Zitto Kabwe Anajenga Hoteli ya Kifahari! [Zitto kafafanua]

Status
Not open for further replies.
Hakika siamini kama mtu anaweza kuiruka property yake mchana kweupe kiasi hiki!...Siku tukileta ushahidi nasikitika tutaweka wapi sura zetu!...
 
Kwa sasa hoteli hii imefikia ghorofa ya 3, na inakwenda kwa kasi!....
Tunaandaa picha kamili za nyumba hiyo ili wabishi muone!
N asiku moja tutamphotoa akiwa ameenda kuangalia maendeleo!
Labda amsusie nduguye!

muje na hati au uthibitisho unaonesha ni mali ya zitto,km kusemekana hata mama yako inasemekana anatembea na house boy wenu
 
Baaada ya miaka 20...................Gazeti la Tanganyika Daima litaandika hivi: Aliyekuwa Mbunge wa Kigoma kaskazini Zitto Kabwe amefulia kabisa na wala hana mahali pa kuishi. Inasemekana wakati wa Ubunge wake alikuwa anapata pesa nyingi sana za posho na mshahara wa Bunge kuweza kujenga hata hoteli za ghorofa tano katika prime areas, lakini badala yake yeye alikuwa akitumbua tu. Hivi sana anahangaika kwani kibanda chake pale Golani kimewekewa X kupisha upanuzi wa barabara.

Wanaomponda Zitto leo ''kujenga'' hiyo hotel ndo watakuwa wa kwanza kumponda wakati huo. Bro kama unapata pesa yako wewe jenga tu, umaarufu ulionao na pesa unayopata huwezi kukosa mkopo wa kujenga ghorofa. Isitoshe unaweza kuwa unachukua vifaa vya ujenzi kwa mali kauli hadi ghorofa liishe.

Hii sio habari kabisa, labda mtoa habari angekuwa na ushahidi kuwa fisadi fulani ndo anamjengea Zitto hilo ghorofa.................otherwise tumuache kijana wa watu kila siku ni kumuandika vibaya tu, kweli hana hata jema moja tukaliandika humu?
 
Kwanini watu tunabisha tu, bila hata kufanya uchunguzi?
Kosa la kwanza la Zitto amebisha na kukana!...Nyie members mnasema kuwa ni halali tu kwake kuwa na nyumba ya aina hii!...Sasa baada ya yeye kukana mlitakiwa muende kwenye hatua ya pili ya kufanya uchunguzi ili kuudhalilisha uongo(Aidha wa Mleta mada, au wa Zitto)!
Fanyeni uchunguzi wazee, watu wa Dodoma waende pale kuchunguza watapewa details!..Mbinu zetu waandishi huwa tunatumia gharama yoyote kupata habari toka kwenye source...msiwe wagumu, tumieni means yoyote, mtapewa full habari!
 
Hakika siamini kama mtu anaweza kuiruka property yake mchana kweupe kiasi hiki!...Siku tukileta ushahidi nasikitika tutaweka wapi sura zetu!...

Ameshakwambia ukiweza thibitisha kuwa ya kwake ANAKUPATIA WEWE NYUMBA HIYO NA KIWANJA CHAKE. Changamkia tenda hiyo mkuu acha kulalalama tu humu!!
 
Watanzania tukubali tukatae tuna wivu ..sana.mkapa hakukosea kusema watu wana wivu sana!!.....

Hivi kuna jinai gani kwa Zitto kuchuma mali yake halali ...isitoshe ni kijana ......,nyie ndio kesho na keshokutwa akishuka kisiasa [if that will happen at all] ndio mtaanza kumcheka ....akianza kutembelea feroza au mark two..za milioni 4.......,yaani wabongo mnataka mfanane fanane tu..!! hata vidole havifanani....kwenu ni raha akiwekeza Manji ...ila akiwekeza Zitto ..au hata kudhaniwa basi kosa......tujiangalieni tukiwa na roho za aina hii tukizeeka tutakuwa wachawi....

Mimi namshauri Zitto kuwa kama akipata kipato chake ...asiogope kujiandalia maisha yake kwa ajili maneno ya watu........ni muhimu awe na nyumba Dar,Kigoma Na Dodoma ....na pia ni muhimu kuwa na miradi miwili mitatu tena ya wazi ie Kilimo,usindikaji wa mazao...,stocks etc...kipato cha mbunge si kikubwa au kidogo ..lakini kinatosha kujiandalia maisha......TENA SIKU UKIJALIWA KUWA NA NYUMBA..USIWEKE SIRI PIGA PICHA TUWEKEE HAPA......BAADAYE HAWA NDIO WATAKAOKUCHEKA KUWA ULICHEZEA MAISHA

MSIMAMO WA KIUCHUMI NI MSINGI WA MWANASIASA BORA NA ASIYEYUMBISHWA!!!!
Mkuu wangu unajua sasa hivi Tanzania tupo ktk njia panda. Ukiwasoma sana Watanzania utajua ya kwamba wana shida kubwa ya kiongozi Mwanamapinduzi mfano wa kina CHE, Chavez au Kagame na ktk sifa za mtu kama huyu mara zote hazitokani na mtu mwenye mtazamo wa Kibepari isipokuwa Mjamaa, na ktk Ujamaa ni swala la Kimaskini ambalo lazima kiongozi atazame na kusimamia maslahi yao..

Hivyo wakiona mtu kama Zitto amejenga Hotel na Ghorofa humwondoa ktk kundi la Wanamapinduzi..Mtu kama Mkapa ni Bepari na kila anachokitaza ni ktk Ubepari hivyo hata Ufisadi haoni haramu isipokuwa ni disdvantage zinazokuwepo ktk Ubepari lazima tuzikubali..ndio maana alisisitiza wivu kwa mtazamo wa kibepari..Na hili ndilo tatizo kubwa sana ktk vyama vyetu ambavyo unawakuta viongozi wameridhika na mfumo wa Ubepari lakini wakati huo huo wanapinga mtu kujilimbikiza mali hata kama analipa kodi zake..

Kwa hiyo kuna mchanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini, kina sisi tunasubiri mageuzi kupitia Mapinduzi ya kifikra na wapo wengine wanategemea mageuzi kupitia samnduku la kura na wengine wanamtafuta mwokozi wao mwanamapinduzi Che ambaye hadi leo hajapatikana. Na nakuhakikishia kama atakuja tokea mtu yeyote kutetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi kwa njia ya Mapinduzi ya Kiuchumi kifikra, basi huyu mtu atakuwa maarufu na ndiye pekee atakae weza kuiondoa CCM madarakani na sio kupitia sanduku la kura.. Mark my word!
 
Sasa mbona gorofa moja na ni nyumba ya kawaida kuliko maneno uliyo kuwa ukisema!! Mbongo kweli nuksi

Wakuda wengine pumba tupu!

Yaani hata ako ka- resedential flat unakasemea kwa status ya Zito! we kweli mchovu!

Ebana jenga mbona awesemi vya upande wa pili ambavyo tunadata nzuri tu! lkn kwa kua ni personal twakaa kimya!

Wewe ulieleta picha ondoa uchovu wako humu.
 
Mkuu wangu unajua sasa hivi Tanzania tupo ktk njia panda. Ukiwasoma sana Watanzania utajua ya kwamba wana shida kubwa ya kiongozi Mwanamapinduzi mfano wa kina CHE, Chavez au Kagame na ktk sifa za mtu kama huyu mara zote hazitokani na mtu mwenye mtazamo wa Kibepari isipokuwa Mjamaa, na ktk Ujamaa ni swala la Kimaskini ambalo lazima kiongozi atazame na kusimamia maslahi yao..

Hivyo wakiona mtu kama Zitto amejenga Hotel na Ghorofa humwondoa ktk kundi la Wanamapinduzi..Mtu kama Mkapa ni Bepari na kila anachokitaza ni ktk Ubepari hivyo hata Ufisadi haoni haramu isipokuwa ni disdvantage zinazokuwepo ktk Ubepari lazima tuzikubali..ndio maana alisisitiza wivu kwa mtazamo wa kibepari..Na hili ndilo tatizo kubwa sana ktk vyama vyetu ambavyo unawakuta viongozi wameridhika na mfumo wa Ubepari lakini wakati huo huo wanapinga mtu kujilimbikiza mali hata kama analipa kodi zake..

Kwa hiyo kuna mchanganyiko mkubwa wa kisiasa nchini, kina sisi tunasubiri mageuzi kupitia Mapinduzi ya kifikra na wapo wengine wanategemea mageuzi kupitia samnduku la kura na wengine wanamtafuta mwokozi wao mwanamapinduzi Che ambaye hadi leo hajapatikana. Na nakuhakikishia kama atakuja tokea mtu yeyote kutetea maslahi ya Wakulima na Wafanyakazi kwa njia ya Mapinduzi ya Kiuchumi kifikra, basi huyu mtu atakuwa maarufu na ndiye pekee atakae weza kuiondoa CCM madarakani na sio kupitia sanduku la kura.. Mark my word!

10/10.
Ndio maana mie huwa nasisitiza tatizo la Tz sio ccm, tatizo la tanzania ni watanzani. Binafsi nikiandika hivyo, hua naona majibu wanayorudisha wadau huonekana ni senteso ngumu sana isiyoeleweka.
 
Wakuu, taarifa hizi ni za Uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa Zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!

Kama jina lako na uwezo wako wa kufikiri ndio ulipofikia
 
Hakuna mwanasiasa masikini au mtu mwenye mwanya wa kuwa tajiri akaamua kuishi umaskini, labda wale tu kwa tabia zao na kwa makusudi wanauchukia utajiri kama alivyokuwa Baba wa Taifa.

Nimewahi kuwaona watu wawili kwa makusudi binafsi hawapendi utajiri japo wakiamua wanaweza kuwa matajiri na kuishi maisha ya kitajiri. Huenda wapo wengine lakini hawa wameamua kuishi maisha ya kawaida.

1. Fr. Riccardo Riccioni (Mtaliano) - Maarufu Morogoro kama Mzungu Peku.

2. Mh. John John Mnyika - Mbunge wa Ubungo CHADEMA.

Kama unawajua wengine ongeza, sioni ajabu kwa Zitto ni kama wanasiasa wengine tusimchafue.
 
Zitto mm naamini kabisa atakuwa anajenga, yule ni fisadi mkubwa sana sema watu hawajashtukia kwa kuwa yupo cdm. cku za mbele mambo yote yatakuwa wazi watu mtashangaa

Eti kwa kua yuko CDM what a weak contribution! unamanisha CDM awajengi? kilaza kweli wewe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom