Viongozi wa CCJ Wajiunga Rasmi na CHADEMA

Kwa kweli Chadema wananishangaza mimi nilidhani ni chama mbadala kama wanavyosema kama hata majimbo muhimu ya Dar es Salaam walikuwa hawana wanachama waliokuwa wametayaarishwa ili wagombee basi nimeshashusha mukari ambao nilidhani mwaka huu wangelikuwa nao katika kupambana na CCM, kazi ipo kwelikweli

Aliyekuambia katika majimbo hayo hakuna wagombea wengine nani?katika majimbo hayo tajwa ya Dar yaani Temeke na Segerea kote kuna wagombea wengine tena zaidi ya mmoja.Kura za maoni ndio zitaamua nani ni nani..
 
Hivi ni vijimambo tu mambo makubwa yanakuja hamtaamini macho na masikio yenu midomo itabaki wazi.
 
Kwa nini Mpendazoe asigombee Kishapu ambayo ameshwahi kuiwakilisha bungeni? Je huko hapakaliki tena kwa ndugu yetu huyu?

Na mimi hilo linanishangaza sana, Jimbo la segerea kuna Rachel Mashishanga ameshatangaza nia ya kugombea na ninaamini kuwa angemuangusha yule mcheza Taarabu aliyepo sasa. Huyu mpenda zoe ana jimbo alilogombea sasa inakuwaje analiacha na kuja kutaka jimbo lingine. Bila kutueleza at least atahakikisha lile jimbo nalo linakwenda upinzani itakuwa ngumu sana kumwelewa huyu mtu. Afadhali angwekwenda ukonga na kumtoa yule Binagi ambaye ndiye anayetoa siri nyingi za chadema kwa CCM na inaonekana anataka kuwauzia jimbo la ukonga bei rahisi.

So far namsupport Rachel kubeba tiketi ya Segerea na atashinda.
 
Aliyekuambia katika majimbo hayo hakuna wagombea wengine nani?katika majimbo hayo tajwa ya Dar yaani Temeke na Segerea kote kuna wagombea wengine tena zaidi ya mmoja.Kura za maoni ndio zitaamua nani ni nani..

GS: achana na hawa wanaodhani kuwa Chadema hakuna utaratibu na watu wakitangaza nia basi ndiyo wamekuwa wagombea. Utashangaa kuona watu wa aina hii wakishabikia mambo bila ya kujua athari zake wengine watajua pale watakaporudwi tu!
 
Hiyo ndio maana ya demokrasia. Ukibaniwa huku tazama pa kutokea pengine tuna vyama vingi mno ingawa havina nguvu
 
Vyama vya siasa Tanzania ni sarakasi tu......hivi hata Kama msajili kawazulia asingesema Zanzibar mjini magharibi kuna mwanachama mmoja tu. Nalazimika kuamini kuwa ccj hawakuwa na wanachama wa kutosha.

Kheri tu walivyojiengua kwenye uchaguzi manake wanajua fika kuwa hawatapitishwa ktk kura za maoni za chadema.

Ccj turned out to be a big joke! Only in tanzania
 
CCJ wenyewe ni failure ..kama chadema walivyo failure..

Kama unafikiria kuwa CHADEMA ni failure, rejea yaliyotokea Tarime, Busanda na Biharamulo, watanzania wameamka sasa, na ccm wategemee kushindwa kukuu hasa kwe ubunge
 
Mkuu,naomba nipingane nawe katika suala la kuhamasisha uwepo wa tabaka la kati.Kwanza ni muhimu kufahamu kuwa katika dunia tunayoishi sasa hakuna uwezekano wa kuwa na jamii isiyo na matabaka (classless society).Tatizo sio uwepo wa matabaka bali mahusiano kati ya matabaka hayo (class relations).

Katika Tanzania yetu ya sasa ambapo civil society imeelemea zaidi upande wa tabaka tawala (na hapo tunaweka kando udhaifu wa civil society),tabaka la kati linaweza kuziba ombwe hilo iwapo litawajibika kikamilifu kupambana na ukandamizaji wa tabaka tawala kwa tabaka la walalahoi.Wengi wetu hapa JF tayari by default ni sehemu ya tabaka hilo la kati unalolihofia.Tatizo hadi sasa ni kuwa licha ya udogo na udhaifu wa tabaka hili linaloweza kuchochea mabadiliko ya kweli,wengi wa waliomo humo wanahangaika zaidi aidha kuishi kama tabaka tawala au wanatamani wawe member wa tabaka hilo la juu.Kinachopuuzwa ni ukweli kuwa tabaka hili linapaswa kuwa karibu zaidi na tabaka la chini (walalahoi) hasa kutokana na mahusiano yao ya kila siku (eg wale wenye vibarua lakini bado wanaishi na wazazi wao) na ukweli kwamba matabaka yote hayo mawilo ni wahanga wa matendo,mbinu na hila za tabaka tawala (rejea sakata la mishahara ya kima cha chini).

Ningeweza kuandika kwa kirefu ila muda na nafasi havitoshi.Ila ningependa kukutoa hofu kuwa uwepo wa tabaka la kati ni jambo hatari kwa jamii.Lililo hatari ni mahusiano kati ya matabaka na kwa tabaka la kati kuelemea upande wa tabaka tawala (kama ilivyo sasa kwa civil society) nakutelekeza wajibu.Pasipo kuziba ombwe lililopo kati ya tabaka tawala na walalahoi ni ndoto kwa mabadiliko yenye manufaa kwa walio wengi kujiri.

Asante Mkuu, lakini huoni kwamba katika mazingira ya Tanzania hivi sasa tabaka la kati kujaribu kusaidia tabaka la chini ni ndoto ya mchana. Wewe mwenyewe umebainisha kwamba waliomo kwenye tabaka la kati wanahangaika zaidi kuishi kama tabaka la juu au wanatamani wame member wa tabaka hilo la juu. Na unakiri kwamba tabaka hili linapuuza ukweli kuwa tabaka hili linapaswa kuwa karibu zaidi na tabaka la walalahoi. Nini kitaweza kulizindua tabaka hili la kati lenye uchu wa kutaka kufika juu lianze kujali na kuwa karibu zaidi na tabaka la chini? Itoshe kusema kwamba inabidi tufike mahali tuelewe na tukiri kwamba matabaka haya yapo, na ni ya hatari sana kwa mustakabali wa nchi na wananchi wake hasa wale wa tabaka la chini ambao kwa jinsi hali ilivyo hawana matumaini yoyote ya kuibukia kwenye tabaka lolote lile. Hapa sizungumzii wale unaosema wana mahusiano ya wazazi (tabaka la chini) na watoto waliokwishaingia kwenye tabaka la kati. Tabaka hili ni lile la chini kabisa la wale Watanzania wenzetu walio vijijini ambao wazazi ama watoto leo hii ukiwapa sh. 500 wanakuona wewe ni 'malaika' uliyeshuka toka mbinguni!

Jukumu letu ni kuwapigia mbiu watawala wetu na sisi wenyewe kujiaminisha kwamba kwamba hatuhitaji matabaka hata yawe yanakuja kwa sura gani nzuri tunayoweza kuielezea. Tusijipe moyo kwamba kwa kuwa dunia yote ina matabaka basi na sisi inabidi tuwe nayo. Tanzania bila matabaka yanayozidi kukua kama ilivyo sasa inawezekana.

Tulipopata Uhuru kulikuwa na matabaka kama hayo ambayo hata sehemu zingine za dunia yalikuwepo. Lakini, ilifanyika kazi na hatua za dhati na za makusudi kabisa kuchukuliwa na watawala wakafanikiwa kuondosha matabaka hayo hadi ikafika mahali kukawa hakuna tofauti yoyote ya maana kimaslahi na kimaisha kati ya kiongozi (rais, waziri, makatibu wakuu n.k.) na wananchi wengine wa kawaida. Isitoshe uongozi ulijitahidi kuchukua hatua za dhati na za wazi kabisa za kuboresha maisha ya tabaka la chini. Kinachojitokeza sasa kwenye matabaka ni ulafi na tamaa ya maisha bora bila kujali uhalisia wa maisha ya Watanzania wengine wenye hali duni ambao nao wanastahili maisha bora.

Kwa nini Watanzania tupende wakati wote kujifananisha na watu wengine, tunaweza kuwa "an exception to the rule" na kuishangaza Afrika na dunia vilevile!
 
Duh! Mwaka huu wa uchaguzi si mchezo ati!

Nimewaona hao makada wa zamani wa CCJ wakikabidhiwa kadi na Freeman katika ofisi za Chadema Kinondoni. Ilitoka kwenye TBC1 news headlines saa kumi hii kwa saa za kibongo.

Chadema, you have my support.
 
Hivi ni vijimambo tu mambo makubwa yanakuja hamtaamini macho na masikio yenu midomo itabaki wazi.

Mkuu Ltn,
Nahisis hivyo, there should be a big heat coming!!!
TV=Tusubiri Vitu.:A S-eek:
 
Mkuu GS,

Sikujua na wewe umetanga za nia!! Signature yako...
(Mgombea Ubunge Mtarajiwa(CHADEMA)-Niunge Mkono)
 
I bet, GS kawaingiza mjini nyie wote!


6.JPG
 
Haya haya!.. dakika za nyongeza kipenga kimeshalia vijana uwanjani...

Bado tunataka kuona hao wasomi ma Profesa wanaopinga utawala wa JK nao wakijiunga. Wafanyakazi wa serikali, NCCR,TLP kasoro Mrema na vyama vingine vyoote jiungeni pamoja ili kila kiti cha kugombea nchi nzima kipate mpinzani. Upinzani wanaposhindwa kuweka mgombea mahala popote nchini huo ni ushindi wa bure kwa CCM na ndiyo makosa yaliyofanyika ktk chaguzi zilizopita haswa huko vijijini..
Safari hii isitokee hivyo....kila jimbo na kila wadhifa upate mshindani.
 
Jamani mbavu zangu! jamaa kanichekesha na maendeleo kwa mtanzania. Attachment inaonekana vizuri ila hawa jamaa hawana lolote. wameonyesha udhaifu mkubwa wanatuhakikishiaje kama watakuwa real tukiwapa kura zetu kama wanachama wa chadema. Nuksi tumekaribisha.

Jamani,hapa ndugu yangu unakosea kabisa.Hivi hatufahamu siasa ni dynamics?si kweli kwamba tumekaribisha nuksi.Wana haki zote na wapeni kura zenu kama watapita kwenye kura za maoni.Siasa ndio ilivyo..Ni wapambanaji wenzetu hawa,tuwakubali.
 
We have to be very careful/watchful/sceptical.
Isijekuwa a super calculated move by CCM to kill CHADEMA.
I pray to GOD is not.
 
Back
Top Bottom