Fursa za kilimo na mustakabali wa Tanzania

Political Jurist

Senior Member
Sep 6, 2021
120
104
Na Amon Nguma.

Dunia kwa nyakati zote imekuwa ikikubwa na changamoto mbalimbali za asili na zitokanazo na shughuli za kibinadamu lakini Mtu au Taifa lililoweza,linaloweza na litakaloweza kuona fursa katikati ya changamoto au kuitumia changamoto kama fursa litakuwa limejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kustawi na kusaidia wengine .

Kwa sasa Dunia inakumbwa na upungufu na uhitaji mkubwa wa Chakula na hii ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa au tabia nchi, vita na migogoro ya kisiasa ambayo imeathiri uzalishaji wa Chakula ,kwa Taifa ambalo lipo katika nafasi nzuri linaweza kufanya vizuri kwa kuzalisha nafaka ,matunda na mbogamboga pamoja na mazao mengine ambayo yanahitajika kwa wingi duniani.

Tanzania ina eneo la Kilomita za Mraba 947,300 sawa na Hekta Milioni 86,610,000 ambapo Hekta Milioni 44 ni eneo la kilimo (Arable Land) na kati ya hizo Hekta Milioni 29.4 zinafaa kwa umwagiliaji, ni asilimia 33 tu ya eneo la Kilimo iliyotumika, lakini pia nchi yetu ina eneo kubwa la misitu takribani Hekta Milioni 40 .Tanzania inazungukwa na maziwa makuu pamoja na Bahari ya Hindi huku ikiwa na Eneo la Maji (Inland Surface Water ) kwa zaidi ya asilimia 6 ya eneo lote la Tanzania.

Kama ambavyo amekuwa akisisitiza Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Tanzania inayo uwezo wa kujilisha kwa utoshelezi na kuwa kimbilio kwa Afrika na Dunia, lakini pia kuwa Kinara katika uzalishaji wa mazao Duniani kama ambavyo Mataifa mengine yamefanya na yanaendelea kufanya na nitatoa mfano kwa uchache.

Nchi ya Morroco ina ukubwa wa Kilomita za Mraba 710,850 eneo lake la Kilimo ni Hekta Milioni 8.5 eneo ambalo linafaa kwa umwagiliaji ni Hekta Milioni 1.35. Morroco imekuwa muuzaji mkubwa wa zao la Nyanya Duniani akiingia kwenye tatu bora ,kwa mwaka 2022 nchi hii iliuza tani 740,000 na kuingiza mapato ya Dola Bilioni 1.1 ambayo ni karibia Tsh.Trilioni 3 mafanikio haya yametokana na mipango mizuri na sera za Kilimo zinazotekelezeka (Proper Planning & Practical Agricultural Policies) ambapo serikali iliweka miundombinu rafiki kwa kilimo kikubwa cha Nyanya.

Aidha kiwango hiki cha Dola Bilioni 1.1 ni kikubwa zaidi kuliko kiwango cha mauzo ya mazao yetu makubwa ya Tumbaku, Pamba na Chai katika kipindi kama hicho.

Nchi ya Mexico inaongoza duniani kwa uuzaji wa Parachichi nje ya Nchi ambapo kwa mwaka 2022 Mexico ilisafirisha na kuuza Parachichi yenye thamani ya Dola Bilioni 3.5 ambayo ni sawa na Tsh.Trilioni 9 kwa zao moja pekee kiwango ambacho hata tukichanganya mauzo yetu makubwa (BIG 5) tunaweza tusifikie, hii ni dhahiri kuwa matunda yana faida kubwa na yanahitajika duniani .Kwa Afrika ni Morocco,Kenya na Afrika Kusini ndio zipo nafasi ya 8,9& 10 mtawalia huku Tanzania haipo hata kwenye 15 bora licha ya kuwa na Ardhi kubwa na maji ya kutosha katika Mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe na sehemu nyingi zinazofaa zao la Parachichi.

Nchi ya Indonesia inaongoza duniani kwa uzalishaji na uuzaji nje ya Nchi (Export) wa zao la Mchikichi/Mawese (Palm Oil) kwa mwaka 2022 Indonesia iliuza Mafuta ya Mawese yenye thamani ya Dola Bilioni 28.7 ambayo ni sawa Tsh.Trilioni 72 hii ni karibu bajeti ya Tanzania kwa miaka 2.

Kwa Tanzania mikoa inakolimwa Mchikichi(palm oil) ni Kigoma, Mbeya na Pwani lakini Mikoa ya Tabora, Katavi, Morogoro,Tanga, Lindi, Mtwara na Kagera inafaa kwa zao la Mchikichi.Tofauti na Alizeti zao la Chikichi likikua linaihakikishia Nchi mavuno ya mafuta ya uhakika na kudumu bila kuathiriwa na hali ya hewa kama mvua na hivyo kupelekea uhakika wa mafuta ya kupikia.

Kwa mifano hii michache ya mazao matatu tajwa hapo juu ni kweli pasipo shaka kuwa kuna fursa kubwa katika Kilimo lakini pia katika upande wa ufugaji na uvuvi, kwa sasa hakuna mazao ya Chakula wala ya Biashara bali mazao yote yanaweza zalishwa na kuwa ya Kibiashara, leo hii zao la Mbogamboga kama nyanya linaweza tengeneza faida kubwa kuliko mazao yaliyokuwa yametengwa au kutegemewa kama mazao makuu ya kibiashara .

Tanzania kwa namna ilivyo na ardhi kubwa na yenye rutuba, maji ya kutosha na mazingira rafiki kwa mazao mbalimbali tunaweza kuzalisha mazao na kuwa kati ya Mataifa yanaoongoza kwa uuzaji wa mazao Duniani na hivyo kutengeneza ajira, faida kubwa na chanzo cha mapato ya Kodi kwa Taifa kwa ajili ya utoaji wa huduma sasa na siku za usoni.

Nini kifanyike ili Tanzania kupiga hatua kubwa katika Kilimo na uzalishaji ??

1). Serikali igawe maeneo kwa Wananchi hususani Vijana. Moja ya tatizo na kikwazo kikubwa hususani kwa vijana ni umiliki wa ardhi hivyo serikali itoe maeneo, mbegu na uwezeshaji kwa vijana kwa ajili ya upandaji wa mazao hususan ya miti kama parachichi kwa mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya lakini Chikichi kwa Mikoa ya Kigoma na mengineyo kwa kufanya hivyo Tanzania itatengeneza mabilionea wa kipindi kijacho ,ajira kwa vijana, mapato ya uhakika na wakati huo mazingira yakiwa yametunzwa.

2). Tubadilishe baadhi ya mapori ya asili kuwa mapori ya faida. Lengo kubwa la Serikali kutenga mapori ni kutunza mazingira sasa mapori hayo yanaweza kusafishwa na kuotesha miti kama Mchikichi, parachichi, embe n.k kwamba tutakuwa na pori la maparachichi au maembe ama chikichi na wakati tunatunza mazingira lakini pia tutavuna mazao kama mafuta na matunda na kutengeneza kipato.Kwa mfano nchini Indonesia eneo lililo na Miti ya Mchikichi (Palm Oil Plantations) inakadiriwa kuwa Hekta Milioni 13 sawa na Ekari Milioni 30 huu ni msitu wenye mazao ya manufaa. Tukiacha pori la asili mtu akikosa kipato ataona pori ndio mkombozi wake kwa kukata mkaa au kuni na kuuza hivyo uharibifu wa mazingira na pia idadi ya watu inakuwa ni vyema tukaanza kubadilisha (replace) aina ya misitu tuliyonayo kwa baadhi ya maeneo.

3). Uwezeshaji wa Mitaji. Baada ya Vijana kupata maeneo Serikali, Taasisi za Fedha na sekta binafsi kwa ujumla kuwekeza katika kuwawezesha vijana mbegu na vifaa ili kuanza kuzalisha na hivyo kutengeneza Mabilionea wa kesho wa Kitanzania.

4). Maafisa Kilimo kufikishwa katika maeneo ya uzalishaji. Haihitaji kila mkulima kujua aina ya udongo au magongwa ya mazao hayo atajifunza kwa uzoefu kutokana na utaalamu au ushauri atakaoupata kutoka kwa maafisa kilimo/mifugo kwani hawa ndio wataalamu wa Kilimo .

5). Kuanzishwe kanda maalum za uzalishaji mazao (Special Production Zone). Hii itasaidia katika utafiti, huduma na masoko ya mazao, kwa mfano Singida inakuwa ni kanda maalum kwa ajili ya uzalishaji wa Kuku na Mayai, Dodoma uzalishaji wa Nyanya n.k .Hii itasaidia upelekaji wa rasilimali watu, fedha na vifaa lakini pia kurahisisha uchukuaji wa mazao kwenda kwenye masoko.

Mengine kama ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji na tafiti za Kilimo yamefanywa vizuri na Serikali ya Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan na mapinduzi ya kibajeti aliyofanya ni udhihirisho kuwa ameona fursa iliyopo katika Kilimo, ni wajibu wa Wizara na wadau kushirikiana na kutoa michango itakayoboresha zaidi sekta ya uzalishaji na kuleta matokeo chanya kwa Taifa letu.

Tanzania inayo fursa kubwa sana katika sekta ya Kilimo na nikutokana na baraka za kijografia ambazo Tanzania imejaaliwa na Mungu.Ni wakati wa kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa katika uzalishaji na kujenga uchumi imara wa sasa ni siku za usoni .Sehemu ambayo Watanzania tunapaswa kujitafuta na kujipata ni kwenye sekta ya Kilimo.

Twendeni shambani kwa nguvu zetu zote, kilimo sio unyonge wala laana ,Kilimo ni baraka na utajiri .

Amon Nguma
0620615659
0788613648 .
 
Sorry sijaenda deep sana lakini labda tuanzie hapa.... Masoko yanasemaje ? Sababu sidhani kama Tatizo ni Production per se.

Dunia ya sasa mtu mmoja anaweza kulisha Tanzania nzima (technology na automation) na production ni kweli iwe kubwa na ikiwa kubwa kumbuka vitu vitashuka bei na wengi hawatawekeza nguvu zao huko, ila sababu chakula ni uhai basi Serikali na nchi ifanye juhudi za kuongeza supply no matter hata kama faida (margins zitashuka mpaka pesa ndogo kuliko) ila tukishiba tutaangalia kuwekeza kwenye vitu ambavyo karne ya 21 vinahitaji human input zaidi na haviwezi kufanya na machinery perfectly.
 
Yeyote anaweza kusema lolote ... There factors to consider . Dunia ya hivi Leo we are not pursuing our own individual interests .. Kuna factors za kuconsider. Be an avid reader Fanya tafiti kadri uwezavyo .

Taarifa hizo still ni taarifa ghafi hakuna processing industry ya kuzichakata .
 
Sorry sijaenda deep sana lakini labda tuanzie hapa.... Masoko yanasemaje ? Sababu sidhani kama Tatizo ni Production per se.

Dunia ya sasa mtu mmoja anaweza kulisha Tanzania nzima (technology na automation) na production ni kweli iwe kubwa na ikiwa kubwa kumbuka vitu vitashuka bei na wengi hawatawekeza nguvu zao huko, ila sababu chakula ni uhai basi Serikali na nchi ifanye juhudi za kuongeza supply no matter hata kama faida (margins zitashuka mpaka pesa ndogo kuliko) ila tukishiba tutaangalia kuwekeza kwenye vitu ambavyo karne ya 21 vinahitaji human input zaidi na haviwezi kufanya na machinery perfectly.
tatizo linaanzia kwenye uzalishaji kwani licha ya kuanza kuuza nje hapa ndani kwa uzalishaji wa sasa bado hatujitoshelezi kwa mazao kama ngano ,sukari na mafuta ya kupikia ,hivyo tatizo kubwa ni uzalishaji au uwekezaji na ndipo tutafute masoko ambayo siyo tatizo kubwa kwani uhitaji pia ni mkubwa na nchi yetu ina diplomasia nzuri na mataifa mengi
 
tatizo linaanzia kwenye uzalishaji kwani licha ya kuanza kuuza nje hapa ndani kwa uzalishaji wa sasa bado hatujitoshelezi
Naam mwaka huu nimezalisha labda tani 10; kutokana na soko la ajabu ajabu labda sikuuza nangojea mwaka kesho huenda bei itapanda (isipopanda huenda ikala kwangu) huenda mimi na wenzangu tungezalisha tani 100 kutokana na watu hawana buying power huenda hata gharama ya mbolea isingerudi kutokana na ni kiasi gani hao watu wanamudu... Na sio kwamba mimi kuweka tani zangu 10 watu hawana njaa (nisingefanya hivyo sababu storage ni gharama)..., sababu kuu ni kwamba watu kipato chao ni kidogo hivyo badala ya milo mitatu wanakula miwili....

Ukiniambia niuze nje kuanzia mambo ya vibali na quality (mahindi yangu quality mbovu sababu hata utunzaji ukipima kuna molds) hivyo masoko ya magharibi ya mbali siwezi kuyapata na hata nikiyapata hao traders wanataka long term relationship na mimi mtu wa bahati nasibu na kutegemea mvua hawawezi kuniamini
kwa mazao kama ngano ,sukari na mafuta ya kupikia ,hivyo tatizo kubwa ni uzalishaji au uwekezaji na ndipo tutafute masoko ambayo siyo tatizo kubwa kwani uhitaji pia ni mkubwa na nchi yetu ina diplomasia nzuri na mataifa mengi
Kwamba mafuta ya kupikia na sukari vinalimwa wapi au unaongelea finished products? kama unaongelea malighafi hata mimi na wewe kabla hatujajiunga kufanya hivyo hao waliofanya nawanaofanya hivyo mwaka hadi mwaka consistence yao ya mapato ipoje ? Kwanini tuangalia mataifa mengi wakati hata ndani tu kuna watu wana njaa ? kwanini tusiwauzie hawa (utakumbuka kwamba hawana buying power) hivyo ndugu yangu kutoka hapa kufika pale inahitaji nguvu za pamoja kutoka kwenye industries tofauti..., na kabla hatujawaza nje tuwaze ni vipi hata wa ndani wanaweza wakapata basic needs kwa kuuza na kununuliana (ni wapi majority wanaweza wakawa absorbed kwa kupata ajira zenye ujira)

Kama kilimo kinalipa / kikianza kulipa kwa majority wenyewe tu watakwenda kufanya hivyo wala bila kuambiwa..., lakini soko la nje sio guaranteed kama unavyodhani (mataifa ya nje ukisema free market watakupiga na kikwazo cha quality yako kwamba ni mbovu na utaendelea kuwauzia malighafi na wao wanakupa finished products)

In short its rather complicated na solution inahitaji system overhaul...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom