Yanayojiri Uchaguzi Mkuu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo 2023: Felix Tshisekedi atangazwa Mshindi wa Urais

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1703826151095.png


SERIKALI YAKATAA KURUDIA UCHAGUZI LICHA YA WAANGALIZI KUDAI KUNA UDANGANYIFU

Kauli ya Serikali inakuja huku kukiwa na shinikizo la Wafuasi na Viongozi wa Upinzani kutaka Uchaguzi huo ufutwe kutokana na madai ya kuwepo kwa ukiukwaji wa Sheria na Uwazi ikiwe baadhi ya Vituo kutopiga Kura.

Ripoti kutoka nchini humo zinadai baadhi ya maeneo yamekuwa na vurugu kati ya Askari wa Kutuliza Ghasia na Wananchi wanaoandamana kutaka marudio ya Uchaguzi ambao hadi sasa unampa nafasi ya Ushindi Rais Felix Tshisekedi ambaye anatajwa kuwa na 77% ya Kura Milioni 9.3 zilizohesabiwa.

Hata hivyo, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI), inadaiwa kutoweka wazi idadi ya waliopiga Kura kati ya Milioni 44 waliojiandikisha na waliojitokeza kushiriki zoezi hilo. Inaelezwa kuwa baadhi ya watu wameanza kuhofia Taifa hilo kurejea kwenye machafuko ya kisiasa endapo uchaguzi huo hautamalizika kwa amani.

Polisi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kinshasa imewazuwia waandamanaji kukusanyika siku ya Jumatano 27/12/2023, baada ya kuandamana dhidi ya uchaguzi wa hivi karibuni katika taifa hilo tete la Afrika ya Kati.

Wanasiasa wakuu wa upinzani waliitisha maandamano hayo baada ya kukataa kura ya wiki iliyopita, ambayo ilikumbwa na ucheleweshaji mkubwa na mtafaruku wa ukiritimba.
Wapinzani watano, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa Gavana wa Mkoa Moise Katumbi, walisema Jumamosi kwamba kura hiyo haipaswi kuthibitishwa kwani ilikuwa imeharibiwa na "udanganyifu mkubwa."

Viongozi wengine watano wa upinzani, ikiwa ni pamoja na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Denis Mukwege na aliyekuwa mtendaji wa mafuta Martin Fayulu, wametoa wito wa maandamano dhidi ya matokeo Jumatano ijayo.

"Tutapinga dhidi ya irregula zilizobainika wakati wa shughuli za kupiga kura," walisema katika barua kwa gavana wa Kinshasa, ambapo wanapanga kukusanyika.

MATOKEO YA AWALI YAANZA KUTANGAZWA

Matokeo ya awali ya kura ya urais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yalianza kuingia taratibu siku ya Ijumaa baada ya uchaguzi uliogubikwa na misukosuko kwenye baadhi ya maeneo nchini humo ambapo mamlaka zilitangaza kuwa uchaguzi huo umemalizika vizuri

Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ceni, ilitangaza matokeo kwa wapiga kura wa Kongo wanaoishi Afrika Kusini, Ubelgiji, Ufaransa, Canada, na Marekani.

Matokeo haya yanawakilisha sehemu ndogo sana ya kura zote zilizopigwa, lakini yalionyesha Felix Tshisekedi, anawania kuongoza kwa muhula wa pili anaongoza kwenye matokeo hayo.

Ucheleweshwaji mkubwa na urasimu ilisababisha baadhi ya vituo kuchelewa kufunguliwa huku vingine kutofunguliwa kabisa, ambapo Ceni iliongeza muda wa kupiga kura kwenye baadhi ya maeno mpaka Alhamisi

Tume ya uchaguzi ilitoa taarifa kuwa hakuna kituo cha kupigia kura kilichoruhusiwa kufunguliwa siku ya Ijumaa.

Kucheleweshwa kwa kiasi kikubwa na machafuko ya utaratibu yaliharibu uchaguzi na baadhi ya vituo vya kupigia kura vilishindwa kufunguliwa kabisa.

Ceni iliongeza muda wa kupiga kura katika baadhi ya maeneo hadi Alhamisi.

Kupitia taarifa, tume ya uchaguzi ilisema hakuna kituo cha kupigia kura kilichoruhusiwa kufunguliwa siku ya Ijumaa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa maafisa, upigaji kura uliendelea kwenye maeneo ambayo hasa yako mbali na mji siku ya Ijumaa

Mfano wananchi wa Kilembwe, katika eneo la Fizi jimbo la South Kivu, mashariki mwa nchi hiyo, walipiga kura kwa kuchelewa sana baada ya vifaa kuwasili kuchelewa siku ya Alhamisi.

Ceni inatarajiwa kuanza kutangaza matokeo ya awali kwenye majimbo 26 ya DRC leo Jumamosi 23/12/2023

22/12/2023 - MATOKEO YA UCHAGUZI KUTANGAZWA HATUA KWA HATUA
Tume Huru ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo - CENI imesema itaanza kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano, hatua kwa hatua.

Tangazuo hilo linatolewa licha ya malalamiko makubwa kutoka wagombea wa upinzani, na wadau wengine waliochunguza mwenendo wa uchaguzi huo, ambao wanasema umekuwa na hitilafu chungu nzima.

Mmoja wa maafisa wakuu wa CENI Didi Manara amesema matokeo ya awali yataanza kuchapishwa leo Ijumaa. Huku matokeo rasmi yakitarajiwa kutangazwa mapema na Mahakama ya Kikatiba mapema Januari 2024.

21/12/2023 MABOXI YALIYOKWISHAPIGIWA KURA WAKATI ZOEZI LA KUPIGA KURA LIKIENDELEA YAKAMATWA




1703243429736.jpeg

Mjini Mbujimayi, karatasi ya matokeo iliyoonyeshwa katika Kituo cha Kupigia Kura 8011051-C inaonyesha wapiga kura 742, wote wakimuunga mkono mgombea Félix Tshisekedi, kati ya wapiga kura 704 waliojipanga kwenye orodha. Kiwango cha ushiriki kinaonyesha 105.40%

20/12/2023 - WAGOMBE WA UPINZANI KONGO WALALAMIKIA DOSARI ZA UCHAGUZI

Wagombea wakuu wa upinzani katika uchaguzi wa rais unaofanyika leo nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wamesema raia wengi wameshuhudia mparaganyiko na dosari nyingi vituoni walipokwenda kupiga kura.

Akizungumza baada ya kupiga kura mjini, Kinshasa, mwanasiasa wa upinzani Martin Fayulu amelalamika dhidi ya kile alichokieleza kuwa ni kukosekana "utaratibu mzuri" vituoni na kuutuhumu upande wa chama tawala kula njama za kuiba kura.

"Hivi sasa (kambi ya rais) imejiandaa kufanya udanganyifu. Nimewaambia watu wa Kongo, hakuna uchakachuaji safari hii, na kama mtu atajaribu kupora ushindi wetu, ibara ya 64 ya katiba ipo, na tutateremka mitaani kudai ushindi wa umma," alisema Fayulu.

Madai ya dosari vituoni yametolewa pia na wagombea wengine ikiwemo Denis Mukwege na mwanasiasa kigogo Moise Katumbi anayetazamiwa kutoa upinzani mkali kwa Rais Felix Tshisekedi anayewania muhula wa pili.

Zaidi ya wapiga kura milioni 44 wamesajiliwa kushiriki zoezi hilo la kidemokrasia la kumchagua rais, bunge la taifa, mabunge ya mikoa na madiwani.

========

20/12/20223 - MUDA WA ZOEZI LA KUPIGA KURA WAONGEZWA

1703136648184.png

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imelazimika kuongeza muda zaidi wa kupiga Kura baada ya Malalamiko mengi kuonesha kulikuwa na ucheleweshaji katika zoezi la kufungua Vituo vya Kupigia Kura katika maeneo mengi.

Hali hiyo imedaiwa kuanza kuibua hisia za Vurugu kwa baadhi ya Wananchi huku Wagombea wa Upinzani wakidai ni njama za Chama Tawala kutaka kushinda Uchaguzi kwa mbinu za wizi wa Matokeo au kuvuruga uwazi katika zoezi hilo.

Takriban Watu Milioni 44 wanatarajiwa kupiga Kura katika Uchaguzi huo ingawa takwimu zinaonesha idadi kubwa ya Watu katika baadhi ya maeneo imeyakimbia Makazi yao kutokana na Mapigano ambayo yalisababisha Watu Milioni 1.5 kushidnwa Kujiandikisha.

AL Jazeera
===============

MAMBO YA KUFAHAMU KUHUSU UCHAGUZI MKUU WA DR - CONGO DESEMBA 20, 2023


Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inatarajia kufanya Uchaguzi wa Mkuu hapo Desemba 20, huku Rais Félix Tshisekedi akitafuta nafasi ya kuongoza kwa muhula wa pili, na wa mwisho, wa miaka 5 madarakani

Takriban Watu Milioni 40 kati ya Raia zaidi ya Milioni 102 wanatarajiwa kupiga Kura kutoka Taifa hilo kubwa zaidi katika eneo la Jangwa la Sahara lenye utajiri wa Madini yenye Thamani Kubwa

KWANINI UCHAGUZI HUU NI MUHIMU?

DRC ndio makazi ya 70% ya Madini ya Coltan yanayotumiwa katika uundaji wa Simu za Mkononi, 30% ya Almasi inayouzwa duniani kote na madini mengine mengi

Licha ya Utajiri huo mkubwa wa Maliasili, Congo inatajwa kuwa kati ya Nchi zilizoshindwa kutumia rasilimali zake katika kuboresha Maisha ya Wananchi. Sababu kuu ni Machafuko ya Kivita, Rushwa pamoja na Utawala Unaoyumba kila wakati

Inakadiriwa kuwa tangu mwaka 2008, takriban watu Milioni 5.4 wamepoteza maisha kutokana na Mapigano, Njaa na Magonjwa ya Mripuko. Hata hivyo, idadi hiyo inaweza kuwa chini au zaidi

NANI WANAGOMBEA URAIS?

Hadi sasa Wagombea waliobaki ni 20 huku 6 wakijiondoa akiwemo aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Augustin Matata Ponyo

WANAOTAJWA KUWA NA USHAWISHI ZAIDI

Mbali na Rais Felix mwenyewe, wagombea wengine wenye nguvu zaidi ni:

1. Martin Fayulu ambaye alitajwa kuwa mshindi wa Urais katika Uchaguzi wa mwaka 2018, ingawa alitajwa kuwa wa pili katika Matokeo, anapewa nafasi zaidi katika Uchaguzi huo

2. Anayefuatia ni Moïse Katumbi, Mfanyabiashara na Gavana wa zamani wa Jimbo la Katanga na Mmiliki wa Klabu ya Mpira wa Miguu ya TP Mazembe

3. Mwingine ni Dkt. Denis Mukwege, Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kwa mwaka 2018 kutokana na Kazi za kutetea haki za Waathirika wa Vitendo vya Ubakaji

Wagombea 4 kati ya 6 waliojiondoa, wameonesha kumuunga mkono Mfanyabiashara Katumbi. Wengine wawili wanamuunga mkono Rais Felix

GHARAMA ZA UCHAGUZI

Wagombea wote walilazimika kulipa faranga za Kongo Milioni 160 (Takriban Tsh. Milioni 151,112,340) ili kulipia ada ya Fomu ya maombi. Kumbuka pesa hii hairejeshwi hata ikitokea umejiondoa au umekatwa na Wajumbe

UTARATIBU WA UCHAGUZI

Mgombea yeyote atakayepata idadi kubwa ya Kura kuzidi wengine, atakuwa Mshindi wa Urais hata kama asipofika 50% ya Kura.

Hakutakuwa na Uchaguzi wa Marudio

Uchaguzi unafanyika Siku 90 kabla ya muda wa Rais aliyeko madarakani kumalizika. Uchaguzi wa mwaka huu unajumuisha Wabunge, Madiwani na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa

MASUALA GANI YANATAJWA KWENYE KAMPENI?

Congo inafanya Uchaguzi wakati Hali ya Uchumi ikitajwa kuzidi kuzorota, Sarafu yake imeporomoka kwa 15% hadi 20% dhidi ya Dola ya Marekani

Zaidi ya 65% ya Wananchi wanaishi katika mazingira ya Umasikini kipato chao kikiwa chini ya Dola 2.5 au chini

MATOKEO YATATANGAZWA LINI?

Kalenda ya Tume ya Uchaguzi inaonesha Matokeo yote yatakuwa hadharani kufikia Desemba 31, 2023.

Kama kila kitu kitaenda kama ilivyopangwa, Rais Mteule ataapishwa rasmi Januari 20, 2024


 

Attachments

  • DRC Election.png
    DRC Election.png
    6.8 KB · Views: 5
Taarifa za awali zisizo rasmi za uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa DRC uliyofanyika hivi karibuni unaonysha tajiri Moise Katumbi anaongoza kwa 63.3% ya kura dhidi ya rais anayemaliza muda wake Felix Tshisekedi mwenye 21% ya kura

Chanzo cha habari hiyo ni shirika la habari la rtnc.
 

Attachments

  • IMG-20231223-WA0001.jpg
    IMG-20231223-WA0001.jpg
    60.7 KB · Views: 2
Taarifa za awali zisizo rasmi za uchaguzi mkuu wa rais na wabunge wa DRC uliyofanyika hivi karibuni unaonysha tajiri Moise Katumbi anaongoza kwa 63.3% ya kura dhidi ya rais anayemaliza muda wake Felix Tshisekedi mwenye 21% ya kura

Chanzo cha habari hiyo ni shirika la habari la rtnc.
DRC mpaka Diaspora wanapiga kura ila Tanzania marufuku.Nchi ya kibwege sana hii!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Tanzania sijui ni lini tutakuwa na tume huru ya uchaguzi.
Pamoja na matatizo la tume huru lakini wagombea wa vyama vya upinzani nalo ni tatizo lingine.

Siku vyama vya upinzani wakipata akili ya kushawishi viongozi wenye majina toka CCM na wakawasimamisha kuwa wagombea urais ndiyo siku kitatokea kifo cha CCM. Kwa sababu hiyo itasababisha mgawanyiko ndani ya CCM hivyo kundi linalomuunga mkono toka CCM ukijumlisha na wanachama wa upinzani ni lazima CCM ife natural death.
 
Pamoja na matatizo la tume huru lakini wagombea wa vyama vya upinzani nalo ni tatizo lingine.

Siku vyama vya upinzani wakipata akili ya kushawishi viongozi wenye majina toka CCM na wakawasimamisha kuwa wagombea urais ndiyo siku kitatokea kifo cha CCM. Kwa sababu hiyo itasababisha mgawanyiko ndani ya CCM hivyo kundi linalomuunga mkono toka CCM ukijumlisha na wanachama wa upinzani ni lazima CCM ife natural death.
Mbona walifanya hivyo kwa Edward Lowasa tena Lowasa alikuwa na nguvu nyingi sana wakati ule

Miye nafikiri kwanza tatizo ni katiba, tume huru na elimu ya urai kwa wananchi wetu uelewa wa wengi bado mdogo sana Kwenye mambo haya ya uchaguzi na demokrasia ya kweli
 
Back
Top Bottom