Zitto Kabwe Anajenga Hoteli ya Kifahari! [Zitto kafafanua]

Status
Not open for further replies.

Mbwiga_Plus

Senior Member
Jan 5, 2011
163
42
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!

Wakati mwingine uongo na uzushi wa kipuuzi Kama huu ukiachwa kuna watakaoamini. Sio tu kujenga Hotel, sina hata kiwanja Dodoma. Sitegemei kuwa na kiwanja Dodoma wala kujenga Dodoma.

Nimezushiwa mengi sana

1. Nina nyumba Masaki

2. Nina 900m StanBic

3. Nina kiwanda cha kokotoNa mengine mengi sana.

Yote hayo sio ya kweli na kuna watu wanayaamini.

1. Sina biashara yeyote hapa Tanzania

2. Sina nyumba yeyote Dar. Nina shamba la Ekari tatu tu Mbutu na halijaendelezwa toka mwaka 2004.

3. Ninaishi flats za kupanga Tabata

4. Sina na wala sijwahi kuwa na tamaa ya utajiri katika maisha yangu. Property isn't my thing kabisa.

JF Mtu akileta accusations dhidi ya mtu mwingine tafadhali aje na ushahidi wa mfano picha ya nyumba, ushahidi wa umiliki ambao ni rahisi sana kupata CDA kwa DODOMA au Wizara ya Ardhi.

Tuache umbeya tuseme kweli. Sikatai Kusemwa kwa ya kweli. Ninajifunza sana kwa critics za ukweli. Lakini uzushi Kama huu unaumiza

Kila la kheri
 
Wanajamvi,

Nimepigiwa simu na Ndugu yangu anayeishi Dodoma mjini akinihabarisha kuwa Mheshimiwa Zitto Kabwe anajenga Hoteli kubwa sana ya Nyota 5 Mjini Dodoma, eneo liitwalo KISASA.

Hili ni jambo jema na la maendeleo sana, lakini Je Zitto, hili jambo ni kweli?
Umekuwa unapinga hata kuwa na magari ya kifahari, huku ukisema kuwa hushabikii UTAJIRI, je fedha za kupandisha jengo kubwa na la kifahari kama hilo ni hizihizi za posho zenu, au umekopa benki, au umepewa na mfadhili, au una vyanzo vingine vilivyofichama?

Tafadhali sana Zitto, njoo ujibu kwa kauli yako mwenyewe!

Nawasilisha!

Nimepata mshangao japokuwa Zitto kama mtu anayo haki ya kuwa na maendeleo .Lakini sasa nyota 5 ?Zitto naamini atakuja kusema hapa tumpomgeze kama ni kweli mie naona ni maendeleo .
 
Wakuu, taarifa hizi ni za Uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa Zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!
 
Zitto anawanyima sana usingizi watu wenya ''dada'' zao wasaka ndoa........go Zitto go
 
post zisizokuwa na evidence zinapoteza mvuto wa kuchangia,tupia ushahidi

Mimi ili nikubaliane na hii issue kuna jina limetajwa kisasa huko dodoma je ni kweli eneo hilo lipo ? Na je kuna ujenzi wa hotel unafanyika kwa sasa ?Tuanzie hapa but again nampongeza Zitto kama anajenga .
 
Duh chanzo cha habari utata mtupu cha kushangaza na kusikitisha zaidi tuhuma nzito kama hizi hata ka-picha ka jengo kwa kutumia simu ya Mchina nalo limeshindikana?
 
Zitto nakuombea kwa Mola maliza haraka sana hiyo Hoteli mimi ni mdau wa utalii nitalaza wageni wangu hapo baba!
 
ZITTO + JUSSA=ROSTAM

if the above formula is correct then why not??
 
Bora lipi? Kumalizia pesa kwa kuokoteza machangudoa pale mitaa ya sabasaba au abane matumizi afanye kitu cha kueleweka kutokana na pato lake? Zito anayo haki ya kuweka kitega uchumi chake kama nafasi na uwezo unamruhusu, na ni wakati mwafaka, asipofanya ssa atakuwa amechelewa. Big up Zito, go ahead.
 
Wakuu, taarifa hizi ni za Uhakika kabisa, maana mleta habari anaelewa kwa undani ishu nzima...
Kwa Zitto hili ni jambo rahisi tu, aeleze wanajamvi kama ni hoteli yake ya kihalali...basi!
Ushahidi uweke basi ili mjadala uende vizuri..
Sioni tatizo lolote la Zitto kujenga hiyo hotel, huenda kakopa benki..
 
Hii thread nayo itaunganishwa kama ileeee ya siku ileeee kwa hoja kwamba habari za Zitto ni nyingi mno humu na watu wamem discuss sana!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom