Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Na mimi hilo linanishangaza sana, Jimbo la segerea kuna Rachel Mashishanga ameshatangaza nia ya kugombea na ninaamini kuwa angemuangusha yule mcheza Taarabu aliyepo sasa. Huyu mpenda zoe ana jimbo alilogombea sasa inakuwaje analiacha na kuja kutaka jimbo lingine. Bila kutueleza at least atahakikisha lile jimbo nalo linakwenda upinzani itakuwa ngumu sana kumwelewa huyu mtu. Afadhali angwekwenda ukonga na kumtoa yule Binagi ambaye ndiye anayetoa siri nyingi za chadema kwa CCM na inaonekana anataka kuwauzia jimbo la ukonga bei rahisi.

So far namsupport Rachel kubeba tiketi ya Segerea na atashinda.

Ndugu yangu sio vizuri kuzungumza allegations kama hizi in public halafu hazina ushahidi.Hata kama unampenda my sisy and my friend Rachel huna sababu ya kumsingizia mtu ili aonekane hafai.Kama unamkubali Rachel for Segerea then mfanyie kampeni ili ashinde kura za maoni,si kuwatukana watu wengine bure.Kama kweli Mzee Binagi ana kashfa hizo basi zilete Makao Makuu na ushaidi uliojitosheleza ili zifanyiwe kazi mapema.Si vema kuwa mashabiki bali tufanye serious analysis za kisiasa ili kukisaidia chama kupata wabunge wengi,tuache kujuana au sababu zingine zozote zile..
 
Hivi ni vijimambo tu mambo makubwa yanakuja hamtaamini macho na masikio yenu midomo itabaki wazi.
Si hivyo tu watapata mishangao hasa hawa sisi m watabaki wanajiuliza maswali yasiyo na majibu. Wavute pumzi kidogo tu.......
 
I have also heard this news from other sources also and seen the picture of Mpendazoe meeting Mbowe. I always thought CCJ was a fluke and I guess this proves it. Well if political parties were soccer teams I would say Chadema has just added to it's roster. How good of political players these new guys will be is yet to be seen.
 
Soon tutasikia Mpendazoe for president Chadema! I can see it coming...

Jamani,muwe mnasoma btn lines.Mpendazoe ameshatangaza nia ya kugombea Ubunge,Urais utakujaje tena?Naona maono yako yanamakengeza kama unavyodai eti unaona ndivyo itakavyokuwa.
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.

Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.
 
Gender Sensitive,
Hivi ikiwa CCM walifanya makusudi kuwakwaza CCJ wakijua kwamba mwisho wake vigogo wachache tu ndio watajiunga na Chadema..Kwa maana kwamba wapo vigogo ambao hawataweza ku cross over toka CCM kwenda Chadema kwa sababu za kihistoria ya chama hicho..vigogo wote waliotishia kuhamia Chadema au chama kingine walikolimbiwa..
Na habari za mjini zinasemekana kuwa wapo vigogo wa chama ambao wangependa sana kukihama chama lakini usalama wao utakuwa hatarini na hakuna sheria wala chombo cha kulinda maisha yao...

Je, Chadema imejiandaa vipi kuwahakikishia hawa watu usalama wao pindi wakiiunga na chama hicho!
 
Nimekupata Mkuu ila kwa kweli siwezi kujibu moja kwa moja kwakuwa mimi sio msemaji wa chama.Kama nitaruhusiwa kusema hayo basi nitamwaga mchele...Ila kifupi sidhani kama watasumbuliwa kwa kuwa tayari jamii inaona yanayotendeka kwahiyo kama kuna lolote litatokea nadhani kabala hata uchunguzi haujafanywa basi jamii itakuwa imeshajua,sidhani kama CCM watafanya hivyo.they have nothing to loose hata kama kuna kudni litajiunga na CHADEMA.
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.

Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.[/QUOTE]

Upande wa pili wa mstari,upi huo,kwa kuwa ninchofahamu CCJ ndio kimeshakufa kifo cha asili.Unamaanisha huna chama chochote kwa sasa?
 
mimi hawa akina mpendazoe na wenzake nawaita mashujaa wa demokrasia tanzania kwani wameonesha uthubutu wa hali ya juu wa ukomavu wa kisiasa japo tumewafahamu rasmi hivi karibuni.
 
hongera GS kwa mafanikio haya ya chadema na nashukuru kwa kutuhabarisha. ukiwa mmoja wa wapiganaji wake, fikisha hongera hizi kwa wenzako....

sasa MM anapaswa kukiri kushindwa kuuona udhaifu a kimkakati wa ccj. ...

toka mwanzo nilijua ccj hakitafika mbali, iliwahi hata kulumbana na MM hapa jamvini, yeye akitetea na mimi nikiponda... hususani sikuona hekima yoyote ya mpendazoe alipojivua uanachama wa ccm kwa style aliyochagua na nikatumia jina la utani kumwita mpendazote...

natahadharisha tena kuwa akigombea segerea, hatashinda na nashauri chadema wasimsimamishe segerea, labda kama ataamua kurudi kishapu.... tusubiri mtaona....

mie si pweza wala si sheikh yahaya.... ni mtazamo tu......
 
Gender Sensitive,
Mkuu ni muhimu sana mnapoona mnashinda kitu mjue adui yenu kajiandaa vipi kukabiliana nanyi. CCM wanayo plan B kwa kila move au hatua waliyoichukua wakitegemea outcome fulani. Kama nilivyokwisha sema historia inatufunza mengi tumewaona kina Kolimba, Malima, Mwaikambo, Dr.Omar na wengine wengi ambao wameondolewa kimazingara na hakuna lililofanyika kabla wala baada ya..

Tumewapoteza viongozi hao na hakika tumebakia tukizungumza maneno tuliyolishwa kuhusiana na mapungufu yao badala ya nia ya wapiganaji hao. Hivyo Chadema mnatakiwa kujipanga kuweka guard ya kila mkijengacho kwani ni rahisi sana kwaCCM kupenya ndani na kuharibu kila mnalokusudia hasa ikiwa muda wenyewe ndio umebakia miezi tu. Hamna nafasi ya kujipanga upya..

Kuhusiana na mzee Mwanakijiji huyu mwache, ni mwandishi makini ambaye anataka kujua baada ya ushindi Chadema watafanya nini tofauti na CCM ktk maswala mengi ya kiitikadi hali mimi nimeisha mwambia huwezi kuingia vitani na biblia mkononi kama silaha yako hasa unapopigana vita na mwarabu. Shinda vita kwanza, kisha utahubiri biblia kwa hatua kwani Tanzania yetu leo hii wananchi wake hawafahamu kabisa kuhusiana na mfumo wa ITIKADI kutokana na UJINGA na kibaya zaidi UMASKINI wetu unaweza kupongeza itikadi inayowahubiri kwa zawadi na misaada kuwa ndiyo iliyo bora zaidi.
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.

Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.[/QUOTE]

Upande wa pili wa mstari,upi huo,kwa kuwa ninchofahamu CCJ ndio kimeshakufa kifo cha asili.Unamaanisha huna chama chochote kwa sasa?

kwa sasa sijaona chama chenye kuwakilisha japo kwa kiasi fulani fikra na maono yangu kuhusu Taifa. CCJ bado inabakia kuwa ni fikra ambayo naweza kujenga kutoka hapo.
 
Good Move for FM/Team; Now chadema wajiimarishe zaidi; Chadema kiwe chama mbadala; mikutano ifanyike haraka ya wanachama na kuwatambulisha; musiende ktk maTV; nendenni waliko wananchi sasa;

Wajumbe kuchangia chadema andika neno "CHADEMA" kwenda 15710 ili kuongeza nguvu za kampeni; hakikisheni kama hiyo code bado inafanya kazi vizuri
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.

Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.

Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.[/QUOTE]

Upande wa pili wa mstari,upi huo,kwa kuwa ninchofahamu CCJ ndio kimeshakufa kifo cha asili.Unamaanisha huna chama chochote kwa sasa?
Tatizo la MMKJ, when it comes to CCJ, he is full of politics even in simple questions and matters!
 
Boramaisha, "Jingine lililonistua ni kumsikia kiongozi mmoja wa Taasisi moja ya Uchumi nchini (anaweza akawa mwanachama wa CHADEMA) akizungumzia habari ya kutaka kuwepo kwa "middle class" nchini na akawahamasisha Watanzania walio Marekani kuungana na walio nchini kuanzisha hiyo 'middle class'" maana yake ni kuua wakulima, wafugaji, wavuvi, waokotaji mwituni, au kwa kifupi ni kuua "prosumers", yaani, "producers-cum-consumers" (wanaozalisha na kula au kutumia kile wazalishacho). Na vingi wazalishavyo havipitii kwnye soko la kisasa kuweza kutathiminiwa kuwa ni sehemu ya GDP ya nchi!

Huyo aliyesema hivyo (Naiko) ametumwa nini?
 
Ni kweli wamejiunga Chadema, kumekuwa na mazungumzo ya muda mrefu kati yao na uongozi wa juu wa Chadema. Ikumbukweni mazungumzo baina yao na si uongozi mzima wa CCJ umetoa baraka hizo na hii haina maana waliounga mkono CCJ wote sasa nao wamefuata mkumbo. Kwa sisi wengine kuna mambo ambayo hatuwezi kuvunja kanuni kwayo kwa sababu ya political expediency or political opportunism if you will.
Uamuzi huu ni wa kueleweka kama tutakavyoona kuanzia wiki chache zijazo baada ya Bunge kuvunjwa.
Chadema itakapovuka mstari ule wa ajenga, nitakuwa mtu wa kwanza kuinga mkono kwa nguvu zangu zote. Kwa sasa bado wako upande wa pili wa mstari.

Upande wa pili wa mstari,upi huo,kwa kuwa ninchofahamu CCJ ndio kimeshakufa kifo cha asili.Unamaanisha huna chama chochote kwa sasa?

Kama namwelewa Mwanakijiji hakuwahi kuwa mpenzi wa Chadema bali alikuwa ni mwana CCM aliyechoshwa na uvundo uliotanda katika bonde CCM ilipopiga kambi na hivyo akawa anatafuta upenyo wa kupata hewa safi. Chadema hawakuweza kumhakikishia hiyo hewa safi kwa asilimia 100% lakini CCJ iliweza kumpa matumaini kwani si tu iliitia wasi wasi CCM na kuipiga tobo bali iliingia kwa staili na gia isiyo ya kawaida. Mimi ni moja wa watu waliomshangaa na wanaoendelea kumshangaa Mwanakijiji kwa msimamo wake huo lakini sasa namhakikishia kuwa huu upepo unaoanza kuvuma ni dalili ya ujio wa tsunami hivyo akae chonjo kwani tsunami haizuiliki. Nachukua hii nafasi pia kuwaomba wale wote walio na mapenzi mema na taifa hili wasikae tena kando kama watazamaji bali washiriki kwa vitendo, Tanzania yawahitaji - nchi inateketea !

Siku zote CCM imekuwa ndiyo mpiga zumari na watu kujimwaga ukumbini lakini safari hii waanze kufanya mazoezi ya kulisakata kwani muziki huu mpya ni moto wa kuotea mbali na una staili yake. Wamezoea kulikoroga na kuwaachia wanywaji, safari hii watalinywa wenyewe kwani tayari wazalendo wa kweli wamewasha indiketa na inabidi mafisadi wakae chonjo. CCJ haikufa bali ina evolve kama ilivyotarajiwa, lazima mkumbuke kuwa kuna walioshughulikiwa kimya kimya na sasa ni wenye sababu, uthubutu, ujasiri na nia ya kweli na thabiti ndiyo watabaki wamesimama baada ya kimbunga kupita, tukae tukijua hilo - Heko Chadema !
 
Back
Top Bottom