CHADEMA haiji kupata tena nguvu ya ushawishi kama iliyokuwa nayo kabla ya Uchaguzi wa 2015

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,305
9,734
Ndugu zangu Watanzania,

Kwa hakika uchaguzi ule utabaki katika historia ya wengi sana,utabaki kama ukumbusho wa kilele cha mafanikio ambayo upinzani ulikuwa umefikia katika kuteka mioyo ya watu,ulikuwa ni wakati ambao upinzani ulikuwa hata ukitangaza asubuhi kuwa mchana kutakuwa na mkutano watu walikuwa wanajitokeza kwa wingi sana. Ni uchaguzi wa kipekee ni uchaguzi wa mbwembwe za aina zote,ni uchaguzi wa aina yake,ulitikisa na Taifa likatetemeka kwa mbwembwe za wanasiasa majukwaani.

Ulitutikisa sana ule uchaguzi wana CCM,ulitutetemesha na kutikisa mioyo yetu hasa kwa wale waliokuwa na mioyo miepesi walitikisika na kutetemeka sana lakini kwa wenye mioyo migumu na ya chuma aina yangu niliwaambia kuwa CCM ni chama kiongozi na katu na kamwe upinzani wa nchi hii hauwezi kupewa Nchi na watanzania wote wenye akili Timamu na mapenzi mema na Taifa letu ,kwa kuwa wapinzani wataliwasha moto Taifa letu na kuliangamiza wakipewa nchi .

Wenye mioyo miepesi walikuwa na hofu na kutetemeka kwa kuwa hawakuamini macho yao kuona mawaziri wakuu wawili wastaafu kwa pamoja wakiungana kwa pamoja kwenda chama kikuu cha upinzani nchini,hawakuamini macho yao walipoona vijana mbalimbali kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini wakiwa upinzani na kujiona fahari kuwa upinzani.

Hawakuamini macho yao na walitetemeka walipoona ni ngumu kuvaa sare za CCM na kupita nazo mjini, walitetemeka sana walipoona watu mbalimbali wakirudisha kadi za chama na kujiunga na upinzani na wengine wakitamba kwa kauli zao za ulipo tupo.kwa hakika ulikuwa ni mtikisiko sana hasa kwa watu mliowaamini kuwa nao pamoja halafu wanakuja kuwasaliti mwishoni bila kutarajia. Usaliti unaumiza na kwa hakika kuna watu waliiumiza CCM kwa usaliti katika uchaguzi ule.

Tulijikuta tunaumizana sisi kwa sisi, yupo aliyekosa nafasi ya kugombea udiwani au ubunge au Urais Akaamua kukihama chama na kuungana na upinzani,na wengine walibaki lakini ushiriki wao ukawa ni mdogo ambapo ni kama wakawa hawajavunja makundi na kuamua kukipigania chama kwa jasho na machozi.

Asante kwa wazee wetu waliojitoa na kuendelea kukiunganisha chama na kuendelea kukipigania chama kwa jasho, maumivu na uchovu mkubwa sana wa mwili.hali Hiyo ilileta morali na nguvu kwa wanachama wote kuendelea kukipigania na kukipambania chama chetu,iliwapa nguvu vijana kwakuwa waliona iliwapasa kuwa msitari wa mbele kukipigania chama.

kwakuwa wazee wetu kama akina mzee Kikwete,mzee Mwinyi,mzee mkapa,mzee kinana,mzee makamba,mzee Mangula ,mzee Malecela ,mzee Pius msekwa walishakipigania chama Tangia wakati wa ujana wao mpaka uzee wao,hivyo ilikuwa ni wakati wa vijana kuwapokea wazee hawa kazi ya kukipigania chama chao ili kishinde kwa kishindo katika nafasi zote.

Mfumo imara na thabiti wa CCM Ndio nguzo inayoendelea kuibeba CCM ,Ndio inayoendelea kuifanya CCM kuwepo madarakani mpaka leo hii, kwa kuwa ndani ya CCM hakuna aliye mkubwa ndani ya CCM ,Ndani ya CCM Chama Ndio kikubwa kuliko mtu, CCM Inajiendesha kitaasisi na siyo kumtegemea mtu mmoja au kikundi fulani.

Ndani ya CCM Kila mwanachama ana nafasi ya kukijenga chama ila hana nafasi ya kukiua chama au kuondoka na chama mfukoni mwake. Ndio maana ukileta ujeuri na kiburi unatupwa nje ya Uzio na chama kinasonga mbele pasipo kutetemeka wala kuyumba,kama huamini na unaamini wewe ni mkubwa kuliko CCM na unaweza kukiua chama basi wewe jaribu kuondoka leo uone kama kuna atakayekufuata.

Leo chama ni imara na madhubuti kuliko wakati mwingine wowote,leo chama kinakimbiliwa na kila mtu,leo kadi za CCM zinatafutwa Kama Dhahabu,leo vijana wa vyuo vikuu wanajiona fahari kuwa wana CCM ,Leo watu wanavaa sare za CCM popote pale bila hofu wala wasiwasi wowote ule, leo ni heshima kujitambulisha kuwa ni mwana CCM .Hii yote ni kwa kuwa kuna machozi ,jasho na Damu ya wana CCM waliokipambania Chama.

wapo waliokifia chama hiki,wapo walioumizwa kwa sababu ya kukipigania chama hiki ,wapo waliojeruhiwa kwa kukipambania chama hiki. Lakini pamoja na kukipigania chama chetu hiki kwa jasho ,damu na machozi bado hawajawahi kujiweka juu ya chama au kuhitaji malipo au fadhila au vyeo au madaraka bali walifanya kazi hiyo kwa uzalendo na upendo kwa chama chetu.

Hivyo vijana na wanachama wote tunakila sababu ya kujifunza kwa somo hili kuwa ndani ya CCM hatugawani vyeo au madaraka au mamlaka bali tunagawana majukumu ya kukipigania chama na kuhakikisha kuwa kinaendelea kusalia madarakani na kinawatumikia vyema watanzania kwa kuwaletea matokea chanya na maisha bora yenye kuleta matumaini katika maisha yao.

Tunapaswa kujifunza kuwa hata ikitokea umekosa nafasi ya kugombea uongozi fulani basi huna budi kumuunga mkono yule anayekuwa amepitishwa na chama kama ambavyo alifanya mzee wetu Kikwete kwa mkapa japo alikuwa na nguvu kubwa tu na ushawishi ndani ya chama na wanachama 1995,tujuwe kuwa kama ilipangwa na Mungu uje uwe kiongozi wa ngazi fulani basi lazima itafika siku Mungu atakuinua na kukupa nafasi hiyo katika njia anazozijuwa mwenyewe Mungu.

Kwa sasa ni ngumu kwa upinzani kuja kupata na kurejesha ile nguvu iliyo kuwa nayo CHADEMA wakati huo,kwa kuwa kwa sasa ilishapoteza imani na kuaminika machoni na mioyoni mwa watanzania, ilisha Kimbiwa na makundi yote yaliyo kuwa yakiwaunga mkono ,ilisha poteza viongozi wote mahili waliokuwa wanaaminika ndani ya chama na nje ya chama,ilishaacha na kuitupa na kuisaliti misingi yake iliyokuwa imeipatia umaarufu.

Lakini kubwa ni kuwa CCM ilishajisahihishaa makosa yake yaliyokitesa,kukiumiza , kukijeruhi na kutishia uhai wake ndio maana kwa sasa CCM Ni Imara, madhubuti na yenye nguvu isiyo pimika,ndio maana inaendelea kupokea na kusajili wananchama wapya kila iitwayo leo,ndio maana inaendelea kuwa Tumaini la watanzania na chama kiongozi barani Afrika. ndio maana watu na viongozi mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wanakuja kujifunza na kupata uzoefu ndani ya CCM. Nawakaribisheni ambao bado mpo nje ya CCM mje mjiunge na CCM na kuwa sehemu ya kulijenga Taifa letu na kuachana na CHADEMA ambao walishapoteana muda mrefu na kila mmoja anaogelea kivyake na kupiga Mbizi kuelekea uelekeo wake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hakuna kwa sasa chama chenye uwezo wa kuitikisa wala kuiyumbisha CCM .Hakuna chama wala mtu mwenye kuipa hofu CCM. CCM ya sasa ni imara na yenye nguvu kubwa sana
Sawa maadam mmekubali tume huru ianzishwe nakuhakikishia hapa mkiweza fikisha hata 30% basi parapanda Italia.

Hakuna wakati CCM ni unpopular kama Sasa, maisha ni magumu, vitu bei ghali, no umeme, no Maji, bundle gharama Rais naye sio orator Sasa kampeni atawapigia nani? Kazi mnayo
 
Sawa maadam mmekubali tume huru ianzishwe nakuhakikishia hapa mkiweza fikisha hata 30% basi parapanda Italia.

Hakuna wakati CCM ni unpopular kama Sasa, maisha ni magumu, vitu bei ghali, no umeme, no Maji, bundle gharama Rais naye sio orator Sasa kampeni atawapigia nani? Kazi mnayo
Kiuchumi Tupo vizuri sana kama nchi . Serikali ya Rais samia imefanikiwa kujenga uchumi unaogusa maisha ya watanzania wote .Ni uchumi unaokua katika mifuko ya watanzania wote kutokana na uwekezaji wa serikali kuweka mabilioni ya fedha katika mambo yanayomgusa Mtanzania.

Suala la mfumuko wa bei ni kuwa serikali yetu imefanikiwa kuudhibiti kwa kiasi kikubwa ,ndio maana unaona na kushuhudia wakenya wakija na kuingia Tanzania kununua mafuta.
 
kila mtu ana uhuru wa maoni lakini kuongea vitu ambavyo huwezi kuvipima kwa kila hali inatibua, ivi konokono unamjua konokono ndio amekuambia habari hizo?, maendeleo hayana chama.
Kwamba wewe huwezi kufanya tathmini ya hali ya kisiasa nchini kwa vyama vya siasa? Kwamba unashindwa kuelewa na kukubali ukweli kuwa vyama vya upinzani hapa nchini ni dhaifu sana na visivyo na malengo zaidi ya Usaka Tonge Tu?
 
Sawa maadam mmekubali tume huru ianzishwe nakuhakikishia hapa mkiweza fikisha hata 30% basi parapanda Italia.

Hakuna wakati CCM ni unpopular kama Sasa, maisha ni magumu, vitu bei ghali, no umeme, no Maji, bundle gharama Rais naye sio orator Sasa kampeni atawapigia nani? Kazi mnayo
Mahali Chadema imevurunda ni kukubali kula matapishi yao

Kuanzia mwanzoni waligoma kuwatambua Covid 19

Lkn sasa hivi wanakubali kuchukua ruzuku

Inaonyesha walivyo vigeugeu na kukosa msimamo
 
Asilimia 80% ya Vijana hawawezi kuipigia kura CCM labda Wazee na wale waoga wa mabadiliko wa Vijijini.
Kwa sasa mamilioni ya vijana wanaiunga mkono CCM ,Ndio maana ukienda vyuo vikuu unaona namna vijana wengi walivyo hamasika kujiunga na CCM
 
Back
Top Bottom