Wabunge wote wa upinzani watoka bungeni baada ya Spika kukataa kuahirisha bunge

Mpaka sasa hakuna Quoram bungeni sijui hiyo bajeti ataipitisha kwa utaratibu gani , ama atalazimisha ?

Bajeti inahusu waziri wa mambo ya ndani ambaye jeshi la uokoaji na zima moto liko chini yake badala ya kumpa nafasi ili aweze kutoa maelekezo mbalimbali yeye anaendesha kikao AIBU KWA WABUNGE WA CCM WALIOPO NDANI YA UKUMBI
 
Spika ameshauriana na serikali awezi kujitungia/kujihamulia. Hana utu na washauri wake ni wanafiki. Hukumu ni hapahapa duniani naona 2015 ni mbali sana.
 
Kwa msisitizo mkubwa, nashauri wabunge wote wa upinzani wafanye press conference sasa hivi, watoe pole kwa waliokutwa na maafa, na wawaeleze watanzania kwa nini wamemua kutoka nje ya bunge. Na baada ya hapo baadhi yao wasafiri haraka kwenda Zanzibar. Hilo tu. Makinda na wabunge wa CCM waendelee na bajeti yao ya ulaji.

Kwa Kanumba bunge lilisimama, IGP mstaafu hakuna kitu, mpigania uhuru Mzee Kyaruzi hakuna kitu, watu 200 Zanzibar wanazama wanaendelea as if hakuna chochote kilichotokea. Wabunge wa CCM wanamuwakilisha nani?
 
hamna akili za kupimia.

Uwezo wake ni mdogo sana, hawezi kupima upepo. Na historia inaonyesha kuwa watawala wote waliokuwa wanakwenda kuanguka akili zao zilikuwa zinafungwa na kufanya mambo kama hawajielewi.
 
wabunge wote wa upinzani yaani wa CUF, CDM, TLP ,NCCR wametoka bungeni kupinga kitendo cha spika kukataa kuahirisha bunge kwa dharura ili kuweza kutoa nafasi kwa serikali kuchukua hatua dhidi ya meli inayozama Znz.

Alitoa hoja Hamad Rashid kuwa Bunge lipitishe bajeti kabla ya mawaziri kuhitimisha ili kutoa nafasi kwa wabunge kufuatilia na kuweza kusafiri. Spika akamjibu kuwa hoja hiyo ingefaa kama maafa yametokea karibu na Bunge kama Chamwino etc ili wabunge waende wakatoe damu .

Hali ni mbaya , Bunge linapitisha bajeti kwa suala gani?
kiranja mkuu, vipi koramu imetimia ili bajeti ipite? maana wabunge wengine wa magamba wako chako ni chenu wanapata mambo mida hii. ua ndo wanapigiwa cm waje waokoe jahazi? kanuni zasemaje mkuu? bunge jeupeeeeeeeee.
 
poleni wazanzibar, ni bora mubaki na nchi yenu kujiunga na tanganyika mtakufa kila siku, huku atuna watalamu watendaji wa kuchunguza vyombo vya maji ila tuna watalamu siasa na masilahi mbele kama tai

pole sana wazanzibar.
 
....wanaweza. Asipowazingua, mtajuaje kama anaweza na ana mamlaka?????.

Du, kweli mawazo yako nayo ni ya hovyo kama jina lako lilivyo, hivi hapo anataka kuwazingua wabunge wa upinzani ili iweje? Kwani walio zama si hata wanachama wa magamba/mabwepande lazima na wenyewe wapo? au kulikuwa na ndugu wa opposition tu? Hebu badiri jina nafikiri na mawazo yako yanaweza kubadirika!
 
Huyu mama ni janga la kimataifa, anaendesha bunge kama shirika lake la misaada..sijui kama tutafika kwa mwendo huu, na wabunge wanamchekea sana huyu mama, na hawa wabunge wa vyama vingine watambue kuwa CHADEMA na wabunge wake wanapokuwa wanapigania haki pale bungeni uwa hawafanyi utani yule mama ni tatizo.
Tatizo wabunge wengi wameenda mjengoni kwa kutumia mbinu chafu ili waweze kuendeleza mambo yao bila bughudha toka mkono wa sheria. Mtu hawezi hata kubuni namna ya kumsaidia mpiga kura zaidi ya kumpa elfu moja hadi elfu kumi, itamsaidia nini mtu karne hii ya 21 kama siyo tusi? Nasema tena wabunge wengi 80% wapo mjengoni lakini hawajui hata nini wanatakiwa kufanya majimboni mwao zaidi ya kuwanunulia pombe huku wakidhani ndo kuwatumikia wananchi wakati ndiyo kuwatia umaskini zaidi.
 
Naona Nchimbi katoa hoja ya kuliahirisha naye spika kwa unafiki wake anaahirisha lakini ni baada ya upinzani kutoka na kutoa tamko.
 
mbona naona kaliahirisha bunge sasa hivi? au kuna mtu kambonyeza? haya majitu bana
 
huyu mama kawa kichekesho leo, mwanzo kakataa kuhairisha Bunge, baada ya wabunge kutoka Nje akaona imekula kwake mara moja akahairisha Bunge kwa aibu kubwa, Nchi hii haina Spika wa Bunge
 
Huyu mama kwa aibu ndio kajifanya anahairisha sasa, yani kweli tuna spika wa ajabu sana. Nawashauri wabunge waanze mapambano ya kusababisha bunge lisitawalike. Maana kwa akili kama hizi ni upuuzi, watu zaidi ya mia mbili wanahofiwa kufa yeye anakaa kuleta hoja zake nyepesi na dhaifu kama makamasi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom