Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

mkuu Malila

hivi hakuna namna katika hili zao la ndizi ukafanya semi-processing, ukanunua ndizi kwa wakulima ukazimenya, kuziosha vizuri na kuzipack kwenye plastic bags kisha ukasambaza kwenye maduka na supermarkets zikahifadhiwa katika ubaridi ....

mwenye kufahamu lolote please
 
Hapa inabidi wajasiriamali wakune vichwa ili hatimaye watoke na jibu la swali hili, viazi siku hizi vinamenywa,na kukaushwa na kuwekwa ktk mifuko na usambazaji ni rahisi sana.
 
Mkuu tafadhali toa maelezo namna gani ya kupata mashamba huko Mahenge

Nalifanyia kazi mkuu, ndio maana ile changamoto ya daraja sasa ina majibu. Muda si mrefu tutapata majibu na njia rahisi ya kuipata ardhi huko Mahenge.
 
Vizuri mkuu tatizo ni ardhi yenye uhakika mfano mkoano kilimanjaro inafaa sana lakini hakuna eneo lenye kiasi ya hekta kumi bila mabonde na milima

Kwa sasa lazima tufikirie kumiliki mashamba makubwa, na kama ni mashamba makubwa inatulazimu tutafute nje ya maeneo kama Kilimanjaro, mikoa kama Kigoma/Rukwa bado kuna mapori mazuri ya kulima.
 
Kilimo cha migomba ni kizuri sana. Kuna Mradi mahususi wa kilimo cha Migomba ya kisasa kilichokuwa kinafadhiliwa kati ya TZ na Belgium katika wilaya zote Mkoa wa Kagera na Kibondo (Kigoma). Nimeiona migomba ambayo imetokana na Mradi huo maeneo ya Biharamulo, ni mizuri sana! Kwa Utaalamu, jaribu kuwasiliana na Ofisi ya Kilimo, Mkoa wa Kagera wanaweza kukupa maelezo na wapi unaweza kupata mbegu zake.
 
Tunaita frozen food. Tanzania inahitaji frozen food ili kupunguza uhaba wa chakula kwani mazao mengi yanaharibika shambani na pia itasaidia kuwapa wateja chaguo la bei. Kwani frozen food mara nyingi ni bei ya chini kulinganisha na fresh food. Pia itaongeza uhakika kwa mkulima kuuza ndizi zake. Huku Ulaya watu wananunua mihogo ambayo ni frozen ambayo imekwisha menywa Mingi inatoka Costa Rica . Kwahiyo ndizi pia inawezekana .
 
PESAYAKO

nashukuru kwa kutoa mwanga kwa hoja husika

kwa kuongezea tu, semi-processed food humpunguzia kadhia na muda mtumiaji/mteja (end user) kwani kazi ya kumenya, kukatakata na kufanya usafi inakuwa imeshafanyika tayari
 
Last edited by a moderator:
Tehe tehe tehe, ndugu zangu wa kule Pangani-Tanga, Bagamoyo-Pwani, Sumbawanga-Rukwa na kule ufipani watakuwa wameupenda sana huu uzi ila kwa mtazamo tofauti. Wakati wewe unahusianisha migomba na uchumi, wao wanafikiria misukule (ndondocha) wataoweza kuwavuna baada ya kuwa na uhakika wa migomba ya kufanyia viini macho.

Mchoma mkaa, mkata kuni, mpasua mbao na mpita njia wana mtazamo tofauti juu ya mti mmoja.
 
Nimepata mawazo zaidi toka kwa mtalaam wa kilimo SUA, kasema ili kupata mavuno mazuri kipimo kiwe 4m x 4m na ukiweza nenda 4m x 5m. Hii itakupa mashina 285 kwa ekari moja. Kwa wanaotaka kulima mgomba, hicho kinaweza kuwa kitu muhimu sana ktk kuanza kilimo hiki.
 
mkuu Malila

hivi hakuna namna katika hili zao la ndizi ukafanya semi-processing, ukanunua ndizi kwa wakulima ukazimenya, kuziosha vizuri na kuzipack kwenye plastic bags kisha ukasambaza kwenye maduka na supermarkets zikahifadhiwa katika ubaridi ....

mwenye kufahamu lolote please

Linawezekana bila tatizo lolote, Yaani hakuna shaka unaweza kufanya hata maindi mabichi, muhimu tuu umeme uwepo maana friji likizima kwisha kazi.
 
Nimepata mawazo zaidi toka kwa mtalaam wa kilimo SUA, kasema ili kupata mavuno mazuri kipimo kiwe 4m x 4m na ukiweza nenda 4m x 5m. Hii itakupa mashina 285 kwa ekari moja. Kwa wanaotaka kulima mgomba, hicho kinaweza kuwa kitu muhimu sana ktk kuanza kilimo hiki.
mkuu malila kwanza shukrani kwa uzi mzuri. mi toka siku nyingi nina nia ya kufanya kilimo cha ndizi kama chanzo kikuu cha pato langu hivyo nimetafiti sana. uganda wanasema wanapanda 3x1.5. kitu kinacholeta mikungu 800 kwa ekari.
 
Nimepata mawazo zaidi toka kwa mtalaam wa kilimo SUA, kasema ili kupata mavuno mazuri kipimo kiwe 4m x 4m na ukiweza nenda 4m x 5m. Hii itakupa mashina 285 kwa ekari moja. Kwa wanaotaka kulima mgomba, hicho kinaweza kuwa kitu muhimu sana ktk kuanza kilimo hiki.
pia kunachangamoto ya upandaji. watu wengi tunategemea machipukizi ambapo utahiji machipukizi 500 hadi 800 kwa eka maana machipukizi 5000-8000 kwa eka kumi ambayo utabidi ununue kwa wakulima wenzako hivyo utabidi uwe sehemu ya wakulima wengi kama rungwe na kilombero.
 
Kwa sasa lazima tufikirie kumiliki mashamba makubwa, na kama ni mashamba makubwa inatulazimu tutafute nje ya maeneo kama Kilimanjaro, mikoa kama Kigoma/Rukwa bado kuna mapori mazuri ya kulima.
mi nafikiria kuanzia mwezi wa kwanza mwakani ekari kama kumi huko rungwe. tatizo huku ardhi ghali sana ukitupatia taarifa za mahenge, mbingu na maeneo mengine ya kilombero utatusaidia sana wakulima wadogo rungwe wanauza mkungu kati ya 1000-1500. wakati mlanguzi anaenda dar kuuzakati ya 15000-20000. tatizo ni kwamba wakulima hawa wanamigomba michache sana.
 
Tayari nimeshamtuma Karl peters wangu Chita november hii nitapata majibu.
 
Kilimo cha migomba ni kizuri sana. Kuna Mradi mahususi wa kilimo cha Migomba ya kisasa kilichokuwa kinafadhiliwa kati ya TZ na Belgium katika wilaya zote Mkoa wa Kagera na Kibondo (Kigoma). Nimeiona migomba ambayo imetokana na Mradi huo maeneo ya Biharamulo, ni mizuri sana! Kwa Utaalamu, jaribu kuwasiliana na Ofisi ya Kilimo, Mkoa wa Kagera wanaweza kukupa maelezo na wapi unaweza kupata mbegu zake.

Kuna rafiki yangu amenipa habari ya ndizi fulani zinaitwa Nitwishe nafikiri ni jina la utani wakimaanisha mkungu wake unakuwa mkubwa sana kiasi cha kwamba hauwezi kujitwisha mwenyewe mpaka mtu akutwishe. Je, hizo ndo ndizi zilizotokana na huo mradi? nasikia zinafanya vizuri sana sokoni na hizo ndizi zinafaa kuliwa kwa kupikwa pia hata zikiiva zinakuwa tamu sana pia zinamatumika hadi kwenye viwanda vya Biskuti. Wengi nasikia wameacha kazi na kujikita kwenye hicho kilimo. Je, aina hiyo ya mgomba unaweza stawi maeneo ya Pwani (Rufiji) ? Nataka na mimi nijaribu hiyo kitu. Pia anayejua jina lake la kitaalamu tafadhali atufahamishe.
 
Kuna mkungu unaotokana na Mradi huu toka shamba moja la mkulima huko Ngara umefikia kilo 230! Kuna taarifa huenda ukavunja rekodi katika vitabu vya Guieness. Mradi umezalisha takriban aina kama tatu za mbegu ambazo zinafaa kwa biashara kuanzia kula hadi kutengeneza mvinyo! Kwa maelezo zaidi, fanya mawasiliano na maafisa kilimo wilaya za Mkoa wa Kagera na wilaya ya Kibondo mkoa wa Kigoma ambako Mradi huu umetekelezwa.
 
Karibuni mahenge. SIto migomba tu hata mipalachichi inakubali. Mtimbira kwa migomba pako poa sana. I can give u people ABC. TIWASILIANE. NITAWASAIDIA.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom