6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 1,826
- 4,076
Niaje waungwana,
Leo ningependa kupata majibu kutoka kwa wajuzi wa mambo ya kidiplomasia, kuhusu kile kinachoendelea huko kwa ndugu zetu wa Haiti.
Kwanza nafahamu kwamba baada ya uhuru, kila nchi huwa na uongozi (serikali) ambayo chini yake kuna vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kuilinda serikali, nchi na wananchi wanaoongozwa na hiyo serikali. Vyombo hivyo huwa katika mpangilio wa:
1. Jeshi ambalo mamlaka yake ni kulinda nchi, wananchi, na raisi wa nchi ambae ndie "serikali".
2. Polisi ambao kazi yao ni kulinda mali za raia, pia kuwalinda raia, na pia kuhakikisha usalama wa ndani ya nchi wakishirikiana na vyombo vingine vya usalama.
3. Uhamiaji ambao kazi yao ni kuhakikisha ni nani anaeingia na kutoka ndani na nje ya nchi.
4. Askari magereza ambao kazi yao ni kuwalinda wafungwa na watuhumiwa mbali mbali.
5. Vyombo mbali mbali vya usalama wa taifa nk.
Kwa maana hiyo mimi naamini au nafikiri kuwa hata Haiti baada ya kupata uhuru ilifanikiwa kuwa na vyombo hivyo ambavyo kila nchi huwa navyo.
Sasa maswali yangu ni manne tu..
1. Je, Haiti bado inavyo hivyo vyombo vya ulinzi na usalama kama vile jeshi na vyombo vingine vya usalama nk mpaka leo?
2. Kama wanavyo ni kwanini jeshi limeshindwa kuingilia ndani kuilinda nchi, kuwalinda wananchi na kulinda viongozi waliowekwa na wananchi hadi kupelekea nchi hiyo kuomba msaada wa kiulinzi kutoka katika nchi zingine?
3. Inamaana jeshi na vyombo vya usalama vyote vya nchi hiyo vimezidiwa nguvu na magenge ya vijana wasiokuwa na mafunzo yoyote ya kijeshi? Tena wanaotumia salaha za kawaida, nikiwa na maana ni bunduki tu za kawaida, hawana kifaru wala ndege ya jeshi?
4. Je, inamaana jeshi la nchi hiyo ni dhaifu na linashindwa hata na Burundi au Congo ambazo zimekuwa zikitumia majeshi yao kupambana na waasi miaka na miaka bila waasi hao kuziangusha serikali zao?