Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Wow.... GS, My friend;

I am proud of CCJ leaders na pia i am very proud of CHADEMA for accepting this change. Hii ndiyo ndoto yangu kwenye upinzani, fighting the common enemy.

Najua MMM naye atakua hepi na kusema ukweli huu ni uamuzi wa busara sana... UNGANENI NA KUWA NA SAUTI ZAIDI BUNGENI, ITS ONLY THEN NDIPO DEMOKRASIA YA KWELI ITAPATIKANA

BTW, HEBU CORRECT HIZO SPELLING, HAO NI OFFICE MATES KWA SASA

AT LIST THIS WILL ALSO SWING THE MEDIA ATTENTION TO UPINZANI

Nimekupata rafiki De Novo.Vipi B point lini tena?
 
TAMKO LA VIONGOZI WA CHAMA CHA JAMII (CCJ) KUWATAKA
WANACHAMA WA CCJ WAGOMBEE NAFASI ZA KUCHAGULIWA
KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO KUPITIA CHADEMA
UTANGULIZI
Ndugu Viongozi, Wanahabari, Wanachama na Wananchi kwa ujumla.
Tunayo furaha kubwa isiyo na kifani, kwa kuungana nanyi katika
mkutano huu ambao unaandika historia mpya yenye kuleta mabadiliko
ya kweli katika taifa letu la Tanzania. Historia ambayo itakumbukwa
kizazi hata kizazi, historia itakayowafanya Watanzania wajivunie na
kuifaidi nchi yao.
Ndugu zangu kabla sijaeleza nini kimetuleta hapa, napenda
kuwarudisha nyuma kidogo. January 18 mwaka huu sisi wananchi
wazalendo tulikutana jijini Dar es Salaam kutekeleza wajibu wetu
kikatiba wa kuunganisha mawazo yetu pamoja na kuunda chama cha
siasa kwa jina la Chama Cha Jamii (CCJ).
CCJ kilizingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu na
baada ya uhuru na kilibeba matarajio ya wananchi wa leo na kesho,
kikiwa na lengo kuu la kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia,
kiuchumi, kijamii, na kisiasa kwa faida yetu sisi sote na vizazi vijavyo.
USAJILI WA MUDA
Mwezi huo huo CCJ ilipeleka maombi ya usajili wa muda katika ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini. Na baada ya urasimu wa hapa na
pale, hatimaye Machi 3, 2010 CCJ ilipata cheti cha usajili wa muda. Hii
ilikuwa ni hatua ya mwanzo kabisa ili kiweze kuanza shughuli za
kutafuta wanachana na hatimaye kikitimiza masharti yaliyopo kwa
mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siasa ya 1992, kiweze kupewa usajili
wa kudumu.
Hata hivyo, toka mwanzo ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini,
imekuwa ikionyesha nia yake waziwazi ya kutotaka kukipa CCJ usajili
wa kudumu hata kama kitatimiza masharti. Ndani ya siku si chini ya
sabini (70), CCJ kilikamilisha masharti yote na kupeleka maombi ya
usajili wa kudumu. Msajili kupitia vyombo vya habari kwa mara nyingine
aliweka wazi nia yake ya kutotoa cheti cha usajili wa kudumu kwa CCJ.
Ndugu wananchi, kutokana na shinikizo toka kwa watanzania wenye
uchungu na nchi hii na wenye kutaka kuona mabadiliko, pia shinikizo
toka kwa ofisi za kibalozi zilizopo nchini, chama cha wanasheria tawi la
Arusha bila kusahau wanachama wa CCJ, hatimaye tarehe 3/5/2010
msajili kwa shingo upande aliamua kufanya uhakiki wa wanachama wa
CCJ kwa mikoa minne akianzia Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na
baadaye Mjini Magharibi.
Ndugu zangu nyote ni mashahidi wa hujuma tulizofanyiwa kiasi cha
kupelekea kusitishwa kwa zoezi zima la uhakiki. Na kwa kuwa nia ya
msajili ilikuwa ni kuichafua CCJ, alitangaza kuwa CCJ-Dar ina
wanachama 13 tu, na licha ya kuwa tulimwandikia barua ya kusitisha
zoezi la uhakiki bado aliendelea na Pwani kisha kutoa tamko kuwa
CCJ-Pwani haina hata ofisi licha ya wanachama. Baadaye akasema
Zanzibar tuna mwanachama mmoja, yote haya aliyafanya kwa
makusudi ili CCJ ionekane si kitu.
Msajili ameonyesha dharau na kejeli za wazi kwa watanzania,
tungependa kuwafahamisha Watanzania kwamba, wananchi wengi
sehemu mbalimbali za nchi yetu watu wa kila rika, dini mbalimbali
wakiwepo wasanii, wakulima, wafanyakazi pamoja na wastaafu
wamekikubali na kukipokea Chama Cha Jamii na wengi wamejiunga.
Tarakimu zilizopo ofisini, mpaka sasa kuna watanzania takriban 9500
wamejiunga na CCJ. Aidha wapo watanzania nje ya nchi kama vile
Marekani, Japani, Uingereza, Korea ya Kusini na Afrika Kusini
waliojiunga na CCJ.
Watanzania hawa waliojiunga na CCJ, aidha walifika wao wenyewe
ofisini au walishawishiwa na wananchi ambao walikuwa tayari
wamejiunga awali ukiondoa wanachama 102 walio jiunga kwenye
mkutano wa hadhara wa kuompokea Mh Mpendazoe uliofanyika pale
Mwembeyanga.
KUGOMBEA KUPITIA CHADEMA
Kwa mda mrefu kumekuwa na mazungummzo kati ya CCJ na
CHADEMA ya kuwa na ushirikiano na hususan katika uchaguzi mkuu
utakaofanyika oktoba 2010, hii inatokana na ukweli kuwa vyama hivi
vina itikadi na mwelekeo unaofanana. Ushirikiano huu ungeendelea
hata baada ya CCJ kupata usajili wa kudumu. Sasa, kwa kuwa muda
tuliobaki nao ni mchache kwa CCJ kupata usajili wa kudumu na
kufanya maandalizi ya kutosha kuelekea uchaguzi mkuu, hivyo basi,
tunatoa wito kwa wanachama wa CCJ wenye sifa na nia ya kugombea
nafasi za uongozi wa kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu ujao,
kugombea kupitia CHADEMA.
Ndugu zangu tunafanya hivi si kwa maslahi yetu au ya vyama vyetu,
isipokuwa tunafanya hivi kwa maslahi ya Taifa. Ndio maana tumeamua
kuachia nyadhifa zetu na kujiunga CHADEMA kama wanachama wa
kawaida. Hivyo basi, tunawaomba wanachama wote wa CCJ bila
kusahau wote wenye mapenzi mema na taifa hili, kuunga mkono
maamuzi haya na kuwachagua wote watakaosimamishwa na
CHADEMA.
Kwa kuwa CCJ tunaamini kuwa Umoja ni Nguvu ya pekee ya wananchi
katika kujenga Usawa na Uhuru na katika kuondoa Umaskini, Ujinga,
Maradhi na kupambana na Ufisadi, na kwa kuwa CHADEMA kinaamini
katika falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ambayo inalenga katika
kuwaamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwandaa Watanzania
wachukue hatua kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao, hivyo
basi tunatangaza rasmi kuwa Dickson Ngʼhily (Naibu Katibu Mkuu-
Bara), Richard Kiyabo (Mwenyekiti-Taifa) na Fred Mpendazoe
(Msemaji-Taifa) watagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu
ujao kwa tiketi ya CHADEMA mara baada ya kuchukua kadi zao za
uanachama wa CHADEMA.
Ndugu zangu nyote ni mashahidi na mnaelewa juu ya utajiri mkubwa
ambao Mwenyezi Mungu ameuweka ndani ya mipaka ya Tanzania.
Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kuwa wananchi wake ni maskini wa
kutupwa, hiki ni kitendawili ambacho jibu lake ni la kusikitisha kwani jibu
ni dhahiri, ni kutokana na uongozi usiojali wanyonge na usio na
uzalendo wa CCM.
Ni dhahiri kwamba watanzania wamechoshwa na hali hii na wanahitaji
mabadiliko ya kweli katika uongozi na uendeshaji wa nchi, hii ni
kutokana na ukweli kuwa CCM na serikali yake haviwezi kuleta
mabadiliko hayo na kamwe haitaweza. Ni dhahiri kwamba watanzania
wamechoka kuishi maisha yasiyo na matumaini, maisha yasiyo na
mwelekeo wa kesho, hivyo mabadiliko yanahitajika.
Na hili ndilo tumaini letu na tena hii ndiyo imani tunayoondoka nayo
kuwa sote kwa pamoja tunahitaji mabadiliko ya dhati na kwa
ushirikiano huu Tanzania yenye neema bila CCM inawezekana! Huu
sio wakati wa kupigishwa porojo na kupewa kanga na Tshirts, ni wakati
wa kusimama pamoja wanaume kwa wanawake, vijana na watoto
kudai mabadiliko katika sanduku la kupigia kura. Narudia tena
Tanzania yenye Neema Bila CCM inawezekana.
Mungu ibariki Tanzania
Asanteni kwa kunisikiliza.

Bado siamini kwamba habari ina ukweli wowote. Kama ni habari ya kweli, kwa maoni yangu naona huu ni usanii zaidi ya ule wa CCM!! Ina maana CCJ ilianzishwa wa ajili ya kutaka kuipiku CCM katika uchaguzi tu, na baada ya hapo iweje?
 
Kwa nini Mpendazoe asigombee Kishapu ambayo ameshwahi kuiwakilisha bungeni? Je huko hapakaliki tena kwa ndugu yetu huyu?
 
Hiki chama tulishasema toka mwanzo kimeanza kisanii....sasa hao vigogo waliokuwa nyuma yao wameyeyukia wapi? kukosa uchaguzi wa mwaka huu basi na chama ndio mwisho...kweli madaraka matamu.....ngoja tuwasikilize kwanza wale waliokuwa wameshupaa kukitetea
 
Sasa mbona walipoteza muda, pesa kutaka kusajili chama wakati chadema ilikuwepo tu...watu wengine wapuuzi tu kupoteza muda wa watu..ccj=chadema..what a joke?
 
Jamani mbavu zangu! jamaa kanichekesha na maendeleo kwa mtanzania. Attachment inaonekana vizuri ila hawa jamaa hawana lolote. wameonyesha udhaifu mkubwa wanatuhakikishiaje kama watakuwa real tukiwapa kura zetu kama wanachama wa chadema. Nuksi tumekaribisha.
 
Sasa mbona walipoteza muda, pesa kutaka kusajili chama wakati chadema ilikuwepo tu...watu wengine wapuuzi tu kupoteza muda wa watu..ccj=chadema..what a joke?
unataka kutuambia kuwa unafikiri ccj ndio hao hao chadema?
Sikubaliani na wewe hata kidogo!CHADEMA imekuwa kimbilio na walishauriwa wafanye hivyo.
 
Ooh politicians in action!
Tamko lao(CCJ?) linasema kuwa wana itikadi na mwelekeo unaofanana...Sasa,walianzisha chama cha nini.I mean kwanini hawakujiunga na CHADEMA tangu hapo mwanzo?Kisha mnakuja kuwalaumu wananchi eti kwanini hawachagui upinzani...Vinyonga kedekede!!!
 
Kwa kweli Chadema wananishangaza mimi nilidhani ni chama mbadala kama wanavyosema kama hata majimbo muhimu ya Dar es Salaam walikuwa hawana wanachama waliokuwa wametayaarishwa ili wagombee basi nimeshashusha mukari ambao nilidhani mwaka huu wangelikuwa nao katika kupambana na CCM, kazi ipo kwelikweli
 
Mnakumbuka Mzee Mtei?

Kwa busara zake, aliwapa ushauri hawa jamaa wajiunge chadema tu!!

sasa naona bado MMMKJ
 
Bado siamini kwamba habari ina ukweli wowote. Kama ni habari ya kweli, kwa maoni yangu naona huu ni usanii zaidi ya ule wa CCM!! Ina maana CCJ ilianzishwa wa ajili ya kutaka kuipiku CCM katika uchaguzi tu, na baada ya hapo iweje?

Kinachokufanya usiamini ni nini hasa?hizi ni habari za kweli Mkuu,kama uko Tz subiri taarifa za habari leo usiku na kwenye magazeti ya kesho..Pia pitia blog za wanahabari kama michuzi nadhani utapata data kamili.Habari ndio hiyo.Usiwe Tomaso.
 
GS, Habari hii naiona haijakaa sawasawa hakuna uhakika wowote kwamba uliyotubandikia ni ya kweli.

Hata hivyo, kama ni kweli hao waliotajwa wamejiunga na CHADEMA ili wawanie ubunge huo ni uamuzi wao na hauna uhusiano wowote na uamuzi wa wanachama wengine wa CCJ. Mie kama 'aliyekuwa mwanachama mtarajiwa' wa chama cha CCJ ambacho kwa sasa kimenyimwa usajili kwa mizengwe, sidhamirii kujiunga na CHADEMA ama chama chochote ambacho itikadi, sera na malengo yake hayajanigusa ipasavyo. Bado CHADEMA haijagusa moyo wangu ili nipate kuridhika kwamba chama hicho kina malengo thabiti ya kuhakikisha kuwepo kwa maendeleo yatakayolenga 'watu' - Watanzania wote. Mpaka sasa CHADEMA haijatuonyesha itakuwa na mikakati gani na itachukua hatua gani za makusudi kabisa kuhakikisha kwamba walioliibia taifa na kulihujumu wanachukuliwa hatua zinazostahili. Pia sijui CHADEMA kina mipango gani ya kuhakikisha hali za wanyonge wa Tanzania zinakuwa nzuri ndani ya miaka 5 ya uongozi wa CHADEMA, kwa sababu hilo linawezekana kabisa iwapo kuna mipango maalum. Hii blabla ya siasa za mrengo wa kati hazitoshi kututhibitishia chochote. Huenda nanyi kwa siasa zenu za mrengo wa kati mtazidi kukuza matabaka katika jamii.

CHADEMA Siasa zenu za majimbo zina kasoro kwa wale tunaoamini juu ya kuendeleza ujenzi wa umoja nchini. Juzijuzi nilimsikia kiongozi mwandamizi wa CHADEMA akizungumza na kutetea kwa nguvu zote wagombea wanaowania uongozi - ubunge, udiwani nk. waruhusiwe kupiga kampeni kwa lugha za kikabila badala ya Kiswahili. Hizi ndio sera zenu CHADEMA za maendeleo za kutaka turudi kwenye kuongea kimatumbi na ki-barbeig majukwaani?

Jingine lililonistua ni kumsikia kiongozi mmoja wa Taasisi moja ya Uchumi nchini (anaweza akawa mwanachama wa CHADEMA) akizungumzia habari ya kutaka kuwepo kwa "middle class" nchini na akawahamasisha Watanzania walio Marekani kuungana na walio nchini kuanzisha hiyo "middle class". Sasa huenda na ninyi CHADEMA siasa zenu za mrengo wa kati zina nia ya kutuletea na kujenga matabaka nchini kama ilivyo kwenye nchi za kibepari - wawepo Watanzania wa juu, wa kati na wa chini! CCJ isipokuwepo, ntaunga mkono chama kinachotetea kwa dhati kabisa usawa na haki sawa kwa kila Mtanzania katika mgawanyo wa keki ya Taifa.

Kwa maoni yangu, kuwa na wapinzani wengi bungeni ambao hawana itikadi maalum inayowaunganisha nako ni kupoteza wakati na nguvu. Mwisho wa siku nchi itaendeshwa kwa mfumo gani?

Mkuu,naomba nipingane nawe katika suala la kuhamasisha uwepo wa tabaka la kati.Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa katika dunia tunayoishi sasa hakuna uwezekano wa kuwa na jamii isiyo na matabaka (classless society).Tatizo sio uwepo wa matabaka bali mahusiano kati ya matabaka hayo (class relations).

Katika Tanzania yetu ya sasa ambapo civil society imeelemea zaidi upande wa tabaka tawala (na hapo tunaweka kando udhaifu wa civil society),tabaka la kati linaweza kuziba ombwe hilo iwapo litawajibika kikamilifu kupambana na ukandamizaji wa tabaka tawala kwa tabaka la walalahoi.Wengi wetu hapa JF tayari by default ni sehemu ya tabaka hilo la kati unalolihofia.Tatizo hadi sasa ni kuwa licha ya udogo na udhaifu wa tabaka hili linaloweza kuchochea mabadiliko ya kweli,wengi wa waliomo humo wanahangaika zaidi aidha kuishi kama tabaka tawala au wanatamani wawe member wa tabaka hilo la juu.Kinachopuuzwa ni ukweli kuwa tabaka hili linapaswa kuwa karibu zaidi na tabaka la chini (walalahoi) hasa kutokana na mahusiano yao ya kila siku (eg wale wenye vibarua lakini bado wanaishi na wazazi wao) na ukweli kwamba matabaka yote hayo mawilo ni wahanga wa matendo,mbinu na hila za tabaka tawala (rejea sakata la mishahara ya kima cha chini).

Ningeweza kuandika kwa kirefu ila muda na nafasi havitoshi.Ila ningependa kukutoa hofu kuwa uwepo wa tabaka la kati ni jambo hatari kwa jamii.Lililo hatari ni mahusiano kati ya matabaka na kwa tabaka la kati kuelemea upande wa tabaka tawala (kama ilivyo sasa kwa civil society) nakutelekeza wajibu.Pasipo kuziba ombwe lililopo kati ya tabaka tawala na walalahoi ni ndoto kwa mabadiliko yenye manufaa kwa walio wengi kujiri.
 
TAMKO LA VIONGOZI WA CHAMA CHA JAMII (CCJ) KUWATAKA
WANACHAMA WA CCJ WAGOMBEE NAFASI ZA KUCHAGULIWA
KATIKA UCHAGUZI MKUU UJAO KUPITIA CHADEMA
UTANGULIZI

Kwa kuwa CCJ tunaamini kuwa Umoja ni Nguvu ya pekee ya wananchi
katika kujenga Usawa na Uhuru na katika kuondoa Umaskini, Ujinga,
Maradhi na kupambana na Ufisadi, na kwa kuwa CHADEMA kinaamini
katika falsafa ya Nguvu na Mamlaka ya Umma ambayo inalenga katika
kuwaamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwandaa Watanzania
wachukue hatua kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao, hivyo
basi tunatangaza rasmi kuwa Dickson Ngʼhily (Naibu Katibu Mkuu-
Bara), Richard Kiyabo (Mwenyekiti-Taifa) na Fred Mpendazoe
(Msemaji-Taifa)
watagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi mkuu
ujao kwa tiketi ya CHADEMA mara baada ya kuchukua kadi zao za
uanachama wa CHADEMA.
Ndugu zangu nyote ni mashahidi na mnaelewa juu ya utajiri mkubwa
ambao Mwenyezi Mungu ameuweka ndani ya mipaka ya Tanzania.
Hata hivyo ni jambo la kusikitisha kuwa wananchi wake ni maskini wa
kutupwa, hiki ni kitendawili ambacho jibu lake ni la kusikitisha kwani jibu
ni dhahiri, ni kutokana na uongozi usiojali wanyonge na usio na
uzalendo wa CCM.
Ni dhahiri kwamba watanzania wamechoshwa na hali hii na wanahitaji
mabadiliko ya kweli katika uongozi na uendeshaji wa nchi, hii ni
kutokana na ukweli kuwa CCM na serikali yake haviwezi kuleta
mabadiliko hayo na kamwe haitaweza. Ni dhahiri kwamba watanzania
wamechoka kuishi maisha yasiyo na matumaini, maisha yasiyo na
mwelekeo wa kesho, hivyo mabadiliko yanahitajika.
Na hili ndilo tumaini letu na tena hii ndiyo imani tunayoondoka nayo
kuwa sote kwa pamoja tunahitaji mabadiliko ya dhati na kwa
ushirikiano huu Tanzania yenye neema bila CCM inawezekana! Huu
sio wakati wa kupigishwa porojo na kupewa kanga na Tshirts, ni wakati
wa kusimama pamoja wanaume kwa wanawake, vijana na watoto
kudai mabadiliko katika sanduku la kupigia kura. Narudia tena
Tanzania yenye Neema Bila CCM inawezekana.
Mungu ibariki Tanzania
Asanteni kwa kunisikiliza.

Huyu aliyesema asanteni kwa kunisikiliza ni Fredy Mpendazoe (msemaji - Taifa) au nani?
 
CCJ wenyewe ni failure ..kama chadema walivyo failure..

Mkuu habari za siku nyingi.Naona habari hii imekuuma,eeh!!!unatakiwa kuwa na ukomavu wa kisiasa..Acha kulia lia kama ilivyo kawaida yako.Mwanaume mzima kila siku kulia tu.Lol!
 
Back
Top Bottom