa baharini ile mbaya. Walitegemea Nini?

CCM ni rafiki yako tu nje ya box la kura. Kukiwa na kura hata ya mjumbe wa serikali ya mtaa, huwa hawaangalii mtu usoni.

ACT wanakula matunda ya siasa za Zitto za maridhiano hewa, kupenda kuonekana wastaarabu wa siasa, na kujitenga na wanaousema ukweli kwa sababu ya upinzani wa asili ( arch rivalry na Chadema).

Ni mpaka ACT watakaporudi na kuwa resistant ndipo watakaporudi kwenye ulingo halisi wa siasa makini.

Najua Zitto siyo kiongozi tena wa ngazi ya kitaifa. Nashauri viongozi wa Sasa wafanye siasa hasa na kuwa objective kwa maana ya kuwa on fire badala ya ku compromise na watawala Ili kupata political mileage isiyosaidia ujenzi wa jamii Pana na maslahi makubwa ya umma.
 
Back
Top Bottom