Usalama wa Taifa: Mpo likizo?

Status
Not open for further replies.
Mwafrika wa kike,

Kudos kwa ujasiri na kamwe usitetereshwe na fisadist ambaye ni kibaraka mwenye kujipendekeza huko kwa watawala. Kikubwa ni kuendeleza hii vita dhidi ya ufisadi na TISS ambayo ina makachero wake katika kila kona (I honestly believe they have someone within BoT). Kama wameshindwa kuzuia ufisadi (how can they while some of them are), kusaidia mwanasheria mkuu na polisi kuwashtaki wahusika wote, basi kuna haja gani kuwa nao?

Kulingana na taarifa yako, naona hii nepotism imeshamiri kwenye serikali ya JK pia. Wazo hili linakuja kutokana na ukweli kwamba hiyo Tangold inahusiana na IMMA. Je, aliyekuwa akiiongoza IMMA kwa muda mrefu na ambaye bado ni mshirika mkuu katika mawakili hawa, si ndiye yule aliyeteuliwa kuiwakilisha Tanzania kwenye nchi inayojulikana kama Umoja wa Kifalme? Huko nako nasikia alimshurutisha fisadi wa kizazi chetu kuwa kiongozi wa watanzania kwa manufaa yake!!!

Yaani huu mtandao wa mafisadi ni mkubwa ajabu na wana nguvu za mali. Nasi basi tuendelee kuungana katika JF na kutumia nguvu zetu za akili, ufahamu na sauti, na hakika tutashinda!
 
Hold on a minute.. yawezekana Balali alipomuambia mama Meghji kuwa zilikuwa ni sababu za "Usalama" alikuwa anajua anachozungumzia? Mtu mkubwa kama yeye kuja na sababu ya "usalama" kati ya sababu zote duniani..

Ndio hapo sasa, huu usalama unatumiwa kila mahali hadi inatisha!
 
Haya sasa:
TISS - Tanzania Intelligence and Security Service;
AU
TISS - Tanzana Inter-bank Services System

Dr Slaa atueleze alikuwa na maana ipi. Inter-bank service ambayo haikuwa na jina la benki husika, alama ambayo laa na wenzake wasingeweza kuitambua?

Halafu ni kwa vipi hizo TISS z Meremeta na DeepGreen na wenzake ziwe nyakati hizo hasa Aug. hadi Dec.? Ni udadisi tu, mimi sina majibu wala ufahamu.

Kalamu hiyo TISS ya benki tafsiri yake sahihi ni

TISS - Tanzania Inter-Bank Settlement System na wala sio Services kama huyo mchovu alivyosema hapo juu.

Hii ni system ya kufanya payments between banks and accounts ambayo inakuwa facilitated na BOT. Ukilipa benk through TISS ya benk sio kwamba statement yako itaonyesha kwamba umemlipa TISS as a system bali utaonyesha kuwa umelipa account fulani.

Hii ni mchezo wa maneno ambao unajulikana na you can tell kuwa hata fisadi mwenyewe kachemsha tafsiri ya kibenki ya TISS maana hajui anachojaribu kuspin hapa.
 
nimeamua kununua kijikombe cha gahawa, na kashata zangu, ladu kidogo pembeni, na vikaimati.. sichezi mbali..

Bi. mdogo mwaga vitu nakuaminia.. na nimeandaa pongezi zako zis weekend..!
 
Heshima yako. Ongera sana kwa kuwa na moyo wa ujasiri kiasi hiki. Tanzania hii inahitaji watu kama wewe.

Hii issue ya ufisadi ni chain ndefu inayoitaji kila mtu kujitahidi kufuatilia na kutoa habari hizi bila kificho kwani tumeona jinsi Dr. Slaa na wenzake walivyojitahidi japo walisema wanapiga kelele na kelele za mlango hazimzuii mwenye nyumba kulala lakini lastly wakubali japo not 100%.

Mapambano yaendelee mpaka kitaeleweka.

Ubarikiwe sana.
 
Duh hizi aibu za mchana mwanawane! inaelekea wakati tunasheherekea hizi public holidays mafisadi wanakuwa na ngoma wanazocheza gizani.

By the way wana JF msimind, ni majina tu yanafanana, sina hisa huko deep green!

ha ha ha ha ,

green29 hata mimi nilianza kushangaa kuwa unataka kuwasaliti wenzako wa deepgreen (lol). Jamaa wanacheza na tarehe tu hapa, wakati wachaga na wapare wanachoma mbuzi na kunywa mbege Moshi wakidhani kuwa benki zimefungwa, wenzao wanafungua account siku ya sikukuu!

Only in Tanzania ndio mtu anaweza kufanya blanda kama hii na akaget away with it huku akisifiwa na vyombo vya habari kuwa ....
 
nimeamua kununua kijikombe cha gahawa, na kashata zangu, ladu kidogo pembeni, na vikaimati.. sichezi mbali..

Bi. mdogo mwaga vitu nakuaminia.. na nimeandaa pongezi zako zis weekend..!

kwi kwi kwi

wewe endeleza vikaimati tu wakati takaimati imati service systems (TISS) wanakutafuta ukamatwe kwa kumiliki vikaimati
 
Katika vitu ambavyo viliondoa credibility ya Slaa na mafisadi wa ngono wenzake kwenye donor community, kwa wasomi na wafanyabiashara ni kutangaza kwenye hiyo dossier kwamba neno TISS kwenye transactions walizoona maana yake ni Tanzania Intelligence and Security Service. Hata teller pale Mwanga Community Bank atakwamba TISS kwenye banking jargon manake ni Tanzania Inter-bank Services System. Usalama wa taifa is so incompetent lakini sio kwenye kiwango cha kuandika TISS kwenye transactions, labda wataandika Kagoda Agriculture.

Halafu mpenzi, unajikuza sana kutangaza vita na usalama wa taifa kwasababu they are incompetent as to know kwamba upo Ohio. Na pili who the f are you to deserve their attention?

fiSADIST, you are advised to refrain from disclosing someone's ID or location whether fictitious or factual. Let the person do so of their own accord and not on basis of counter-argument by you.
Have a nice day!
 
Icadon:
Kuanzia tarehe mosi Aug. hadi Desemba 2005 kulikuwa na janga gani katika nchi jirani lililosababisha matumizi hao?

Covert Ops si lazima kuwe na janga..mfano mzuri kile kichapo alichokuwa anapewa Buyoya wakati wa usiku pale mpakani...
 
Wana JF na especially my sister the African Lady.

Let us take a deep breath and read between the lines. Ukweli ni kwamba hizo transactions ni fishy yes, and in this case TISS ni Tanzania Inter-Bank Settlement System, na ni system(and I know how it works), currently being used to facilitate inter-bank transactions within local banks in Tanzania. Kinachotokea ni kama hutaki ku-expose who is the actual recipient was hizo pesa na kama ni transansaction within the realm of the local banking system, then kwenye transaction logs zako unaweza kuweka TISS. Ila nivigumu kuiweka hivyo kama transaction ina involve foreign banks (meaning outside your local banking realm) manake sheria za money laundering zitakubana, lakini napo pia kuna mbinu zingine zinazoweza kutumika.

Nadhani issue ya TISS (Idara) kuhusiana na hilo transaction log siyo and we could be barking at the wrong tree! Nadhani kilichotokea ni kuwa pesa hizo zilikombwa mara ya mwisho na wenye akaunti wakatoa order ziwekwe kwenye local account kwenye benki nyingine through TISS (inter-bank settlement) badala ya kuandika cheques etc.

Lingine ni kwamba Tanzania Intelligence Community lina watu very well versed with their profession and most of them are very articulate professionals, na hilo I stand by my comment and I don't have to prove it, ila pia kuna wachache wanaojidai wamo kumbe hawamo na ndio hao tunakumbana nao mitaani mbwembwe nyiingi. Kwa mfano kwa issue ya BOT niliandika majuzi kuwa walimwabia Balali mara nyingi tu kuwa analizwa lakini hakusikia, kumbuka huyu jamaa BWM alimpa kichwa saana.Hata ile document ya kwanza kuhusu BOT scam alionyeshwa na TISS yeye akapuuzia, na hii ni kala ya circulation yake over the internet! Sasa la ajabu ni kwamba, yeye badala ya kusikiliza ushauri wa TISS akatumia bango la TISS (according to Meghji)kuwa malipo ya Kagoda ni kwa shughuli za usalama wa taifa, ambalo pia nina uhakika Mama Meghji amelizua tu. Yeye aliboronga na hata hiyo barua ya ku-retract naamini kaiandika juzi tu! Mbona mwanzoni alikuwa anamtetea Balali. Mama akubali tu kazi imemshinda; alichoweza ni kuziagiza suti za JK for inauguration ceremony hapo alifanya kazi nzuri!

La mwisho ni kwamba tusiliangalie hili la BOT kuwa ni kubwa mno; makubwa yapo ambapo serikali inapoteza over $2 million kila siku na mahali hapo ni TRA. Kama kuna penye ufisadi kikomo ni TRA, kuanzia system yenyewe ya taxation, structure ya shirika lenyewe na viongozi wake ndo basi tena, wakiongozwa na Yona, Mramba, Meghji! Kama kuna wa kuwavalia njuga ni TRA, kwa vile hakuna nchi inayoweza kuendelea kama haina taxation system inayoeleweka. Yetu ni kumliza mchapa kazi!
 
Icadon
Nkurunzinza aliingia madarakani lini vile? nakumbuka akiwa porini alisema (kupitia BBC) kuwa yeye ni rafiki wa JK na atafurahi kusikia JK akichaguliwa kuwa Rais!!!

binafsi nilishangaa a rebel (wakati huo) kusema maneno yale!!!
 
Hao vigogo wa Usalama wa taifa(TISS) wangekuwa wanazingatia proffesionalism wasingeandika barua ambayo ilivuja inayomtaka Waziri Mkuu azuie hoja ya Dr Slaa ya BOT isiingie bungeni. Kwa kweli ni mwanausalama mmoja tu aliyefanya kazi ya usalama wa taifa, huyo aliyetoa hiyo barua na ripoti hadharani. Hao wengine ni wana usalama wa mafisadi tu. Na ni mafisadi kabisa, wamepewa fedha mgao wa BOT

Asha
 
Mwafrika wa Kike,

Chukua tano! mbona ulisema ungenipita? Lakini sikulaumu naamini ulikuwa unakusanya the dataz.

Huyo mjinga anaanza kuongelea mambo ya Ohio, ni dalili ya watu wanaoanza ku panic.

Haya mapambano sio ya fikra tena na sasa yanaanza kuwa physical. Inabidi kujiandaa maana tumenyanyaswa kwa muda mrefu sana na nchi kuibiwa na watu ambao hata hawana respect na ubinadamu.

Muhimu ni kumkamata mmoja mmoja na wataropoka tu. Watu walimsaliti Saddam ndio iwe akina Mkapa?

Tatizo kwa TZ ni kwamba JK bado anatikisa kiberiti kuangalia kama jumuia ya kimataifa na sisi Watanzania je tunaelewa kwa kiasi gani?

Anafanya mchezo mchafu maana hiyo report itavuja siku sio nyingi.

Wapiganaji wa JF, nawatakia mapambano mema, maana mwaka huu ukiisha salama, huenda nchi yetu ikawa ahueni.
 
Yup,

Hii exactly ndio Dr Slaa alitaka ijulikane. Kuna cover ilitumika hapa ili kutoonyesha hizi pesa zimelipwa wapi na kwa nani. Hii TISS inaserve hapa kama double sword. Ukifuatilia zaidi, watalamu watakuambia kuwa TISS ya kibenki imetumika hapa. Lakini mafuatiliaji zaidi ikiwemo majibu ya Balali yalisema kuwa hili ni suala la usalama wa Taifa.

So whether kwa bahati mbaya au double coincidence, hii TISS imetumika both ways lakini in the end, money trail inaishia TISS na serikali inafunga kwa kusema kuwa ni suala la usalama wa taifa.

Lingine ni kwamba Tanzania Intelligence Community lina watu very well versed with their profession and most of them are very articulate professionals, na hilo I stand by my comment and I don't have to prove it, ila pia kuna wachache wanaojidai wamo kumbe hawamo na ndio hao tunakumbana nao mitaani mbwembwe nyiingi. Kwa mfano kwa issue ya BOT niliandika majuzi kuwa walimwabia Balali mara nyingi tu kuwa analizwa lakini hakusikia, kumbuka huyu jamaa BWM alimpa kichwa saana.Hata ile document ya kwanza kuhusu BOT scam alionyeshwa na TISS yeye akapuuzia, na hii ni kala ya circulation yake over the internet! Sasa la ajabu ni kwamba, yeye badala ya kusikiliza ushauri wa TISS akatumia bango la TISS (according to Meghji)kuwa malipo ya Kagoda ni kwa shughuli za usalama wa taifa, ambalo pia nina uhakika Mama Meghji amelizua tu. Yeye aliboronga na hata hiyo barua ya ku-retract naamini kaiandika juzi tu! Mbona mwanzoni alikuwa anamtetea Balali. Mama akubali tu kazi imemshinda; alichoweza ni kuziagiza suti za JK for inauguration ceremony hapo alifanya kazi nzuri!

Exactly this is what I am talking about. Unajua watu wamekuwa wanakwepa sana kuzungumzia hili jambo. Nilizisikia kejeli zote zilizotolewa kwa Dr Slaa kuwa amechemsha kuwa kuhusisha TISS ya kibenki na TISS ya usalama. Kumbuka kuwa cover ya TISS ya usalama imetumika sana hapa kuzuia uchunguzi zaidi katika haya malipo husika. Hawa professionals wa usalama wa taifa ndio wamechemsha hapa kwa kudhani kuwa wangetumia neno TISS la kibenki basi wangefunga trail na watu wachoke.

TISS inatumika kufacilitate payments, hawa wasomi na wataalamu waje watueleze kuwa hizi pesa zilienda wapi na sio kucheza na maneno. Kila mtu akiwemo Slaa alijua TISS ya kibenki na namna inavyofanya kazi. Haya mambo ya kusema kuwa usalama wa taifa ulitumika hapa imegonga pande zote na inabidi TISS wa usalama waje clean kuhusu hili.

La mwisho ni kwamba tusiliangalie hili la BOT kuwa ni kubwa mno; makubwa yapo ambapo serikali inapoteza over $2 million kila siku na mahali hapo ni TRA. Kama kuna penye ufisadi kikomo ni TRA, kuanzia system yenyewe ya taxation, structure ya shirika lenyewe na viongozi wake ndo basi tena, wakiongozwa na Yona, Mramba, Meghji! Kama kuna wa kuwavalia njuga ni TRA, kwa vile hakuna nchi inayoweza kuendelea kama haina taxation system inayoeleweka. Yetu ni kumliza mchapa kazi!

Kweli zalendo,

Tutaanza na BOT kwa sasa maana ndio tembo mkubwa chumbani kwa sasa kisha hayo ya TRA pia yatafuata kadri siku zinavyoenda.
 
Anafanya mchezo mchafu maana hiyo report itavuja siku sio nyingi.

Nina subiri kwanza yule Mkurugenzi wa BoT aliyewekwa kando na tayari ameishahojiwa na vijana wa kazi apelekwe mahakamani. Baada ya hapo nina uhakika hiyo report ya E&Y itatoka tu kwa kuwa huyo jamaa nina uhakika anayo na ni mtu wa visasi lazima ataimwaga ili kuwakomoa, maana ukimwaga mboga mwenzako anamwaga ugali ili wote tukose!

Kama hataitoa huyo basi katika kutajana tajana lazima kuna watu wataimwaga tu ili kukomoana baada ya kuona huu mchezo mchafu unaoendelea. JK sasa hivi amekalia kaa la moto japo hajui, ila kwa kuwa anahisi sisi bado ni wadanganyika, basi mafisadi wenzake watamuumbua tu!
 
Hao vigogo wa Usalama wa taifa(TISS) wangekuwa wanazingatia proffesionalism wasingeandika barua ambayo ilivuja inayomtaka Waziri Mkuu azuie hoja ya Dr Slaa ya BOT isiingie bungeni. Kwa kweli ni mwanausalama mmoja tu aliyefanya kazi ya usalama wa taifa, huyo aliyetoa hiyo barua na ripoti hadharani. Hao wengine ni wana usalama wa mafisadi tu. Na ni mafisadi kabisa, wamepewa fedha mgao wa BOT

Asha

I respect your views and I do understand your opinion. Lakini ukisoma posting yangu nimesema most of them, sija jumlisha wote wala haina maana kuwa hawapo wabovu!

I do not believe in stereotyping nor do I applaud it.
 
Hao vigogo wa Usalama wa taifa(TISS) wangekuwa wanazingatia proffesionalism wasingeandika barua ambayo ilivuja inayomtaka Waziri Mkuu azuie hoja ya Dr Slaa ya BOT isiingie bungeni. Kwa kweli ni mwanausalama mmoja tu aliyefanya kazi ya usalama wa taifa, huyo aliyetoa hiyo barua na ripoti hadharani. Hao wengine ni wana usalama wa mafisadi tu. Na ni mafisadi kabisa, wamepewa fedha mgao wa BOT

Asha

Nakuambia hapa wameshikwa pabaya sana.
Walitumia neno TISS wakidhani kuwa litaishia kwenye ile service ya malipo ya kibenki lakini wakasau kuwa visingizio vyao vya kuwa haya malipo ni ya usalama wa taifa yalikuwa yanawarudisha kwenye the real TISS yenyewe iliiyojaa wezi na mafisadi.

Ile barua kwa waziri mkuu ilipovuja ndipo chupi zilianza kuwabana kisawasawa. Hapa sasa hivi ni bango tu. Kwa nini Kikwete ameacha kutaja makampuni ya DeepGreen na Tangold kwenye report yake?
 
Mwafrika wa Kike,

Chukua tano! mbona ulisema ungenipita? Lakini sikulaumu naamini ulikuwa unakusanya the dataz.

Si unakumbuka Kibaki aliharibu sherehe yetu ya ushindi wa Raila ikabidi iahirishwe kwa muda kidogo. Hata hivyo nilipata majani ya kutosha jumapili na jumatatu na niliondoka jumanne asubuhi sana kama ilivyopangwa mwanzoni.

Huyo mjinga anaanza kuongelea mambo ya Ohio, ni dalili ya watu wanaoanza ku panic.

Haya mapambano sio ya fikra tena na sasa yanaanza kuwa physical. Inabidi kujiandaa maana tumenyanyaswa kwa muda mrefu sana na nchi kuibiwa na watu ambao hata hawana respect na ubinadamu.

Muhimu ni kumkamata mmoja mmoja na wataropoka tu. Watu walimsaliti Saddam ndio iwe akina Mkapa?

Hana idea pale nilipo na hata akijua hakuna kitu anaweza kufanya kwa sasa maana huu ni mtambo mkubwa sana.

Tatizo kwa TZ ni kwamba JK bado anatikisa kiberiti kuangalia kama jumuia ya kimataifa na sisi Watanzania je tunaelewa kwa kiasi gani?

Anafanya mchezo mchafu maana hiyo report itavuja siku sio nyingi.

Wapiganaji wa JF, nawatakia mapambano mema, maana mwaka huu ukiisha salama, huenda nchi yetu ikawa ahueni.

Huu ni mwanzo tu, usiwe na wasiwasi mpiganaji na unakaribishwa Marekani Valentine Day - karibu usherehekee uzinduzi maalumu wa juhudi za kumtafutia Mkjj mke!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom