Senegal: Bunge lapitisha azimio la kuahirisha Uchaguzi Mkuu hadi Desemba 15, 2024 licha ya vurugu kuzuka Bungeni

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,119
1707205499292.png
SENEGAL: Wabunge wa chama Tawala na wengine wanaounga mkono Serikali, wamepiga Kura na kupitisha ombi la Rais Macky Sall, la kuahirisha Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Februari 25, 2024 ambapo sasa umesogezwa mbele hadi Desemba 15, 2024 .

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wabunge wa upinzani kutolewa ndani ya Ukumbi wa Bunge kutokana na kupinga mabadiliko hayo yaliyoibua vurugu Bungeni pamoja na maandamano makali kutoka kwa Wananchi wanaoshinikiza Uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa awali.

Kwa uamuzi huo, Rais Macky Sall atabakia kuwa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya muda wa Kikatiba hadi pale mrithi wake atakapopatikana. Sall alitakiwa kuondoka Ikulu Aprili 2, 2024 kama Uchaguzi ungefanyika Februari 25, 2024.

Tangazo la kuahirishwa kwa Uchaguzi limeripotiwa kuzusha vurugu katika Miji mbalimbali ya Taifa hilo, hali iliyosababisha Serikali kuziagiza Kampuni za Simu kuzima Huduma ya Intaneti kwa madai kuwa inatumika kusambaza taarifa za Uchochezi na Machafuko.
 
Kuondoka ataondoka tu mana hawamtaki hana namna
Hii Dunia ina watu wa hovyo huyu Sall alitishia kuivakia Gambia amtoe Rais aliekatalia madarakani yeye nae tumtumie jeshi tumtoe shenz
 
Nchi ya hovyo sana hiyo bora hata wametolewa Afcon mapema Viongozi wao wana tamaa sana..
 
Back
Top Bottom