Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

Kama huamin Mkuu,njoo kirua mtu ana ekari 5 afu mambo ni Yale yale, anyway jambo unalofanya ni jema sana mungu akuongoze kwenye mafanikio
sijabisha. bei inategemea ndizi na ndizi. jiulize kwanini bei ipo hivyo, labda wamefunga mpaka?. je bei ikiwa juu hufika ngapi? je dar ni tsh ngapi?. inatakiwa utafiti sababu kabla ya kuja na conclusion.

ngoja nikupe mfano. Brazil inazalisha 33% ya kahawa duniani. kuna miaka barafu huanguka kwenye mashamba ya kusini na kusababisha uzalishajji mdogo na bei kupanda sana. miaka ambayo uzalishaji ni mkubwa bei huporomoka. siamini mkungu wa ndizi za mtori huwa 600 miaka yote. mwezi uliopita nilinunua mzuzu shambani tukuyu kwa 5000.
 
sijabisha. bei inategemea ndizi na ndizi. jiulize kwanini bei ipo hivyo, labda wamefunga mpaka?. je bei ikiwa juu hufika ngapi? je dar ni tsh ngapi?. inatakiwa utafiti sababu kabla ya kuja na conclusion.

ngoja nikupe mfano. Brazil inazalisha 33% ya kahawa duniani. kuna miaka barafu huanguka kwenye mashamba ya kusini na kusababisha uzalishajji mdogo na bei kupanda sana. miaka ambayo uzalishaji ni mkubwa bei huporomoka. siamini mkungu wa ndizi za mtori huwa 600 miaka yote. mwezi uliopita nilinunua mzuzu shambani tukuyu kwa 5000.

Mkuu unaongelea tukuyu labda huko ndizi ni adimu, huku kuna kipindi inafika mtu anatoa elfu 2 anaondoka na mikungu 5. All the best bro
 
Sabayi na Malila msipuuze post ya Alex Mponela, unaweza kuta mkapata ardhi nzuri na ya bwelele huko. mkuu Malila ni vyema kwenda kujionea mwenyewe kama ulivyosema utaenda chita.kuna jamaa yangu aliwahi niambia eti huko malinyi ardhi ni 5,000 kwa ekari!!. watu wengi wakikwambia eti ardhi ni ghali sana mara nyingi huangalia ile ya ''mjini'' au karibu na barabara, lakini ukiingia hata km 5 au 10 ndani utakuta bei cheap ajabu.
hii kitu bado iko valid? namaanisha niko interested sana kupata arhi kama eka 10 na kuendelea mkoa wa morogoro vijijini, naweza pata kwa bei kama hiyo??
 
attachment.php
 

Attachments

  • 1448814946259.jpg
    1448814946259.jpg
    12.5 KB · Views: 507
attachment.php
attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • 1448814946988.jpg
    1448814946988.jpg
    14.3 KB · Views: 465
  • 1448814947810.jpg
    1448814947810.jpg
    11.9 KB · Views: 438
  • 1448814949703.jpg
    1448814949703.jpg
    11.6 KB · Views: 434
Asanate kwa update: Hizi Gharama ni Mkoa Gani?
Natafuta mbegu za Ndizi Tamu,nimeuliza nimeambiwa ndizi Tamu zinatoka Moshi/Kilimanjaro
Je zinaweza kustawi ukanda wa Pwani Dar/Mkuranga?
mi napenda kuangalia ukulima wa mazao mbalimbali. kuhusu ndizi nikapata habari zilizonipendeza nikasema nishirikiane nanyi.

ukipanda ndizi leo itachukua kati ya miezi kumi hadi kumi na mbili kuzaa mkungu. pia itategemea hali ya maji maana ndizi zinahitaji maji mengi sana. ukishuvuna mkungu huo mmea unaukata na itachukua miezi mingine kama hiyo kwa machipukizi ya ndizi kuvunwa. kuvuna huku kunaweza endelea kwa miaka 25 hapo ndio mtu unaweza kutoa mimea yote na kuanza upya. twende kwenye uzaaji.

