Comi
JF-Expert Member
- Oct 2, 2011
- 3,328
- 955
Baraza la bakwata latoa tamko kuwataka waumini kushiriki katika sensa ya mwaka huu ili kuiwezesha serkali kuendelea kuboresha mahitaji ya watanzania,pia sheikh mkuu amewaambia waendelee kutetea mambo yao ya msingi
SHEIKH Mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba ametoa msimamo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), akiwataka Waislamu wote nchini kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26, mwaka huu.
Mufti Simba ameonya kile baadhi ya waislam kufanya uchochezi kwa wananchi ili wasishiriki zoezi la sensa na kusema BAKWATA haihusiki.
Akisisitiza umuhimu wa Waislam kujitokeza kuhesabiwa, Mufti Simba alisema, "Mimi kama kiongozi wa Waislamu natoa wito kwa Waislamu wote hapa nchini, kushiriki kwa ukamilifu katika zoezi la Sensa litakalofanyika nchini mwetu."
Aliongeza: "Katika nchi yetu Sensa zimefanyika nyingi miaka ya nyuma na hazikuhusishwa na dini wala ukabila, ni jambo lililo zoeleka na kukubalika na wote''
Ameonya wale wote wanaochochea waislam kukwamisha juhudi za serikali kwa minajili ya udini.
Source: Mwananchi | Jambo leo | Habari Leo