Wassira: Nasisitiza Vincent Nyerere sio Ukoo Wa Nyerere

Nimeshangazwa na aina ya kampeni za magamba,kwa mfano; Ole Sendeka amesema Wamasai wasiwasikilize watu kutoka Musoma!SWALI JE,Wasira anatoka WAPI? AMA KWEI NYANI HAONI KUNDULE.
hamjaelewa bado? Kwa ccm neno nyerere ni mtaji, cdm inaonekana kuwapiga bao kwa kumtumia memba wa familia ya JKN ktk kampen, nionavo ni kama saikolojia itawafanya wameru kuamini kuwa nyerere & family wamejiunga cdm! Hawaongei hivo kimakosa kuna jambo wanaliona hapo likiiwaaribia BWM hakumshambulia vicent kimakosa! Uwepo wa kiboko arumeru ni kichomi kwa ccm!
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Sendeka aende kwanza kumtoa mwanafunzi aliyezaa nae na kumficha kwa kutoa ng'ombe wengi kwa walimu na familia ktk tarafa ya sukuro simanjiro.
 
Wassira na Sendeka hatutawashangaa kusema hayo, wasingesema ndiyo tungewashangaa maana kama Mkapa kathubutu we ulitegemea nini kutoka kwa hawa? "Mtoto wa nyoka ni nyoka"
 
Wanasiasa wanapotegemea kura za huruma ili kupata ushindi bila kuangalia masuala (issues) muhimu yanayowakabili watu wa Arumeru Mashariki ni dalili tosha ya kufilisika kisiasa.

Hivi masuala la ardhi, maji, elimu, huduma za afya, mazingira na mengine ambayo CCM wameshindwa kuyatatua kwa miaka 50 nani atayatatua? Watu wa Arumeru Mashariki ni wajibu wao kumchagua mbunge ambaye anakerwa na issues na siyo masuala binafsi kama kuwa na familia kubwa tegemezi.

Mpira uko kwenu wapiga kura hapo tarehe 01.04.2012
 
za kweli hizo?au habari na dawa

siku zote tunasema ccm ndo mbaya wa watanzania kuna watu wanadai ni baadhi ya watu waliomo serikalini. Hizi kauli za uropokaji bila kuangalia nyuma yako kuna nini ndo zilizopo serikali. Kila waziri anaongea chake hata kama kitamkwaza mwenzie. Haya mambo yameasisiwa na chama kikiwa kinapigana in an end stage. Ukisikiliza kauli zao hakuna utofauti na muuaji anayekaribia kufa,atakuwa anaropokaropoka tu.
 
Ole Sendeka hakumponda Wassira kwa sababu Wasira ni mwanaArusha kichama, yeye ni mlezi wa chama mkoa wa Arusha, so haimuhusu kabisa hoja kwamba yeye pia ni wa Musoma
 
hivi akiwa mtoto wa nyerere ama la wananchi wa arumeru wananufaika nini? Na uhusiano huu? Mnapoteza muda kwa mambo ya kijinga!
 
Nimeshangazwa na aina ya kampeni za magamba,kwa mfano; Ole Sendeka amesema Wamasai wasiwasikilize watu kutoka Musoma!SWALI JE,Wasira anatoka WAPI? AMA KWEI NYANI HAONI KUNDULE.

Wassira ni mlezi wa CCM Arusha, so yeye ni MwanaArusha. Tafakari kwa undani!
 
Wana JF nipo katika mkutano wa CCM katika kijiji cha Ngabobo Kata ya Ngarenanyuki jimbo la Arumeru na mhutubiaji mkuu ni Ole Sendeka mbunge wa Simanjiro na Stephen Wassira Mbunge wa Bunda.

Wassira anasema akija hapa mtu akajitambulisha kwa jina la Nyerere mumfukuze maana anadanganya, Nyerere alishakufa na alikuwa CCM hakuna Nyerere CHADEMA na mtu wa huko Musoma alipozaliwa mwalimu Nyerere na anajiita tu hili jina.

Ole sendeka anasema Wamasai msikubali kuamuliwa na watu wa Musoma, wa Musoma wakae hukohuko kwao huku watuachie wenyewe.

Kibaj anasema mumchague Siyoi kwa kumsaidia ana mzigo mkubwa nyuma yake ana familia kubwa ahurumiwe ili asadie kulisha wanaomtegemea na Mungu atawabariki wote.

Mkutano unafungwa ila kuna makundi makundi yanapinga kauli hizo na wapo wanaokubali.

My Take: CCM hakuna hoja wala mtoa hoja ni vituko tupu

Ni mimi Mgeni wenu wa Jamii Forum


Haya ni malumbano ya kijinga. Utadhani kwamba usipozaliwa ukoo wa Nyerere basi wewe hufai kuwa mwanasiasa. Tena wanaotamka hivyo wala hawatoki ukoo wa Nyerere lakini wako bize ku-disown wenzao badala ya kunadi mgombea wao. Kwani usipozaliwa familia ya Nyerere wewe ni second class citizen?
 
Back
Top Bottom