kwa wakulima wa kawaida ekari ya ndizi huzaa tani 7 za ndizi ambazo ni sawa na kg 7000. kwenye vituo vya utafiti ilionekana ekari moja inaweza kuzalisha mpaka tani 24 yaani kg 24000. mkungu mmoja wa ndizi kwa wastani unauzito wa kg 12. kwa hiyo ukipata kilo 7000 utakuwa umepata mikungu 583 ya ndizi. kwa dar es salaam mkungu mmoja wa ndizi ni kati ya tsh 12000-18000 ikitegemea na kipindi.basi kwa mikungu 583 utapata tsh millioni 7 hadi milllioni 10!!. je ukiwa na ekari 10, 20 au 30 utakuwa wapi?. mambo ya kuzingatia nikuhakikisha migomba yako inapata maji ya kutosha na unaikinga na magonjwa na panya wala mizizi. pia ni vizuri ukalima eneo kubwa kidogo au mkakubaliana na majirani ili kuepuka kusafirisha mzigo kidogokidogo kitu kinachoweza kukupa hasara. wenye experiance na nyongeza naombeni muongezee. Malila, Chasha, Sabayi, Kubota etc

update 26/3/2015

wakuu nimepata ekari tatu nimeanza kuzipanda kidogokidogo. mmpaka sasa nimepanda miche 200 niliyopanda mwezi wa february. Ila napanga mpaka mwezi wa saba niwe nimemaliza. Nimefanya utafiti na kwa kauzoefu nilikopata nimejifunza yafuatayo.

Watafiti wa Uganda walifanya utafiti kuhusu spacing ya migomba. Kuna waliyoweka 3mx3m na kupanda migomba 400 kwa ekari. Mikungu iliyozaliwa ilikuwa na kilo 14. 2.5x2.5 walipanda migomba 640 kwa ekari na ilikuwa na mikungu ya kilo 12.5 hadi 13. Kuna mingine ilikuwa 2x2 na walipanda migomba 1000 kwa ekari na mikungu yake ilikuwa kilo 11.

Kutokana na hivyo mi napanda 2.5x2, ambayo itatoa migomba 800 kwa ekari. Huu ulikuwa utafiti wa ndizi Uganda ila mimi napanda mzuzu.

Shimo linakuwa kipenyo cha 60cm na urefu wa 60cm. au urefu wa hadi gotini kwa mtu mzima. Kila shimo wanachimbia sh 300 hadi 500 kulingana na ugumu. Maximum 400,000 kwa ekari.

Kila mche nanunua tsh 300 na kubeba hadi shambani ni tsh 200. Jumla itakuwa 400,000 kwa ekari.

Napandia debe moja la samadikila shimo. Nimeinunua 20,000 na kila debe wanabebea tsh 400. Jumla ni 340,000 kwa ekari. Kupanda ni 100 sawa na 80,000 kwa ekari.

Jumla ya kukamilisha eka itakuwa 1, 220,000. Gharama za palizi na zingine ntakuwa nawaupdate.
 
haaa haaa haaaa

dah ... jkt kiboko

nilienda kuiba zabibu nyeupe pale kwenye shamba la zabibu makutupora jkt ... afande akatokea nilijidumbukiza kwenye shimo refu kutoka ikawa ishu, ikabidi nivue kombati nilichane chane ili kutengeneza kamba ya kupandia

Nyie jamaa mnechekesha sana, nakumbuka nilivyokuwa Jkt oljoro tulikuwa na afande mmoja wa jikoni, huyo afande ukiuunguza mboga ama ukipika ugali mbichi lazima uote moto. Yaani unasogezwa karibu na moto mpaka unachanganyikiwa, alikuwa anasema kwa ukali " kurute ota moto, kuruta ota moto" Ukifanikiwa kutoka hapo ni jasho na umeipata fresh, si unajua tena combat inavyojua kupata moto.
 
Red Giant hongera sana shamba limependeza, zaidi ya mbolea ya samadi ni mbolea gani nyingine inayofaa kwa migomba?
 
Last edited by a moderator:
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom