Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Gender Sensitive,
Mkuu ni muhimu sana mnapoona mnashinda kitu mjue adui yenu kajiandaa vipi kukabiliana nanyi. CCM wanayo plan B kwa kila move au hatua waliyoichukua wakitegemea outcome fulani. Kama nilivyokwisha sema historia inatufunza mengi tumewaona kina Kolimba, Malima, Mwaikambo, Dr.Omar na wengine wengi ambao wameondolewa kimazingara na hakuna lililofanyika kabla wala baada ya..

Tumewapoteza viongozi hao na hakika tumebakia tukizungumza maneno tuliyolishwa kuhusiana na mapungufu yao badala ya nia ya wapiganaji hao. Hivyo Chadema mnatakiwa kujipanga kuweka guard ya kila mkijengacho kwani ni rahisi sana kwaCCM kupenya ndani na kuharibu kila mnalokusudia hasa ikiwa muda wenyewe ndio umebakia miezi tu. Hamna nafasi ya kujipanga upya..

Kuhusiana na mzee Mwanakijiji huyu mwache, ni mwandishi makini ambaye anataka kujua baada ya ushindi Chadema watafanya nini tofauti na CCM ktk maswala mengi ya kiitikadi hali mimi nimeisha mwambia huwezi kuingia vitani na biblia mkononi kama silaha yako hasa unapopigana vita na mwarabu. Shinda vita kwanza, kisha utahubiri biblia kwa hatua kwani Tanzania yetu leo hii wananchi wake hawafahamu kabisa kuhusiana na mfumo wa ITIKADI kutokana na UJINGA na kibaya zaidi UMASKINI wetu unaweza kupongeza itikadi inayowahubiri kwa zawadi na misaada kuwa ndiyo iliyo bora zaidi.

Maneno ya maana sana haya. Wengi hawajui siasa za Afrika zinaenda kiafrika.....
 
Boramaisha, "Jingine lililonistua ni kumsikia kiongozi mmoja wa Taasisi moja ya Uchumi nchini (anaweza akawa mwanachama wa CHADEMA) akizungumzia habari ya kutaka kuwepo kwa "middle class" nchini na akawahamasisha Watanzania walio Marekani kuungana na walio nchini kuanzisha hiyo 'middle class'" maana yake ni kuua wakulima, wafugaji, wavuvi, waokotaji mwituni, au kwa kifupi ni kuua "prosumers", yaani, "producers-cum-consumers" (wanaozalisha na kula au kutumia kile wazalishacho). Na vingi wazalishavyo havipitii kwnye soko la kisasa kuweza kutathiminiwa kuwa ni sehemu ya GDP ya nchi!

Huyo aliyesema hivyo (Naiko) ametumwa nini?
Wakuu samahani sana... hivi mnaelewa maana na sababu ya kujenga middle class?

Mnapopinga kitu kwanza tazameni hali halisi na ndio maana Mwanakijiji anatukamata kwa maswali ambayo majibu yake ni rahisi lakini mtazamo wa wengi unakanganya ukweli. Nchi yoyote duniani ina tabaka mbili - Walionacho na Wasikokuwa nacho. Njia pekee ya kuleta maendeleo ni kuondoa tabaka hizo kwa kujenga middle class ambayo kwa kila inapoongezeka kundi moja linapungua iwe matajiri au maskini kujaza middle class. Hata mkulima, waokota kuni wavuvi na kadhalika wapo ktk tabaka za utajiri na maskini hiyvo middle class inavunja tabaka na sio kuongeza maskini..

Hizi ni fikra za Kijamaa ati tunaweza kugawana umaskini kama haki ya usawa wa watu wote pasipo kutazama udhaifu wa mgao huo ktk kuendesha uchumi wa kile kilichozaliwa mwanzo.. Hata wewe ukiwa na millioni leo hii ni ujinga ukigawa kwa familia yako ya watu 10 ukitegemea kila mmoja atafanikiwa na hizo laki 10. Kumbuka tu kila mmoja wa ndugu zako ana interest zake na uwezo wa kuanzisha mradi, mara zote kutokana na umaskini ambao maisha yao hawajakamata mkonoi laki kumi wataishia kulewa na kuoa wake zaidi..Huu ndio ukweli na ni lazima falsafa yoyote ikubali mazingira haya..

Akili ni kuziwezesha hizo millioni kuzaa zaidi hali ukiwahusisha hao ndugu zako ktk uzalishaji na kuboresha maisha yao sambamba na mtaji unavyozidi kukua..Kwa njia hii unawahakikishia pato la kudumu kwa kila hatua ya maendeleo..Utajiri wako wa hiyo millioni utawaondoa ndugu zako toka umaskini na kuwa kati, wenye ajira ya kuwawezesha kununua vitu vingine ktk maisha yao. Huu mpango wa kugawana urithi ndio umefilisi nyumba na koo zote za wakazi wa Kariakoo kama sio nchi nzima..
 
Nashukuru sana kwa vijana wa mjini kuniwezesha kufikiri kama mtoto wa mjini. Hili la CCJ ukiliangalia kibongobongo ilikuwa ni upuuzi kama tuliosema mwanzo, vyama vimetosha. Hawa watu wanaodhani bongo utaleta elitism sijui kuongelea itikadi blah blah wanafanya theory exercise ambazo ni huku online na kwenye vitabu.

Sisi huku JF especially tulioko nje kwa miaka mingi tunasumbuliwa sana na tatizo la kuidiscuss bongo kwa kutumia prism ya nchi hizi tunazoishi, wakati bongo mapigo tofauti. Dawa ni kwenda kibongobongo tu, upinzani wajiunge kuondoa CCM kwanza, halafu hayo mambo mengine yafuate.

Hakuna haja ya vyama vya upinzani kugombea urais, JK ni automatic kutokana na mfumo wetu. Nguvu ziwekwe kwenye ubunge ili wananchi waone tofauti bungeni kati ya upinzani na hao vilaza wa CCM.

Zitto, Dr. Slaa na wengine mtakaoingia bungeni oct nawatakia uchaguzi mwema.
 
Wakuu samahani sana... hivi mnaelewa maana na sababu ya kujenga middle class?
Nchi yoyote duniani ina tabaka mbili - Walionacho na Wasikokuwa nacho. Njia pekee ya kuleta maendeleo ni kuondoa tabaka hizo kwa kujenga middle class ambayo kwa kila inapoongezeka kundi moja linapungua iwe matajiri au maskini kujaza middle class. Hata mkulima, waokota kuni wavuvi na kadhalika wapo ktk tabaka za utajiri na maskini hiyvo middle class inavunja tabaka na sio kuongeza maskini..
Sawa kabisa Mkuu, bila middle class nchi inakuwa polarised between the haves (+ve) na the havenots (-ve) na hii ni hali ya hatari kabisa kwani mlipuko kati ya matabaka haya mawili unaweza kutokea wakati wowote. Middle class hapa inakuwa kama cushion ni muhimu kabisa katika kupunguza mvutano/uhasama kati ya hayo makundi mawili (neutralization).
 
Moelex23,
Mkuu umesema kibongobongo... sawa JK akichukua Ikulu pasipo Upinzani ana madaraka makubwa sana ya kuua bunge hilo kwa kila hoja..unafikiri ata form serikali ya aina gani? kina nani watakuwa ministers.. Je, kama leo kaweza kuvuta mabillioni, think amepata mwanya wa mwisho kumalizia kabla hajatoswa yeye na CCM nzima atamalizia vipi?..
Ushindi wowote wa Wabunge pasipo Ikulu ni kujimaliza kiuchumi...Mobutu alivyojua tu kwamba kuna hatari ya kuondolewa alivuta hadi kuwa third richest in the world..Wapo madiketa wengi sana waliofikia kushindwa bungeni wakabakia wao wakaiba, wakaua na kumaliza Upinzani kwa nguvu ya jeshi la taifa. We don't wonna go there..... Tuchukue IKULU pia..
 
Mkuu Mkandara::

Kama CCM wameshindwa kukubali CUF 2000, 2005 kuchukua Zanzibar, unadhani hata JK akishindwa kura kuna mpinzani anaweza kupewa nchi?? Come on now, not only that, JK kwa kweli wananchi especially vijijini wanampenda, kwa hiyo bila hata kuiba kura hawezi kukosa 51% kwa mazingira ya nchi yetu yalivyo.

Ingekuwa kuna uwezekano, ningekuwa napiga debe, lakini Reality ni Reality.
 
Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.

Wanachama wa CCJ na viongozi waliobaki waiunge CHADEMA kwenye uchaguzi huku wakiwa bado ni wanachama na viongozi wa CCJ alafu baada ya uchaguzi CCJ iendelee kupigania usajili wa kudumu na kuendeleza itikadi yake? Nilifikiri sasa hivi tutasikia mwanachama mmoja wa CCJ akitake over nafasi za Viongozi wa CCJ waliohama.
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.

Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.

Mwanakijiji,nadhani hii ilikuwa fursa nzuri kwako kukiri hadharani kuwa YOU GOT THIS WHOLE THING WRONG.To err is human but to rectify is greatness.Unapotuambia "si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo" unamaanisha viongozi gani tena?Au kulikuwa na uongozi wa CCJ wa hadharani na uongozi mwingine wa msituni?Au ndio ile mikakati ya siri uliyokuwa unatuaminisha itatokea lakini kilichotokea ni kile tulichotarajia wengi?

Of course,kama ambavyo sio kila kinachosemwa na uongozi wa kifisadi wa CCM lazima kifuatwe na wanachama wa chama hicho ndivyo ambavyo uamuzi na ushauri wa uongozi wa juu wa CCJ kwamba wanajiunga na Chadema haumaanishi kila mwana-CCJ awafuate.Hata hivyo,unless hao wana-CCJ wa "msituni" wana mkakati wa kuendeleza chama ambacho kwa sasa ni officially marehemu,kung'ang'ania ishu ya "ajenda za kipekee za CCJ" ni suala la kuchekesha kama sio kusikitisha.

Naamini waliojiunga na Chadema wamesoma alama za nyakati na kutambua kuwa mpiga ngumi ukuta hujiumiza mwenyewe.Hili linapaswa kuwa somo muhimu kwa sie wote tunaotaka kuiona CCM ikiondoka madarakani (japo umekuwa ukisistiza kuwa lengo la CCJ sio kuiondoa CCM madarakani) lakini tunaishi nje ya Tanzania (na hivyo kuwa somehow short-sighted katika ujuzi wa hali halisi ya siasa chafu za Tanzania).Na pengine fundisho la msingi ni kwamba tatizo la Tanzania na wanasiasa wake halijawahi kutokuwa na "ajenda za kipekee" bali kutafsiri ajenda hizo katika vitendo.Unaweza kubaki na imani kuwa Chadema haijafikia kiwango stahili "kama cha CCJ" lakini,sadly,utabaki unasapoti chama ambacho kwa sasa ni alomst non-existent.

Mzee,you were taken for a very long ride.And we told you!
 
Mkuu Mkandara::

Kama CCM wameshindwa kukubali CUF 2000, 2005 kuchukua Zanzibar, unadhani hata JK akishindwa kura kuna mpinzani anaweza kupewa nchi?? Come on now, not only that, JK kwa kweli wananchi especially vijijini wanampenda, kwa hiyo bila hata kuiba kura hawezi kukosa 51% kwa mazingira ya nchi yetu yalivyo.

Ingekuwa kuna uwezekano, ningekuwa napiga debe, lakini Reality ni Reality.
Amini maneno yangu JK anaweza kabisa kushindwa..what we need is someone maarufu na mwenye mvuto..Huko vijijini ndiko wanataka kuona mabadaliko kuliko mijini, hali yao imekuwa mbaya zaidi na kila unapoona mlolongo watu ktk mikutano ya Jk ni kwa sababu wanafikiria kuna pilau la Maulidi.

Kama kesho Salim au Dr.Slaa akisema atagombea kwa tiketi ya Chadema na kufanya ziara zake huko vijijini itakuwa pata shika! believe me Operation sangara inafahamika na kupokelewa vizuri vijijini kuliko mijini na hakika huyo Mpendazoe na wabunge wengine possibility yao kushinda ni ndogo sana ikiwa hatuna mtu kiti kikubwa.

Demokratic wasingeshinda majimbo yao dhidi ya McCain kama sii wananchi kumkubali Obama na hakika kila nchi huhesabika uwezekano wa chama kushinda viti vingi kutokana na mgombea wa kiti kikubwa. Ni Obama aliyewezesha Democratic kuchukua hata majimbo ya Republican na hao walioshinda ni wawakilishi wa sera za Obama..Ni rais anayekuja na Changes kisha wabunge ni wawakilishi wa agenda hizo.. How can u board a bus ambalo halina dereva kama sii kudandia train kwa nyuma..
 
Mkandara!
Don't underestimate CCM! Hapa aje Dr Slaa au nani huko vijijini ndiyo kwenye kifo chao.Tatizo kubwa la vyama vya upinzani havijaweza kujenga mtandao sehemu kubwa ya Nchi na hasa vijijini ilihali CCM kwa hilo imefanikiwa na inazidi kujizatiti.Hizi Kelele ni mijini na kwa wenye uelewa .Na kwa Taifa lenye wapiga kura takribani milioni 21 Hawa ni robo yao tu.
 
Kwangu mimi naona ni habari nzuri kwetu sisi wanamageuzi wapinzani, wataongeza nguvu hasa baada ya kufanyiwa ntimanyongo na msajili!
 
Mkandara!
Don't underestimate CCM! Hapa aje Dr Slaa au nani huko vijijini ndiyo kwenye kifo chao.Tatizo kubwa la vyama vya upinzani havijaweza kujenga mtandao sehemu kubwa ya Nchi na hasa vijijini ilihali CCM kwa hilo imefanikiwa na inazidi kujizatiti.Hizi Kelele ni mijini na kwa wenye uelewa .Na kwa Taifa lenye wapiga kura takribani milioni 21 Hawa ni robo yao tu.
Mkuu utashangaa kwamba CCM wanaweza shindwa kirahisi sana hasa baada ya mwalimu kuondoka. Mkuu NCCR na Mrema karibu wachukue nchi na hawakuwa na Mtandao wowote vijijini, CUF waliokuwa wame base mijini walitingisha uchaguzi uliofuata..

Ni uchaguzi uliopita tu ndio wabunge wengi wa CCM wameweza kupeta kirahisi kwa sababu wananchi walifikiria JK ndio tumaini lao against CCM yenyewe..Historia inaonyesha wazi CCM anaweza kushindwa tazama chaguzi ndogo walivyopita kwa taabu tena vijijini..

Sema CCM chama kubwa, hilo halina ubishi na wala siwezi kudiriki kuwakatisha tamaa wapinzani kina David ambao wanataka kupambana na Golath.. CCM wanaweza sana kupika matokeo na nguvu zote wanazo wao. Lakini for the first time ikitokea hivyo ktk mazingira tulokuwa nayo leo sijui kama mjini patakalika mwaka huu.
 
Sasa! ni kweli hawa CCJ walikuwa na wanachama? Dereva unapoondoka Abilia wafanye nini kabla ya kutafuta usafiri mwingine?
 
Nitafurahi endapo Chadema itatambua ukweli.... Ebu Slaa agombee urais 2010 halafu muone wimbi la 'panic 'ya CCM
 
chadema bado saana, hivi watu wa CCJ mbona wanataka kutoka kwa mgongo wa chedema/ Wangeanzisha chama chao tukakion -ina maana wanatanga tanga tu ili mradi waonyeshe ile mfa maji!! Poleni CCJ Hamkujipanga na sasa mnataka kufanya kile tukiitacho "kuzima moto" yaani kufanya mambo haraka haraka ktk hatua za mwisho!! Yaani kama ni mwamnafunzi anafanya assignment ya cku tatu kwa masaa mamwili ili akisanye kabla ya deadline .Na hiki ndo kifo cha wana CCJ Kisiasa maana nina imanai watadhibitiwa kwa uhakiaka!!
 
vyama vinakufa, fikra hazifi wala hazifungwi.
 
vyama vinakufa, fikra hazifi wala hazifungwi.
The thing is hata RA anafikiria hivyo hivyo! mkuu wangu kuna mjamaa wa fikra kama Kingunge? uliwahi au ulibahatika kumsikiliza mzee huyu akiongea ...Haya mtazame leo anayoyafanya nini na hizo itikadi...
Wapo watu wanaweza kuizungumzia Biblia au kuran hadi ukalia na machozi wape nafasi kidogo watakuibia hadi mkeo..Hakuna njia ya mkato be part of changes to come.
 
kama mifano yako hapo ni kweli kwanini tuwafuate hao wengine; tutajuaje na wenyewe hawatotuibia wake zetu?
 
Back
Top Bottom