Wito: Tujiondoe CHADEMA

Imekuwa kawaida sasa kwa vijana wengi kushabikia mno CHADEMA.Hii inapelekea hata kusahau pale chama hiki kinapo boronga,wao hufumba macho na kutanguliza ushabiki mbele.
Jambo hili ni baya kwa mustakabali wa taifa letu,kwani pale ambapo CHADEMA itafanikiwa kuchukua dola,itakumbana na wakati mgumu kwani imezoea kujiona sahihi wakati wote.

Mbaya zaidi wengi wa mashabiki ni wale wasio hata na kadi ya chama,nao wanajiita wana CHADEMA.

Jambo la msingi kukumbushana ni kuwa sisi ni watanzania.Nawasihi mashabiki wa CHADEMA ni bora wakajiondoa CHADEMA na kujiona kama watanzania neutral ambao watashabikia maslahi ya taifa,na chama kinacho yatekeleza ndicho kiungwe mkono.
Hii itawawezesha kuikosoa chadema pale inapo kosea,na hivyo CHADEMA itakuwa imara na kupata nguvu zaidi.

TANZANIA:Nakupenda sana.

BANGE BANGE BANGE ZIMESABABISHA NISOTE JELA,BANGE BANGE BANGEEEEEEEEEEE ZITAPELEKEA USOTE SANAAAAA,AAAAAAAAAAH AAAAAAAAAAAH AAAAAAAAAAAAAAH,TUMECHOKA MIAKA HAMSINI YA UVUMILIVU TUMEICHOKA SASA TuMEFIKA MWISHO ALIEKUTUMA MWAMBIE WATZ WAMECHOKA UVUMILIVU SASA WANATAKA MABADILIKO
 
cdm ni cham makini chenye taratibu zake za kupokea maoni au ukosoaji kutoka pande zote. Ila umenishangaza unapotuambia tujitoe, nadhani ungetushauri sisi tusio na kadi za cdm tukachukue pamoja na gwanda, tungekusifu . Pia ingekuwa busara utueleze kwa ushahidi je ni wapi cdm ilipokataa kukosolewa au kutofuata ushauri uliotolewa na wananchi.

shida ccm wanaogopa M4C, wanaweweseka kila wakisikia ratiba yake, matokeo yake wanadai eti hakuna askari wa kuwalinda, kama Arusha waliwapiga raia mtaani kwa risasi na kuwaua tuna haja ya kulindwa na genge la wauaji.

viva cdm... peopl.............................................zzzz power.................................
 
ha2na haja kuendelea kubisha na huyu shabik wa mafisad! maan 2mechoshwa na propaganda zen nw we take over the power!

Kamwe siwezi kuwa shabiki wa mafisadi,kwani naipenda nchi yangu Tanzania na ni miongoni mwa watu wanao amini CHADEMA ni chama sahihi kwa sasa kuongoza nchi.
Kinacho nikera ni ushabiki wa ukipofu wa kudhani CDM ni chama cha malaika.
Wakati wa kujikagua na kujirekebisha ni sasa!
 
Una akili sana wewe. Huu ushabiki is too much, sasa naona umeshika kasi. hakuna aliye mtakatifu hapa duniani sasa iweje hawa wanaojiita wanachadema wasione mapungufu ya chadema? au ndio kusema hayapo? acheni ushabiki bwana wekeni maslahi ya taifa mbele.

Basi tusijitoe CHADEMA bali tupendekeze kwenye kura za maoni kufutwa kwa vyama vyote halafu tubaki na sera za maslahi ya nchi bila vyama maana kama ni ushabiki wa vyama kila chama kina washabiki wake na wana umbumbumbu wa kichama kama alivyo mtu mmoja mwenye jina linalofanana na kitambaa cheupe wanachovalishwa watoto wachanga ili wakikojoa mikojo isitiririkie pasipostahili....wote washabiki tu si wa maslahi ya nchi wala taifa.

Tufute vyama tubaki na wagombea binafsi katika katiba ijayo
 
Imekuwa kawaida sasa kwa vijana wengi kushabikia mno CHADEMA.Hii inapelekea hata kusahau pale chama hiki kinapo boronga,wao hufumba macho na kutanguliza ushabiki mbele.
Jambo hili ni baya kwa mustakabali wa taifa letu,kwani pale ambapo CHADEMA itafanikiwa kuchukua dola,itakumbana na wakati mgumu kwani imezoea kujiona sahihi wakati wote.

Mbaya zaidi wengi wa mashabiki ni wale wasio hata na kadi ya chama,nao wanajiita wana CHADEMA.

Jambo la msingi kukumbushana ni kuwa sisi ni watanzania.Nawasihi mashabiki wa CHADEMA ni bora wakajiondoa CHADEMA na kujiona kama watanzania neutral ambao watashabikia maslahi ya taifa,na chama kinacho yatekeleza ndicho kiungwe mkono.
Hii itawawezesha kuikosoa chadema pale inapo kosea,na hivyo CHADEMA itakuwa imara na kupata nguvu zaidi.

TANZANIA:Nakupenda sana.

Wewe umetumwa na nape tu huna jipya kwanini usiseme walio ccm wajitoe wawe neutral? Hata kama hawana kadi kura yao haitohesabika?
 
Mjinga mjibu sawasawa na ujinga wake... ndivyo biblia inatuagiza. Lakini namhurumia na kusamehe maana hajui asemalo. Nadhani katafuta aandike nini jf kaona aandike ujinga huu. tupa kuleeee
 
Ahsante mkuu mtu wenu.
Ushabiki wa kutoangalia ukweli wa mambo ulivyo ni hatari na hufanya hata fikra kuvia.
 
Back
Top Bottom