Ushauri wa kanuni bora za kilimo cha Migomba na Soko lake

Pia kwa habari ya mbegu za kuanzia ni kweli vituo vya utafiti wanazo, kama kile cha Minazi DSM ninakumbuka miaka kama 12 iliyopita walionyesha teknolojia ya kubeba mashina/ mbegu za migomba kwa mamia nani ya kichupa kidogo. Hivyo kwa wanaoenda kulima mbali wanaweza kupata mbegu na teknolojia hiyo ya kusafirisha mbegu toka kwao.

Mkuu, naomba unielekeze vizuri zaidi kuhusu kilipo kituo hiki, pamoja na namba zao za simu kama unazo. Nataka kuwasiliana nao.
Asante.
 
Ni kweli, ni gharama sana pale Mbingu, hata juzi nimeongea na bosi wa MOCOA kasema, kipande hapa Mbingu ni balaa. Hii vita simalizii jf hapa, naenda huko huko hata kama ni Chita.

Mkuu Chita kuna Kambi pale na Jeshi la wananchi na ni walimaji wazuri...... wasije wakakuwekea 'usiku' kuekeza...!!
 
Mkuu, naomba unielekeze vizuri zaidi kuhusu kilipo kituo hiki, pamoja na namba zao za simu kama unazo. Nataka kuwasiliana nao.
Asante.

Simu yao nilishafuta kitambo, ila ukiwa mwenge dar, fuata njia ya kwenda Coca Cola, mkono wako wa kuume mbele kidogo, uliza ofisi za mbegu bora za kilimo ( zamani ilijulikana sana kwa miembe/minazi bora).
 
Thanks Mkuu.
 
Wale ni jkt sio jw, hawa tutashirikiana kukimbiza nguruwe pori mkuu. Wakiwa majirani zako usiwazuie kuficha pololo lao bandani kwako, ukiwazibia wanakubambika kesi !!!!!!!!!!!!!

Hapo kwenye red kaka umenikumbusha mbali, kumbe msamiati huo bado upo kwenye matumizi huko jakata. Nakuaminia kaka!
 
Waliokosa jakata bahati yao mbaya, kuna siku nikiwa poultry coy Ruvu, ilibidi nimeze mayai mawili mabichi fasta kufuta ushahidi !!!!!!!!
 
Kwii kwii kwiiii,....... siku hiyo pololo liligoma kaka, ilibidi mayai yakapasukie tumboni kama chatu, walahi umenikumbusha mbali! Nilimtaimu jamaa kombati yake alikuwa ameanika nilivokuja kuivaa niliitupa kubaini ilivyokuwa imejaa Chawa, chawa walikuwa wamepewa jina fulani nimelisahau....
 
haaa haaa haaaa

dah ... jkt kiboko

nilienda kuiba zabibu nyeupe pale kwenye shamba la zabibu makutupora jkt ... afande akatokea nilijidumbukiza kwenye shimo refu kutoka ikawa ishu, ikabidi nivue kombati nilichane chane ili kutengeneza kamba ya kupandia
 
I hope umesha acha wizi mkuu
 
I hope umesha acha wizi mkuu
Kule tulikuwa hatuibi, ila tulikuwa tunajifunza mbinu nzuri na mbaya za kuishi uraiani. Kwa hiyo baada ya jakata unachagua mbinu nzuri na zile mbaya unaziacha kule kule jakata.Kupitia jakata nilijifunza kula mihogo mibichi na viazi vitamu na hata hoho mbichi kumbe zinaliwa mbichi, hiyo ni jkt.
 
hahahaaa nilikuwa namtania mkuu hata mimi nilivyokuwa sekondari nilikuwa mwizi sana wa Maparachichi ila haimaanishi kuwa mimi ni mwizi I wish ningepita JKT
 
migomba.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe apiga marufuku ‘kuchumbia migomba’
SERIKALI wilayani Rungwe mkoani Mbeya imepiga marufuku wanunuzi na wachuuzi wa ndizi kuacha mara moja tabia ya kulipia mashina ya zao hilo kabla halijazaa kwa wakulima mashambani. Imesema tabia hiyo inawanyonya wakulima.Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Chrispin Meela alitoa agizo hilo alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mikakati ya halmashauri hiyo katika kuhakikisha inatafuta soko la uhakika la zao hilo.

Meela alisema ipo tabia ya wafanyabiashara wa ndizi ‘kuchumbia migomba’ ama mikungu michanga kwa kuwapatia wakulima fedha kidogo jambo linalowadidimiza kimaendeleo. Alisema Serikali wilayani Rungwe imeweka mikakati mizuri ya kuhakikisha zao hilo linakuwa na ubora na kuwapo kwa soko la uhakika ili kuweza kuitangaza Wilaya ya kwa kilimo bora cha zao la ndizi mbichi na mbivu.

Meela alisema kuwa kitendo cha wachuuzi kununua migomba ya ndizi ikiwa mashambani (kuchumbia) kunachangia kwa kiasi kikubwa kumnyonya mkulima na hivyo kuendelea kuishi maisha duni na kushindwa kujikwamua kiuchumi hususan kunufaika na zao hilo. Wilaya ya Rungwe ni miongoni mwa wilaya mkoani Mbeya zinazozalisha zao la ndizi kwa wingi ambapo wananchi wengi wanategemea kilimo cha zao hilo.

Kwa upande wake mkulima Frank Kisondela ambaye ni mkazi wa Lufingo alisema kuwa wanaishukuru Serikali kwa uamuzi wa kupiga marufuku na kutafuta soko la uhakika ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa wakulima kujikwamua kiuchumi.

Nchi yetu ina mabonde mengi yafaayo kulima migomba na hatimaye tunaweza vuna ndizi, kuna nyika nzuri ambazo zikilimwa kwa kumwagilia tunaweza pata zao lingine la biashara. Zipo aina nyingi sana za migomba na hata hybrid zipo. Migomba ni annual plant, sina hakika sana kama ni binual. Mkungu mzuri pale mahakama ya ndizi Mabibo unafikia Tsh 20,000/ ( hii bei ni ya mwezi wa pili 2013, sijui leo), kule Mbingu mwezi huo huo ilikuwa ni Tsh 5000/ kwa wakulima.

Eka moja huoteshwa migomba kama 500 ikiwa spacing itakuwa 3m x 3m. Kama ukiwa na eka kumi za mgomba huko Mahenge/Kilosa utakuwa na migomba 5000, na kama utavuna mikungu 300 kwa mwezi utapata 1,500,000/ ukiwa shambani na ukapata 10,000,000/ kama utafikisha Mabibo. Hapa nazungumzia mshale/mzuzu.

Gharama za matunzo si kubwa, na magonjwa si mengi, zaidi sana ni maji na thinning ili kupata mazao bora, mbolea ni muhimu.

Najua kuna watalaamu wengi sana wa kilimo, mimi nimechokoza maada ili kwa pamoja tuishambulie na kutoka na kitu kizuri kwa faida yetu sote, kukiwa na kosa nisamehewe bure. Kwa sasa Wachina wanajenga daraja la mto Kilombero, twendeni Mahenge tukalime mgomba.
 
Mkuu tafadhali toa maelezo namna gani ya kupata mashamba huko Mahenge
 
Vizuri mkuu tatizo ni ardhi yenye uhakika mfano mkoano kilimanjaro inafaa sana lakini hakuna eneo lenye kiasi ya hekta kumi bila mabonde na milima
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom