Kila mara wananchi tulipohoji kuruhusiwa Kwa wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi kuingia nchini kununua mazao ya vyakula mashambani kwa pesa za kitanzania, tulijibiwa kuwa " Tusimpangie MKULIMA wapi auze mazao yake".
Pesa za Umma zimetumika kuagiza mbolea na pembejeo za KILIMO nje ya nchi Kwa Dollars, iweje wafanyabiashara Kutoka nje ya nchi waruhusiwe kununua nafaka mashambani kwa pesa za madafu?
Pesa ya wananchi imetumika kuweka RUZUKU kwenye Bei ya mbolea Ili MKULIMA anunue Kwa Bei himilivu, iweje wafanyabiashara Kutoka nje waruhusiwe kwenda mashambani kununua mazao Badala ya kununua masokoni?
Tukilea mtindo huo kuzoeleka, KARIAKOO itakosa wanunuzi Kutoka nje ya nchi maana watakimbilia mashambani kumpiga MKULIMA.
Makampuni Kutoka nje yataingia mashambani kununua maembe, machungwa, parachichi nk nk, masoko yetu yatafanya KAZI Gani kama mnyororo huo utafupishwa kiasi hicho?
Kwanini Serikali itumie tena hazina ya pesa za kigeni kuagiza Mchele na vyakula nje ya nchi wakati ingeweza kuyanunua mazao hayo muda huu na yakatunzwa katika maghala yaliyoko katika mikoa mbalimbali nchini?
Jukumu mojawapo muhimu la wizara unayosimamia ni kuhakikisha MKULIMA ananufaika na JASHO lake, lakini pia wizara inawajibika kuhakikisha inadhibiti mfumuko wa Bei holela.
USHAURI.
1. Wanunuzi wa mazao ya vyakula Kutoka nje waelekezwe kununua mazao kwenye maghala ya Serikali au kwenye masoko makubwa ya mikoa na wilaya na waje na Dollars, maana hivi sasa Nchi yetu Ina uhaba wa pesa za kigeni.
2. Vikundi vya wakulima viwezeshwe mikopo Ili vifanye package ya bidhaa zao Ili wauze nje ya nchi Kwa pesa za kigeni.
3. Maghala ya Serikali yafunguliwe katika miezi ya September Hadi February Ili kusaidia wakulima na wananchi kununua vyakula Kwa Bei nafuu kipindi ambacho wanasubiri kukomaa Kwa mazao Yao.
Kwa kufanya hivyo, Serikali itaweza kudhibiti mfumuko wa Bei maana itajua Kwa HAKIKA demand ya soko la ndani ni kiasi Gani hivyo kuuza ziada nje bila kuathiri Bei katika masoko ndani ya nchi.
ANGALIZO;Lipo TISHIO la njaa litakaloikabiri Dunia miaka michache ijayo hivyo, Nchi inatakiwa kuhakikisha inaweka akiba ya CHAKULA itakayodumu angalau Kwa miaka mitatu Ili kuhakikisha utulivu unakuwapo nchini endapo tutapitia kipindi hicho kigumu.
Mungu ibariki TANZANIA.
Amen.