Mufti Issa Shaaban Simba, Sheikh Mkuu wa Tanzania ametoa kauli murua kabisa ya kama kiongozi wa BAKWATA.
Sensa ya mwisho ya 1967 iliyokuwa ina harufu za kikoloni kutugawa kwa makundi ya dini, kabila haina mashiko mwaka huu 2012. Hivyo kama kuna taasisi au mtu anayetumia takwimu za mwaka 1967 ni vizuri kuainisha kuwa ni miaka 45 tangu sensa ya mwisho iliyokuwa na vipengele vya dini na haina mashiko sasa.
Serikali, taasisi na watu binafsi sasa ni wakati wa kusonga mbele na kuachana na kutaka kujua dini ipi ina idadi ya watu wangapi hilo tuwaachie taasisi zao za dini kufanya jambo kwani serikali haina dini.
Wapo watakaopingana na Mufti Issa Shaaban Simba, mfano watakaosema mbona Uingereza ktk sensa yao wanataka kujua dini ya mtu hivyo nasi tuige. Uingereza ni nchi ya Kikristo (Church of England), Malkia/Mfalme ni Kiongozi mkuu wa Church of England, bendera ya England ina symbol ya Msalaba na tumeona ktk Euro 2012 football competition washabiki wa England wamebeba bendera yenye Msalaba kuainisha kiaina kuwa ni nchi ya mfumo Kristo.
Uingereza wanataka kujua dini ya wakaazi wa Uingereza kwa vile wakaazi wenye dini nyingine kama Uislamu, Uhindu, Budhha n.k ni watu wenye rangi, desturi tofauti na Waingereza asilia (Asilimia zaidi ya 90 ya wakaazi wa Uingereza ni watu weupe wanaojibainisha na Ukristo hata kama si waumini wa kwenda Kanisani).
Sisi Tanzania asilimia 99 ya wakaazi wa Tanzania ni wa rangi nyeusi, mila na desturi zinaingilia kwa sana hivyo hatuna haja ya kuwa na kipengele cha dini ktk sensa kuwatambua watu wa dini nyingine (Rangi) kama Uingereza, sisi hatuna hofu ya wageni wa rangi nyingine (dini nyingine) kubadilisha U-Tanzania wetu.
Mufti Issa Shaaban Simba, Sheikh Mkuu wa Tanzania na BAKWATA wanastahili kupewa pongezi kwa kufunguka kwa staili ya umoja wa Tanzania kwanza na pia wadau wote kuwa makini na kutumia takwimu za sensa zilizopitwa na wakati kama sensa ya mwaka 1967 yenye harufu ya kasumba ya mkoloni kutugawa.