Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama yatembelea maghala ya jeshi na chuo cha taifa cha ulinzi

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
738
478
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA YATEMBELEA MAGHALA YA JESHI NA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI NA KUFURAHISHWA NA UTEKELEZAJI WA MIRADI HIYO

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Stergomena Tax, machi 16, 2024 ameshiriki katika ziara ya kikazi ya Kamati ya Bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama kukagua miradi ya maendeleo inayoendeshwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga kupitia Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Maghala ya kuhifadhia vifaa ya Gongolamboto na Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Kunduchi, Dar - es - Salaam.

Kamati hiyo ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama iliongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Vita Rashid Mfaume Kawawa ilikagua utekelezaji wa mradi wa maghala mapya yanayojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kambi ya Gongolamboto na baadaye kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi ambapo pia ilikagua mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi za washiriki wa kozi za chuo hicho.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama ilipongeza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika kusimamia miradi hiyo ya Kimkakati Jeshini na kwa kuhakikisha pesa inayotolewa na Serikali inatimiza malengo yaliyokusudiwa. Aidha Kamati hiyo ya Bunge imeonyesha kufurahishwa na Ubora wa majengo na Maghala hayo yanayojengwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
 

Attachments

  • IMG-20240317-WA0034.jpg
    IMG-20240317-WA0034.jpg
    493.3 KB · Views: 5
  • IMG-20240317-WA0035.jpg
    IMG-20240317-WA0035.jpg
    247.7 KB · Views: 5
  • IMG-20240317-WA0033.jpg
    IMG-20240317-WA0033.jpg
    202 KB · Views: 6
  • IMG-20240317-WA0032.jpg
    IMG-20240317-WA0032.jpg
    215.9 KB · Views: 6
  • IMG-20240317-WA0030.jpg
    IMG-20240317-WA0030.jpg
    332.7 KB · Views: 6
  • IMG-20240317-WA0028.jpg
    IMG-20240317-WA0028.jpg
    316.3 KB · Views: 5
  • IMG-20240317-WA0031.jpg
    IMG-20240317-WA0031.jpg
    530.3 KB · Views: 4
  • IMG-20240317-WA0027.jpg
    IMG-20240317-WA0027.jpg
    409.5 KB · Views: 5
  • IMG-20240317-WA0023.jpg
    IMG-20240317-WA0023.jpg
    355.3 KB · Views: 4
  • IMG-20240317-WA0029.jpg
    IMG-20240317-WA0029.jpg
    435.6 KB · Views: 5
Watu wajinga kweli Hawa.

Usalama na ulinzi wa Taifa, sio tu mabunduki.

Usalama na Ulinzi ni pamoja na CHAKULA.

Ni kweli wamejithibitishia kua Mchele, maharage ya msaada ya GMO, ni Afya Kwa Watanzania???.


JPM alipiga marufuku COVID-19 V.. akaonekana mshamba, ila Sayansi ikaja kuthibitisha kua JPM alikua sahihi.



Mama yenu akaja kuruhusu, Et tu kuwaridhisha wamataifa, diplomasiaa ??.


Sahizi kakubali Mahindi na Mchele...katika Nchi ambayo 70% ni mapori

Waziri wa Kuliko, Mifugo, MJUAJI BASHE aliendelea kuchukua Vijana wa Kishua na kuwapeleka Ulaya kujifunza kilimo😅😅


Hivi Waafrika, tulilogwa na nani??.

Anagalieni KAPTEN IBRAHIM TRAORE wa Botiswana, anavyofanya mapinduzi ya kilimo Kwa vitendo .
 
photo_2024-03-17_18-13-18.jpg
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt Stergomena Tax, leo Machi 16, 2024 ameshiriki katika ziara ya Kikazi ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kukagua miradi ya maendeleo unayoendeshwa na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga kupitia Jeshi la Ulinzi wa Tanzania Maghala ya Kuifadhia Vifaa ya Gongolamboto na Chuo cha Ulinzi wa Taifa, Kunduchi, Dar-es-Salaam.
photo_2024-03-17_18-13-21.jpg

photo_2024-03-17_18-13-22.jpg
Kamati hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wake, Vita Rashid Mfaume Kawawa imekagua utekelezaji wa mradi wa maghala mapya yanayojengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kambi ya Gongolamboto na baadaye kamati hiyo pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ilitembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi ambapo pia ilikagua mradi wa Ujenzi wa nyumba za makazi za washiriki wa kozi za chuo hicho.

Kamati imepongeza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika kusimamia miradi hiyo ya Kimkakati Jeshini na kwa kuhakikisha pesa inayotolewa na Serikali inatimiza malengo yaliyokusudiwa.

Aidha, Kamati hiyo ya Bunge imeonyesha kufurahishwa Ubora wa majengo na Maghala hayo yanayojengwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania.
photo_2024-03-17_18-13-15.jpg

photo_2024-03-17_18-13-33.jpg
 
Back
Top Bottom