Mh. Wassira ni mtu wa CCM na pia ni mbunge wa Bunda ambayo iko mkoa wa Mara ambayo makao makuu yake ni Musoma..
Ole Sendeka akimpinga Mh. Nyerere pia anapaswa kumpinga Mh. Wassira kwa kuwa wote wanatoka Musoma.
Kilichonishangaza ni Wassira kushangilia kauli hii ya kibaguzi ya Sendeka kama ZUZU.
Hii imenikumbusha ile hotuba ya JKN, kwamba sisi watanzania ni wajinga. Mtanzania ana dhahabu anakuja mtu chupa anamwambia kwamba ile sio dhahabu anabadilishiwa na chupa halafu huyo matanzania anatoka akichekelea kama ZUZU kumbe alichobadilishia na chupa na dhahabu yake ndiyo imechukuliwa.
Huyo ndiyo Wassira ni kama ZUZU aliyotoa dhahabu na kupewa vipande vya chupa. Fumbo mfumbie MJINGA!