Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,482
- 7,459
Hakuna ubishi kuwa CHADEMA iliishi maisha ya mateso sana mara baada ya uchaguzi wa Rais 2015. Hakuna rangi ambayo hawakuiona, kuanzia chama chenyewe hadi wanachama na viongozi wake. Tunaopenda na kujali utu, tulisikitishwa sana na mateso waliokuwa wakiyapata CHADEMA. Waswahili wanasema Mungu si Athumani. Baada ya kifo cha JPM, na aliyekuwa Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kuchukua hatamu za urais, pamekuwepo na mabadiliko makubwa sana na kurejesha uhai wa Chama. Waliokimbia nchi wamerudi, waliofungwa wamefunguliwa, mikutano yao imefunguliwa, biashara zao zimerejea na Kila kitu chao kimerudi normal.
Sidhani kama ilikuwa kazi rahisi kwa Samia kushawishi chama chake na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya big u-turn ya namna ya kudeal na vyama vya upinzani hasa CHADEMA. Mama wa watu akaja na slogan iitwayo 4Rs akikusudia kujenga Taifa lenye staha na stara. Kwamba wao CCM na CHADEMA ni kitu kimoja na wanajenga nyumba moja. Mama amesema kukosoa RUKSAA ila akosolewe kistaarabu. Kushauriwa RUKSAA, ila kistaarabu.
Ogopa mtu mweusi. Narudia tena ogopa mtu mweusi. Ubongo wake unasahau haraka kuliko kiumbe hai yoyote duniani. CHADEMA wakaota pembe. Likaja saga la Bandari. Majibu ya Serikali kwa wanaohoji mkataba wa Bandari ni kuwa Serikali imesikia maoni ya wananchi na itayafanyia kazi.
Busara ya kawaida ni kusubiri hicho Serikali ilichoahidi. Lakini wapiii, si kwa mtu mweusi. CHADEMA kwa kushirikisha na washirika wake imekuwa mstari wa mbele kumtukana Rais Samia kwa kila aina ya matusi, dharau, kejeli hadi vitisho. Utadhani sio wao walioombwa kukosoa kistaarabu na kushauri pale inapo budi. Leo wao ndio wamefikia hatua hadi ya kuomba Mungu "Aingilie Kati" ili wao "waishike nchi". Najua wahafidhina huko CCM na Serikalini wanamcheka mama kwa meno yote 32. Huenda wanajua rangi halisi ya mtu mweusi, rangi halisi ya CHADEMA. Ndiyo, kama si akili ya kuku huenda wakoloni wasingetutawala. H.M. Stanley anakiri katika kitabu chake kuwa alilazimika kuwabebesha waafrika nguo za Kaniki (mashuka meusi) na Marekani (mashuka meupe) ili kuwahonga machifu ili wampe ruhusa na ulinzi apitapo katika tawala zao. Ogopa mtu mweusi.
Hakuna ubishi kuwa chini ya uhai wa chuma, JPM hakuna pua ingeinuka na kusema chochote kuhusu Mkataba (kama ungeingiwa katika uongozi wake). Nadhani JPM alikuwa na uwezo wa akili sawa na wakoloni kiasi alijua watanzania tu karibu zaidi na punda au ng'ombe. Tunahitaji kuchungwa kupelekwa malishoni na kurudishwa zizini. Mimi si Mshabiki wa JPM na si Mshabiki wa nguvu popote pale, ila JPM nilimuelewa sana unapodili na mtu mweusi.
Kwa kadri nijuavyo, Muomba shari hupata haraka kuliko Muomba Heri. CHADEMA wanaomba Shari, tena kwa spidi kubwa. Najua wataipata. Mungu yuleyule wa miaka 7 iliyopita ndiye Mungu huyohuyo aliyopo sasa. Kama Mungu hataingilia ugomvi wao (kama wanavyoomba), basi tarehe zitafika. Tutapata KIONGOZI wamtakao CHADEMA. Huyu hatakuwa "muuzaji" wa mali za watanganyika. Mimi naungana na Chama changu cha CHADEMA katika maombi. Naomba mmoja kati ya hawa awe Rais chaguo la maombi yetu.
1. Mwigulu Nchemba
2. Paul Makonda
3. Lengai Ole Sabaya.
4 Au hata PM wa sasa.
Naam, CCM si wajinga. Wanatujua vizuri watu weusi. CCM wakituletea hawa, sisi CHADEMA tutakuwa na furaha sana.
Nimalize kwa kusema Dhambi Mnayoifanya CHADEMA haitawaacha salama. Haitawaacha salama kwasababu pia inawapa muono wana CCM kujua ni aina gani ya kiongozi atawafanya wa relax kama walivyo relax kwa miaka 7 iliyopita. Lengai Ole Sabaya, Paul Makonda Mwigulu Nchemba, sisi CHADEMA tunawataka baada ya mzanzibari.
Mungu Ibariki Tanzania.