Spika wa Bunge Tulia Ackson ashitakiwa Kwa Wananchi , namba yake ya simu yawekwa hadharani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,721
218,273
Pamoja na mambo Mengine kwenye viwanja vya furahisha Mwanza Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika amewaagiza wananchi kumpigia simu Spika huyo ili kumlazimisha awaondoe Bungeni wabunge 19 maarufu kama COVID 19 , ambao amedai wamewekwa bungeni humo kinyume cha sheria

Mnyika amedai kwamba ni vema kila mwananchi akampigia simu au akamuandikia SMS Spika ili kumtaka haraka aondoe Wabunge wasio na Chama Bungeni humo , amedai kesi iliyo mahakamani haina uhusiano wowote na wao kuondolewa bungeni .

Namba ya Spika imetajwa kuwa ni 0784 763 *** ambayo baada ya kuifuatilia tumejiridhisha kwamba , imesajiliwa TCRA kwa jina la Tulia Ackson Mwansasu

Kazi kwenu wananchi , namba za simu za viongozi siyo siri , ndio maana za Ma RPC na IGP zote ziko hadharani , hawakuzitoa kama mapambo , wametupa ili tukiwa na lolote tuwapigie
 
Hapa chadema ndio maana mnaitwa chama cha wauni…..hivi unawekaje namba ya mtu hadharani! Huu ni ushamba wa hali ya juu! Hiki ndio chama kinataka kipewe nchi kinatenda ujinga huu na wakijua ni kosa!

Hivi mnawapa namba wananchi ili wamtukane tuu halafu mpate nini?
 
Mnyika anajua Sheria vizuri, kutoa namba ya mtu tena kwenye Public bila ridhaa yake ni kosa kisheria. Mtu anaweza kwenda lodge au gesti akafanya uhalifu kwenye kitabu Cha wageni akajaza namba ya spika. Sio Kila mnayemuona hapo ni mtu mwema.
NB: Sipo upande wa Dr. Tulia.
 
Tulia anaweza kwenda Mahakamani akiona kaonewa
 
NIJARIBU BAHATI, nimechoka ku-date na vitoto vya 2000

Mazeee, anajibu text zangu fresh tuu
Ntawapa mrejeshoo
 
Hapa chadema ndio maana mnaitwa chama cha wauni…..hivi unawekaje namba ya mtu hadharani! Huu ni ushamba wa hali ya juu! Hiki ndio chama kinataka kipewe nchi kinatenda ujinga huu na wakijua ni kosa!

Hivi mnawapa namba wananchi ili wamtukane tuu halafu mpate nini?
We unawaza kweli hao wavuta bangi wapewe nchi? Hata wao wenyewe hawazi hayo
 
Back
Top Bottom