Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

Karibuni mahenge. SIto migomba tu hata mipalachichi inakubali. Mtimbira kwa migomba pako poa sana. I can give u people ABC. TIWASILIANE. NITAWASAIDIA.

Mkuu, Karl peters wangu hajarudi toka Chita, sasa nisaidie yafuatayo.

Bei kwa eka moja ya shamba plain,
Manpower ipo au ni ya kuagiza,
Mazao yanamea vizuri hapo,
Umbali wa jumla in km, toka Dar mpaka hapo, au toka mikumi mpaka hapo,
Je Parachichi miche ipo hapo au ni ya kuagiza,
 
Mkuu, Karl peters wangu hajarudi toka Chita, sasa nisaidie yafuatayo.

Bei kwa eka moja ya shamba plain,
Manpower ipo au ni ya kuagiza,
Mazao yanamea vizuri hapo,
Umbali wa jumla in km, toka Dar mpaka hapo, au toka mikumi mpaka hapo,
Je Parachichi miche ipo hapo au ni ya kuagiza,
Nina ufahamu mzuri na wilaya ya Ulanga kule mahenge/ mtimbira. Huko maeneo ni mazuri sana.
 
are haina specific bei. Mimi nilinnunua heka 10 mwaka 2009 kwa shilingi laki 3kwa heka zote. Ni eneo Zuri kwa migomba. So Kama mko tayari nitawaulizia. If ua serious.
mkuu kama zako hizo niandae ngapi kwa sasa. ni ya kijiji au ya watu. natanguliza shukrani.
 
Wana jamvi hivi karibuni nilikuwa bukoba kikazi na nimeshuhudia migomba ime nyauka na kusababisha ndugu zetu wahaya kubadili mfumo wao wa maisha yaani kuanza kula ugali na wali, tofauti na zamani walipo kuwa wanategemea ndizi kama chakula chao kikuu
 

Attachments

  • 1391013646866.jpg
    1391013646866.jpg
    67.9 KB · Views: 257
Kuna mkungu unaotokana na Mradi huu toka shamba moja la mkulima huko Ngara umefikia kilo 230! Kuna taarifa huenda ukavunja rekodi katika vitabu vya Guieness. Mradi umezalisha takriban aina kama tatu za mbegu ambazo zinafaa kwa biashara kuanzia kula hadi kutengeneza mvinyo! Kwa maelezo zaidi, fanya mawasiliano na maafisa kilimo wilaya za Mkoa wa Kagera na wilaya ya Kibondo mkoa wa Kigoma ambako Mradi huu umetekelezwa.

Dah mkuu huo mkungu ni balaaa, kilo 230??

Nafikiri hao jamaa wana mbegu za hybrid pia zinazo-fit mazingira yetu haya ya ukanda wa pwani
 
Ndugu wana JF nimevutiwa na mada mbalimbali za kilimo, ila naomba yeyoye anayefahamu ABC's za kilimo cha migomba anifahamishe kwani nina nia ya kushiriki katika kilimo hiki.
 
wakuu nimepata ekari tatu nimeanza kuzipanda kidogokidogo. mmpaka sasa nimepanda miche 200 niliyopanda mwezi wa february. Ila napanga mpaka mwezi wa saba niwe nimemaliza. Nimefanya utafiti na kwa kauzoefu nilikopata nimejifunza yafuatayo.
Watafiti wa Uganda walifanya utafiti kuhusu spacing ya migomba. Kuna waliyoweka 3mx3m na kupanda migomba 400 kwa ekari. Mikungu iliyozaliwa ilikuwa na kilo 14. 2.5x2.5 walipanda migomba 640 kwa ekari na ilikuwa na mikungu ya kilo 12.5 hadi 13. Kuna mingine ilikuwa 2x2 na walipanda migomba 1000 kwa ekari na mikungu yake ilikuwa kilo 11. Kutokana na hivyo mi napanda 2.5x2, ambayo itatoa migomba 800 kwa ekari. Huu ulikuwa kwa ndizi Uganda ila mimi napanda mzuzu.
Shimo linakuwa kipenyo cha 60cm na urefu wa 60cm. au urefu wa hadi gotini kwa mtu mzima. Kila shimo wanachimbia sh 300 hadi 500 kulingana na ugumu. Maximum 400,000 kwa ekari.
Kila mche nanunua tsh 300 na kubeba hadi shambani ni tsh 200. Jumla itakuwa 400,000 kwa ekari.
Napandia debe moja la samadikila shimo. Nimeinunua 20,000 na kila debe wanabebea tsh 400. Jumla ni 340,000 kwa ekari. Kupanda ni 100 sawa na 80,000 kwa ekari.
Jumla ya kukamilisha eka itakuwa 1, 220,000. Gharama za palizi na zingine ntakuwa nawaupdate.
 
Nilikuwa na wazo humu waungwana...mtu anapochangia kama anajua na soko la mazao popote pia ni vizuri kusema,maana nimeona watu wengi wanachangia kuhusu kulima ila kwenye swala la masoko tatizo.
Wengine humu tunapenda kununua na kuuza tu.

Ni wazo tu lakini.......
 
Sa hivi njoo huku kirua uone mkungu wa ndizi mshale ni sh.600, namaanisha shilingi Mia sita ya kitanzania afu hakuna mtu anakuja kununua mkungu wala nini, mpk imefika hatua ndizi zinakatwa katwa anapewa ng'ombe, so msidhani kutajirikia kwenye ndizi ni rahisi kama mnavodhani
 
Sa hivi njoo huku kirua uone mkungu wa ndizi mshale ni sh.600, namaanisha shilingi Mia sita ya kitanzania afu hakuna mtu anakuja kununua mkungu wala nini, mpk imefika hatua ndizi zinakatwa katwa anapewa ng'ombe, so msidhani kutajirikia kwenye ndizi ni rahisi kama mnavodhani

Kweli kilimo wakati mwingine hakina muamana,ila kuna kamsemo kamoja kanasema "arms at higher" haka ndio kanakotupa ujasiri wa kutaka kilimo cha ndizi.
 
Sa hivi njoo huku kirua uone mkungu wa ndizi mshale ni sh.600, namaanisha shilingi Mia sita ya kitanzania afu hakuna mtu anakuja kununua mkungu wala nini, mpk imefika hatua ndizi zinakatwa katwa anapewa ng'ombe, so msidhani kutajirikia kwenye ndizi ni rahisi kama mnavodhani
rungwe ndizi mzuzu inajumliwa kwa 2000-5000. ikifika dar inauzwa 12,000-18,000. zinafikaga hadi 30,000. uliza hizo mshale ikipanda sana inafika tsh ngapi? liza pia dar ni tsh ngapi?
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom