Wassira: Nasisitiza Vincent Nyerere sio Ukoo Wa Nyerere

Nawakumbusha wale wasomaji wa Biblia wakati Wanadamu wanajenga mnara ili wamfikie Mungu kule Babeli (Mnara wa Babeli). Kumbuka kuwa wote walikuwa na lugha moja na kwa umoja ule, ni wazi walikuwa wafike hadi mbinguni.
Mungu alichofanya ni kuwachanganya kwa kuwapa lugha tofauti ili wasielewane. Mnara ukaishia palepale!
CCM wamechanganyikiwa kama wa-Babeli, wanapiga kampeni moja lakini hawaelewani.
Babeli umeanguka !
 
Hao watu bwana wameishiwa sera, wanatapatapa tuu hawana muelekeo...wanapingana wao kwa wao, Wassira wa Musoma amefuata nini Arumeru?Kweli wameishiwa point...waoneeni huruma tu hata msiwapashe tena.Vincent kaza buti kamanda, uko juu ndio maana wanakuandama...
 
Wana JF nipo katika mkutano wa CCM katika kijiji cha Ngabobo Kata ya Ngarenanyuki jimbo la Arumeru na mhutubiaji mkuu ni Ole Sendeka mbunge wa Simanjiro na Stephen Wassira Mbunge wa Bunda.

Wassira anasema akija hapa mtu akajitambulisha kwa jina la Nyerere mumfukuze maana anadanganya, Nyerere alishakufa na alikuwa CCM hakuna Nyerere CHADEMA na mtu wa huko Musoma alipozaliwa mwalimu Nyerere na anajiita tu hili jina.

Ole sendeka anasema Wamasai msikubali kuamuliwa na watu wa Musoma, wa Musoma wakae hukohuko kwao huku watuachie wenyewe.

Kibaj anasema mumchague Siyoi kwa kumsaidia ana mzigo mkubwa nyuma yake ana familia kubwa ahurumiwe ili asadie kulisha wanaomtegemea na Mungu atawabariki wote.

Mkutano unafungwa ila kuna makundi makundi yanapinga kauli hizo na wapo wanaokubali.

My Take: CCM hakuna hoja wala mtoa hoja ni vituko tupu

Ni mimi Mgeni wenu wa Jamii Forum


Nomba uhusiano wa HIYO KAULI NA UCHAGUZI ARUMERU!
 
Ole Sendeka anawaambia wana Arumeru Mashariki wamkatae Nyerere anayemnadi mgombea wa CDM kwa sababu ni wa Musoma halafu anasahau kwamba yupo jukwaa moja na mtu wa Musoma akimnadi mgombea wa CCM. Huyu bwana kweli anafikiri kwa kutumia makalio. Mbaya zaidi hata Wasira akishangilia utumbo huo.

Ole Sendeka personal short history:

1: Div 0 Form vi @ Old moshi
2: Kampa mimba mwanafunzi huko Simanjiro;
3; Has poorest reasoning capability: almost null minded
eg; kasema wamasai wasiwasikilize watu wa Musoma akimsema Vicent Nyerere, "meanwhile yupo na Wassira
mtu wa Musoma as well, imagine, Div. 0 @ work,

Ole + Wassira i disregarded them long time, tunawajua they are not new, have no news, no views, hence it's
useless to review what they talk......
with big stomachs still hawashibi, i am out.... c u
 
Lazima Vicent Nyerere ni tishio. kwa nini CCM wanapanick sana na uwepo wake huko Meru? Na huyu Wassira ataacha lini kusema uwongo? Baba yake Joshua, mchungaji Nassari kamuumbua jana, leo anaamkia uwongo mwingine! amedanganya mangapi huyo huko wizarani?

Just imagine: ameacha kazi yake ya uwaziri anapiga jalamba huko Arusha....

Ndio mawaziri wetu hawa
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom