Wabunge wote wa upinzani watoka bungeni baada ya Spika kukataa kuahirisha bunge

naona sasa wameamua kujifunza kwa vitendo kutoka upinzani,ccm ni chama pinzani toka siku nyingi sema hawajijui tuuuuu
 
Ni mnafiki sana naona watu wamemshitua kuwa umeabisha kwa kukataa muongozi na umewapa chati wapinzani ya kutusema.
 
Vodacom walipoendesha shindano la Miss Tanzania baada ya kuzama kwa Mv Spice, wazanzibari walisusia msaada wa Vodacom, leo Spika kagoma kuahirisha bunge wakati Hamad Rashid katoa taarifa. Ni wakati sasa wa wabunge wa Zanzibar bila kujali itikadi zao wasusie vikao vya bunge!
 
Huyu mama anapaswa kujua kuwa wanaokufa ni watanzania wenzetu , kitendo cha kukosa quoram ya kupitisha bajeti ndio anaamua kuahirisha ni usanii wa hali ya juu kabisa.
 
wakuu naona nchimbi katoa hoja ya kuhairisha bajeti na bunge limekubali. ni aibu kubwa kwa makinda kwani kakataa nini na sasa kakubali nini. ni aibu kubwa kwa magamba. wananchi wanaona kila kitu kinavyokwenda na serikali yao dhalimu inavyowafanyia.
 
Huyu Mama anafanya kazi kwa kufuata kaambiwa nini aseme bungeni. Huyu mama alitumwa kutimiza malengo ya watu waliomuweka. Hawezi kufanya maamuzi yake mpaka apate kimemo ni kipi cha kufanya. Nadhani uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana
 
  • Thanks
Reactions: FJM
si alisema kuairisha bunge mpaka labda bahari iwe chamwino inamaana sasa imesogea.?
 
Wabunge wa ZNZ hata wa CCM Wameshirikiana na wa upinzani kwenye kutoa tamko juu ya msimamo wao kutoka nje
 
huyu mama kawa kichekesho leo, mwanzo kakataa kuhairisha Bunge, baada ya wabunge kutoka Nje akaona imekula kwake mara moja akahairisha Bunge kwa aibu kubwa, Nchi hii haina Spika wa Bunge

Hatuna Spika hapa! Kuna mama mmoja tu kapewa nafasi ya kuamua atakalo, anayeitumia vibaya pia nafasi hiyo!
 
Hii Bajeti ya Mambo ya ndani kutokana na maovu yanayofanywa na wizara hii inaweza chukua hata week maana ni hao hao wa usalama na mambo mengine wamekuwa wakiruhusu hata kama Boti imejaza ........Mungu yu pamoja nasi
 
Kwa msisitizo mkubwa, nashauri wabunge wote wa upinzani wafanye press conference sasa hivi, watoe pole kwa waliokutwa na maafa, na wawaeleze watanzania kwa nini wamemua kutoka nje ya bunge. Na baada ya hapo baadhi yao wasafiri haraka kwenda Zanzibar. Hilo tu. Makinda na wabunge wa CCM waendelee na bajeti yao ya ulaji.

Kwa Kanumba bunge lilisimama, IGP mstaafu hakuna kitu, mpigania uhuru Mzee Kyaruzi hakuna kitu, watu 200 Zanzibar wanazama wanaendelea as if hakuna chochote kilichotokea. Wabunge wa CCM wanamuwakilisha nani?

Halafu kesho kila mbunge wa CCM ataanza kwa kutoa salam za rambirambi!Wapuuzi sana hawa awtu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom