Bibi Titi Mohammed, Mwanamke anayetajwa kumtikisa Nyerere na kupewa Kesi ya Uhaini

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
20231018_075826.jpg
20231018_075824.jpg

Titi Mohammed Salum Mandangwa kazaliwa katika familia ya dini haswaa, lakini kapita vikwazo vingi. Amezaliwa 1926, Dar es Salaam na kufariki Johannesburg, RSA katika hospitali ya Net Care, Novemba 5, 2000. Aliishi miaka 74 ya machozi, jasho na damu.

Alizaliwa kwa jina la Titi Mohammed Salum Mandangwa maarufu "Bibi Titi Mohammed". Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji. Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima.

Baba aligoma TITI asipelekwe shule. alikataa TITI asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri. Mama yake TITI alimpeleka shule baadae. Baba yake alifariki TITI akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka TITI Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4

TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu. Bibi aliolewa na mtu mzima, Titi akiwa na miaka 14 tu. TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu.

TITI alijifungua mtoto wa kike aitwae HALI ambaye alikuja kuolewa na MZEE IDD HAMIS, Mshambuliaji hatari wa zamani wa Cosmopolitans, klabu ya kwanza kutwaa ubingwa Tanzania ambapo walikuwa wakiishi mtaa wa Sikukuu na Udowe na kubahatika kupata watoto 3 wa kiume.

Baadae, TITI aliachana na mume huyo kijeba ambaye alikuwa ni baba wa HALIMA , mume ambaye hakuwa chaguo lake. TITI alianza kuwa maarufu angali mdogo alipokuwa kiongozi wa ngoma za maulid ambazo zilimjenga uwezo wa kujiamini na hivyo akawa maarufu sana.

TITI aliolewa na dereva wa teksi aitwae Boi Selemani, baada ya ndoa yake ya kwanza kusambaratika. BOI, alikuwa ni rafiki wa SCHNEIDER PLANTAN aliyekuwa mmoja wa viongozi wa TAA, Bw. PLANTAN alienda nyumbani kwa BOI na kumweleza kuwa ametumwa kumweleza TITI ajiunge na TANU

BOI alikubali na akajinunulia kadi na.15 ya TANU na pia akamnunulia TITI kadi na.16. Jumla alitoa TZS 12/= kwani kila kadi iliuzwa TZS 6/=.Ndivyo walivyojiunga TANU. BOI pia alichangia TSH 10/= kwa ajili ya nauli ya Mwalimu NYERERE kwenda UNO (TSH 5/= kila mmoja).

TANU ilizaliwa tarehe 7.7.1954. Wanachama wa mwanzo kupata kadi za TANU walikuwa NYERERE (Kadi na.1), A. SYKES Na.2, A. SYSKES No.3 D. AZZIZ No.4, DENIS PHOMBEAH No.5, DOME OKOCH Na.6, J. RUPIA Na.7

Bibi Titi Mohammed alikutanishwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1954, wakafanikiwa kuwa marafiki wa kudumu (ingawa baadae walikuja kuwa na uadui wa kisiasa, usiokuwa na uwazi) na uadui ambao ulimfikisha Bibi Titi Mohammed magereza kwa makosa ya uhaini dhidi ya serikali

Bibi Titi Mohammed hakuwepo wakati wa TAA au TANU ya mwanzo. aliletwa baadae na kukutana na Nyerere, 1954/55 na dereva Taxi aliyejuana na shemeji wa Bibi Titi, ingawa katika pekenyua yangu nimekutana na jina la Schneider Plantan (kama mtu aliyemshawishi kujiunga na TANU).

Boi aliwahi kumlalamikia Schneider kuwa mkewe Bi. Titi hatulii nyumbani kwa ajili ya shughuli za TANU kiasi imekuwa yeye ndiyo mfuaji wa nguo zake na mpishi wa chakula chake. Boi Selemani alikuwa dereva wa taxi. Schneider ana historia kubwa pia kwa historia ya siasa za TANU

Kuna wakati Boi (mumewe Bibi Titi Mohammed) alilalamika kwa Schneider Plantan hadi kusema, "TITI ni mwanamke wa kiislam, kasoma madrasa, kapanda jukwaani bila baibui. Hii si sawa kabisa".. Picha hii ni viwanja vya Jangwani 1955 Nyerere akijianda kwenda UNO (Umoja wa Mataifa)

Schneider Plantan ndiye aliyesimama kidete kuwaleta vijana wasomi katika chama cha TAA ili kuwaondoa wazee wa mwanzo waliokuwa wamechoka na kuifanya TAA isifanye siasa za maana za harakati kwa ajili ya ukombozi wa Tanganyika. Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Sasa TANU ilipokuja kuasisiwa mwaka wa 1954 Schneider ndiye aliyemleta Bi. Titi Mohammed katika TANU pamoja na wenzake akina Tatu Binti Mzee na wanawake wengine ili kuipa nguvu TANU mbele ya makundi ya wanawake waliokuwa nyuma wakati huo.

Mwaka 1955 wakati safari ya Nyerere kwenda UNO inatayarishwa ugomvi wa Boi na Bibi Titi ulipamba moto. Boi akimlaumu Schneider kwa kumuingiza mkewe kwenye siasa na harakati za kudai uhuru. Bi. Titi na wenzake wako katika hekaheka ya kuhamasisha wananchi kujiunga na TANU

“BOI mwenyewe ndie aliyeniruhusu kujiunga na TANU na tena ndiye aliyeninunulia kadi ya uanachama. TANU pia ilimwandikia barua anisaidue mambo ya TANU.Lakini mwisho hizi safari zilimshinda. Nilikuwa nakaa nje ya DSM hata kwa miezi 3 na nikirudi sikai hata siku 10, nasafiri tena”

“BOI akaniambia anataka kuoa mke mwingine. Nikamwambia sawa, niache na kazi yangu kwani nimeizoea. Kwahiyo BOI akamuoa Bi. KHADIJA lakini wakashindwana wakaachana. Nilifunga mizigo yangu nikaondoka kwa BOI”. Anasema TITI baada ya ndoa yake na Boi kuparanganyika

Baadae sana, Nyerere alivutiwa na Titi, akapewa kadi namba 16. Nyerere alikuwa na kadi namba 1 na Boi Selemani alipewa kadi namba 15. Kulia ni Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir, Mwl Nyerere na nyuma ya Nyerere ni Maria Nyerere, Rajab Diwani na John Rupia

Mapambano yote ya wanawake wa TANU katika kudai uhuru wa Tanganyika wakati huo wakiongozwa na Bibi Titi Mohammed yalikuwa yakifanyika kwa kuanzia katika ofisi za Lumumba (ambazo sasa CCM wamejimilikisha kama jengo lao na kuziita ofisi ndogo za CCM). Zilijengwa kwa nguvu ya umma

Mwaka 1955 (baada ya kujiunga na TANU na kuwa mwanachama kamili), Nyerere na Bibi Titi Mohammed walifanya mkutano mkubwa wa hadhara Tabora. Walipata mwaliko kutoka kwa watu wa Tabora, Kumbuka kuwa Tabora ya wakati huo ilikuwa na hamasa kubwa katika harakati za kudai uhuru.

TITI ndiye aliyekuwa akiimbisha na kuhutubia kwanza kabla ya NYERERE kupanda jukwaani “kushusha” nondo. Kwa hakika, TITI alikuwa akikonga nyoyo kwa kiswahili chake cha pwani na nyimbo zake: (Hongera mwanangu eeh na mi nihongere eeh hongera X 2) na (Mama Usungu, Mama Usungu X 2).

Baada ya kufahamiana na Mwalimu Nyerere, Bibi Titi Mohammed alipewa uongozi katika Women Wing ya TANU ambapo alishiriki katika kuhamasisha wanawake kuunga mkono harakati za TANU za kudai uhuru. Aliongoza makongamano, mihadhara na harakati za nyumba kwa nyumba kuhamasisha

Tarehe 8.7.1955, TITI binti Mohammed akiwa Mwenyekiti wa Tawi la Wanawake wa TANU, alifanya mkutano mkubwa na kuvuna wanachama 400 na ndani ya miezi 3 tu akawa amepata wanachama 5,000: Bibi anasema kwa kauli yake;

“Nilizunguka Tanganyika nzima. tulienda Tanga tarehe 1.1.1956 na Bwana mkubwa na RAJAB DIWANI tukazunguka siku 21. Kamati Kuu ikanipa ruhusa ya kusafiri peke yangu. Pia nilifanya safari nyingi na OSCAR KAMBONA. Tukiwa na KAMBONA tulikuwa tukipita nyumba hadi nyumba, usiku na mchana”

Mwaka 1957, pale kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, mbele ya mgeni kutoka chama cha LABOUR cha Uingereza, Bibi Titi alipewa nafasi ya kuhutubia mkutano wa TANU wakati Nyerere akiwa Butiama mapumzikoni kwa mama yake. Nyakati hizo siasa haikuonekana kama ni shughuli ya wanawake, wao walitakiwa kubaki nyumbani tu.

Bibi Titi akihutubia akinyoosha vidole kwa wanaume aliwaeleza wanawake wenzake “wanawake amkeni. Tokeni majumbani tupambane pamoja na wanaume mpaka uhuru ipatikane. Msiogope. Msiogope. Msiogope”

“Mnawaona hawa? Basi wafanye watakavyofanya hawa, pamoja na hao wengine wote wanaowatisha Duniani, wametoka katika matumbo ya wanawake na waliishi humo miezi tisa.. kila mmoja kanyonya ziwa la mama yake miaka miwili.. sasa tujitokeze wasituahinde hawa”

“Kutawaliwa siyo kuzuri ndugu zangu, hili ni letu sote siyo la wanaume pekee yao, njooni akina dada, njooni akina mama na vikongwe pia.”

Aliunguruma Bibi Titi Salum Mohammed Mandangwa jukwaani huku zikisikika kelele za vifijo na nderemo, hoihoi na vigelegele.

Kutoka hapo jina la Bibi Titi ndiyo likawa habari ya mji wote. Habari zake zikazagaa hadi Afrika ya Mashariki yote. Wanawake wengi sana wakajitokeza na kujiunga na TANU na harakati zake. Msibani, harusini, nyumbani habari ikawa “TITI, TITI, TITI, TITI”

Wapigania uhuru wa Kenya wakati huo akiwepo Tom Mboya, Jaramogi Oginga Odinga, wakaleta maombi Tanganyika, Hibi Titi aende Kenya kuwasaidia kushawishi serikali ya Uingereza kumtoa kifungoni Mzee Jomo Kenyatta aliyefungwa kwa kosa la uhaini (kudai uhuru).

Bibi Titi akaenda zake hadi Kenya. Akatoa fora katika mikutano yake ya Mombasa, Kisumu, Machakos na Nairobi. Titi jukwaani alikuwa akivalia mini-skirts sawa na wanawake wa Kenya, akilia kwa uchungu na kulitaja jina la Kenyatta awe huru lakini mwisho wa ujumbe wake akiwataka wanawake wampiganie Kenyatta watoke ndani.

Haikupita kitambo kirefu, Mzee Jomo Kenyatta aliachiwa huru na safari yake ya kwanza alisafiri hadi Tanzania na kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam na muda mwingi alimshukuru Bibi Titi Mohammed.

Katika mkutano huo Nyerere alisema yupo tayari kuhairisha uhuru wa Tanganyika (ambao tayari ulikuwa umejulikana) ili tusubiri Kenya wapate uhuru wao nchi ziungane kuwa moja na Kenyatta awe Rais wake.

Tamko zito sana ambalo bila shaka lilitokana na kazi ya Bibi Titi. Uhuru uhairishwe na Rais awe mtu mwingine kutoka Kenya? Mwalimu Nyerere aliipenda sana Afrika, alitamani muungano wa Afrika sawa na muungano wa Marekani moja. Taifa lenye nguvu kiuchumi.

Baada ya uhuru kupatikana Bibi Titi alipata ubunge Rufiji na akateuliwa kuwa waziri mdogo wa utamaduni na maendeleo. TITI akapeleka hoja ya KISWAHILI Kutumika Bungeni: TITI alikuwa ameishia darasa la 4 tu hivyo alikuwa hawezi “kutema yai” kwa ufasaha. Siku moja mwanzoni mwa 1960s akiwa bungeni akatoa hoja kwamba wananchi wa Magomeni wanataka nao wawe na taa za barabarani ambapo alisema

“We want fire in Magomeni.... We want fire in small bottles”. Maneno ya Bibi Titi. Wabunge walicheka pamoja na NYERERE akiwa Waziri Mkuu ambapo aliamuru KISWAHILI kianze kutumika bungeni.

Bibi Titi Mohammed alikuwa pia mwenyekiti wa UWT na EAMWS tawi la Tanganyika. Mjumbe wa tume ya Maulid (kamati ndogo ya kuandaa Maulid kila mwaka), Mwenyekiti wa kamati akiwa Tewa Said Tewa (mbunge wa Kisarawe) na katibu akiwa Chifu Abdallah Said Fundikira (aliyekuwa waziri wa sheria). Wakapata kiwanja kikubwa Chang’ombe kwa ajili ya ujenzi wa chuo kikuu (kabla hata UDSM haijapata eneo).

Nyerere alialikwa kuweka jiwe la msingi. Nyerere na serikali yake hawakupendezwa na jambo hilo. Mradi ulikuwa unafadhiliwa na Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser Hussein. Serikali ikasimamisha mradi na kuvunja kabisa EAMWS na kuundwa baraza lingine kwa ajili ya waislam.

Mwalimu Nyerere na wenzake ndani ya TANU, pamoja na kukataa ubaguzi kwa kukubali kuwapokea na kuwapigia kura wahindi kwenye mpango wa kura tatu, kwenye hili la uislam - wahindi hawakutakiwa wasaidie waislam na hapo ikavunjwa EAMWS kwa amri ya serikali likaundwa BAKWATA la waafrika watupu kutoka Sunni.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Bibi Titi Mohammed na Tewa (Tewa Said Tewa alikuwa Rais wa jumuiya ya EAMWS) wakapoteza viti vyao ndani ya TANU na serikalini. Aliyekuwa katibu, chifu Abdallah Fundikira akapelekwa Nairobi kuwa mwenyekiti wa shirika la ndege la jumuiya ya Afrika Mashariki (EAAC).

Ndani ya halmashauri kuu ya Taifa ya TANU, Bibi Titi alipambana na kuwabwaga wanasiasa wakongwe kwa hoja nzito pale mjadala wa kuivunja EAMWS ulipokuwa unajadiliwa. Mwaka 1968, Bibi Titi Mohammed alikamatwa na kuhusishwa na tukio la uhaini (ni hadithi nyingine ndefu)

Mwaka 1967, TITI, bila kupepesa macho wala kutikisa pua, akabwaga manyanga na kujiuzulu ujumbe wa Kamati Kuu ya TANU kwani alikuwa hakubaliani na Kipengele cha 5(a) cha Azimio la Arusha kuhusu maadili kwamba ni marufuku kiongozi wa serikali au TANU kuwa na nyumba ya kupangisha.

Safari hii ya pili Bi. Titi Mohammed na Tewa Said Tewa walikwenda Msasani kumuona Mwalimu Nyerere kumuuliza kwa nini anaachia vyombo vya dola vinapiga vita East African Muslim Welfare Society (EAMWS).. Hii ilikuwa mwaka wa 1968 katikati ya kile kilichokuja kujulikana kama “mgogoro wa EAMWS.”

TITI alikuwa na nyumba 2 ambapo moja aliijenga kwa kuuza vito vyake vya dhahabu na nyingine ni ya mkopo. Nyumba moja ipo Upanga mkabala na Makao Makuu, JWTZ na nyingine ipo Temeke. Uhusiano wa NYERERE na TITI ukawa umelegalega baada ya kumkosoa Nyerere kwenye azimio la Arusha.

Oktoba ya mwaka 1969, Bibi Titi Mohammed na aliyekuwa waziri wa kazi wakati huo, Michael Kamaliza walikamatwa, pamoja na maafisa wa jeshi wengine wapatao wanne na kufanya idadi ya waliokamatwa kufikia 7, wakituhumiwa kwa kupanga njama za kuipindua serikali iliyokuwa madarakani.

TITI alikuwa ni mwanamke pekee katika kesi hiyo. Walidaiwa kupanga kutekeleza azma hiyo wakati Rais NYERERE atakapokuwa nje ya nchi. Kesi ilianza kurindima 6.6.1970 chini ya Jaji Mkuu, Georges, CJ na upande wa mashtaka ukiongozwa na MARK BOMANI.

Washtakiwa wengine katika shtaka hilo la uhaini walikuwa ni Gray Likungu Mattaka, John Dustan Lifa Chipaka, Michael Marshal Mowbrya, William Makori Chacha na Alfred Philip Millinga. Wote kwa pamoja walishtakiwa kwa tuhuma za kupanga njama kumpindua Rais Nyerere

JUMAMOSI ya Agosti 1, 1970 Mahakama Kuu ya Tanzania iliambiwa na mkurugenzi wa mashitaka ni jinsi gani Bibi Titi Mohammed alivyogharamia mapinduzi ya kumuua Julius Nyerere na kuiangusha serikali yake (jaribio la kimapinduzi dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani)

Kesi ilinguruma kwa siku (127). TITI na wenzake kasoro Bw. MILLINGA walitiwa hatiani kutokana na ushahidi madhubuti na kupewa kifungo cha maisha. TITI akaenda kutumikia kifungo gereza la Isanga, Dodoma.

Bi. Titi akiwa Gereza la Isanga Dodoma, moja ya magereza magumu. Kabla yake mwaka wa 1953 mwanasiasa mkubwa sana Tanganyika sehemu za Maziwa Makuu, Ali Migeyo alifungwa gereza hilo na wakoloni wa kiingereza kwa kosa la kufanya mkutano wa siasa Kamachumu bila idhini ya serikali

Miaka 17 baadae, mpigania uhuru Bibi. Titi Mohammed nae anajikuta kifungoni kwa kuhusika na kesi ya uhaini katika jaribio la kutaka kuipindua na kuiondoa madarakani serikali ya Mwalimu Nyerere aliyoipigania wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kutoka kwa wakoloni.

Akiwa hapo gerezani Bi. Titi anaandika historia ya uhuru wa Tanganyika na anaeleza ushirikiano wake na Nyerere wakati wakiwa katika ofisi ya TANU New Street. Bibi Titi anaeleza katika muswada wake, anaoandika jela jinsi yeye na wenzake walipita mtaa kwa mtaa kueneza TANU.

Baada ya TITI kukumbwa na dhahama ya kesi ya uhaini, mumewe akaamua kumuacha aliona hiyo ni fedheha kubwa isiyovumilika kwenye jamii! Nyumba 2 za Bibi TITI Zataifishwa: Wakati akiwa anatumikia kifungo chake cha maisha, serikali ikataifisha nyumba zake mbili zilizotajwa hapo juu

Baada ya kuhukumiwa kwenda jela kwa kosa la uhaini, Bibi Titi Mohammed aliamua kukata rufaa yake katika mahakama ya rufaa Afrika Mashariki - Court of Appeal for Eastern Africa (iliyokuwa chini ya East Africa Community, ile jumuiya ya zamani), rufaa ambayo nayo ilishindikana pia.

Mwanamama mmoja mwanasiasa machachari wa Kenya baada ya kupata habari za TITI kufungwa maisha alikuja Butiama na akaomba aonane na Mwalimu na mama yake. Alipoonana nao akasema

“Utakuwa ni wizi wa fadhila kama wewe NYERERE utaendelea kumfunga TITI licha ya yote aliyokufanyia wewe, TZ na sehemu hii ya dunia. Tafadhali sana nimetumwa na wanawake wa Kenya nikuombe umwachie huru kama yeye alivyopigania kuachiwa huru kwa JOMO KENYATTA”.

Mwalimu Julius Kambarage NYERERE alimjibu mama huyo kuwa maombi hayo ameyapokea na atayafanyia kazi. Rais NYERERE, akitumia mamlaka yake chini ya ibara ya 45 ya Katiba, alimsamehe Bibi TITI Mohammed mwezi April 1972.

Baada ya kusikia msamaha huo, Bi. TITI Mohammed hakuamini masikio yake kwani aliishaamua kupambana na hali yake na alijua angelifia gerezani. Hivyo, alipanda garimoshi kutoka Dodoma kwenda Dar es salaam akiwa na furaha tele na meno yote 32 nje.

Ndugu zake walimlaki kwa bashasha na nderemo na akaenda kuishi kwenye nyumba liyozeeka kweli ya mama yake mzazi iliyokuwa maeneo ya Temeke. Mama yake, aliyekuwa mtu mzima sana, almanusra azimie kwa mshtuko wa kumuona mwanae baada ya kutoka magereza.

Baada ya kuachiwa, TITI alienda kuishi Temeke. Maisha ya kipweke sana kwani ndugu na marafiki walimnyanyapaa: “Mtu angeweza kufikiri kwamba nina ugonjwa wa kuambukiza”. TITI akawa muda mwingi anakaa kibarazani kwao akiuza mafuta ya taa ya rejareja ili kuweza kumudu maisha!

Akiwa ofisini kwake Nairobi, Kenya tayari amesahau kuhusu Ujumbe wake kwa Nyerere, siku moja akapata habari kwamba kuna mgeni kutoka Tanzania anataka kumuona. Akaagiza apite ndani.

Alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, John Samuel Malecela akiwa na ujumbe kutoka kwa Nyerere “nimetumwa nije nikupe habari njema kwamba Nyerere tayari amemuachia huru Titi Mohammed Salum Mandangwa”

Baada ya kupata ujumbe huo, mwanasiasa Mwanamama huyo kuutoka nchini Kenya aliyejawa na furaha akasema: “Naomba kamwambie Mwalimu NYERERE kwa niaba ya wanawake wote wa Kenya na wananchi wa Afrika Mashariki, nasema ahsante sana kwa uungwana wake na uaikivu wake”.

Bibi Titi aliendelea kuishi maisha ya chini kabisa Temeke, mtaa wa Ngarambe, nyumba zake mbili za kisasa kabisa Upanga zilitaifishwa na Azimio la Arusha. Bibi Titi aliwekwa chini ya ulinzi fulani (semi house arrest), kutwa nzima alikuwa akikaa nje ya kibaraza chake akiuza mafuta ya taa kwa kupimia watu vibaba.

Nyumba zake Bi. Titi Mohammed alirudishiwa na Rais Mwinyi. Nyumba moja ipo mkabala na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Hivyo, Bibi TITI akahamia nyumba ya Upanga.

Mara zote wakati akiwa uraiani baada ya kutoka gereza la Isanga, Dodoma, Bibi Titi akihojiwa na wanahabari kuhusu masuala ya kesi yake ya uhaini akiwa gerezani alikuwa akiwajibu “tumuachie Mungu” lakini alieleza kwa kirefu tu ugomvi na tofauti yake na Mwl, Nyerere.

Titi Mohammed alikuja kueleza kirefu ugomvi wake na Mwl, Nyerere katika mahojiano aliyofanya na gazeti la RAI mwaka 1994. Alisema kuanguka kwake kisiasa kulitokana na kumpinga Mwalimu Nyerere kwenye halmashauri kuu ya TANU, wakati Nyerere anatafuta kuungwa mkono na waislam ndani ya TANU baada ya kuivunja EAMWS.

TITI alifariki tarehe 5.11.2000 katika hospitali ya Net care, Johannesburg, Afrika Kusini alikokwenda kupata matibabu. Mwaka mmoja baada ya kifo cha Nyerere.

Imeandikwa na MMM, Martin Maranja Masese.
 
View attachment 2785053View attachment 2785054

Historia nzuri kumbe siku zote nyerere hajawahi kua na rafiki wa milele, kila mtu maarufu wali tofoutiana aliogopa kuzidiwa umaarufu na wengine.
 
Atakuwa alikuwa mdini, Nyerere aliona mbali
Kuna baadhi ya watu mzee mchonga asinge wapiga PINI wangekuja msumbua sana huko mbele.

Baadhi walishaanza Ota mapembe.

Walipoanza kuleta ajenda za kidini, kibaguzi, kikabila.

Kuna baadhi ya mambo yule mzee alikua sahihi.

This time tuna RELIGIOUS FANATICS wanafanya juu chini kutaka kuturudisha kule ambako mzee mchonga alikokataa.

Inafika mahali unajiuliza Hawa watu Wana CONSCIENCE kweli au ni UMAAMUMA, UJUHA, au kutia kuonekana kwamba wao ni wanaharakati Fulani Fulani bila kujali kwamba wanachokipania chinichini kwa sura ya kificho kwamba kitaleta madhara ya Jumuiya hii ya watanganyika.
 
TITI MOHAMMED SALUM MANDANGWA; Mwamba​

FB_IMG_16977028548586903.jpg
a

liyemtikisa Nyerere na kupewa UHAINI.

Titi Mohammed Salum Mandangwa kazaliwa katika ya dini haswaa, lakini kapita vikwazo vingi. Amezaliwa 1926, Dar es Salaam na kufariki Johannesburg, RSA katika hospitali ya Net Care, Novemba 5, 2000. Aliishi miaka 74 ya machozi, jasho na damu.

NYERERE kama JIWE tu nguvu nyingi akili kidogo mwisho taifa linapata hasara za mara kwa mara.
Inasikitisha kwa kweli na siasa zake za ujamaa ziliacha mamia ya watu kuwa masikini. Image ukikutwa na sukari au kifurushi cha pipi nyumba ni kesi ya uhujumu uchumi
 
Darasa toka mwanangu Mohamed Said ambaye naona kama umebadili ID
 
Na alikuwa Mngindo na sio Mndengereko.
Mandwangwa ni watu kutoka wilaya kilwa na mpaka Leo wapo
 
Wangendereko na wangindo wote wametokea mkoa wa Lindi. Haya makabila hayana tofauti sana. Anyway. Karibu..
 
Back
Top Bottom