Usalama wa Taifa: Mpo likizo?

Status
Not open for further replies.
Kimya cha watajwa hapo juu kinasikitisha kwa kweli lakini at least JF watu hawako kimya
 
Taa nyekundu inamuakia Kikwete,mwenzie Kibaki C***** inabana sasa hivi

Kibaki naye alikuwa mpinzani once..

labda Contract ya serikali na Travel Channel ilikuwa inaitaka serikali yetu iwape kila kitu including usafiri wakiwa nchini, na ukizingatia tuna helicopter chache basi wakaona wawape moja ya bird(s) za jeshi. Kukaa kwao kimya ndio kunatufanya tufikirie kuna mkono wa ufisadi, wangetoa tamko na kuonyesha sehemu ya contract(kama hiko).
 
Inaonekana hii ilikuwa ni bitter pill to swallow

I can understand

lakini ndio tumepewa platform sasa tufanyeje tuwalambe miguu hawa watu?
 
Ahh Nimechoka sasa, Nitasema haya na litakalokuwa liwe:

Hawa jamaa wa usalama wa taifa (TISS) wamezidi sana na inabidi tuanze kuwashikia bango nao. Niliwapa breki kidogo maana ile hofu ya agents kunitafuta na kuitafuta familia yangu ilikuwa inanisumbua lakini sasa gloves are off. Nitaanza kuweka vitu vyenu hapa nyie wezi na mafisadi wa usalama wa taifa na lolote mnalotaka kufanya mfanye tu. Ni mimi na JF against nyie:

Katika unafiki wa hali ya juu, Raisi Kikwete juzi ametangaza kumfuta kazi Balali (ambaye alishatangaza kujiuzulu) na kutoa amri ya kuendelea kufanya uchunguzi wa BOT. Cha kutia hasira ni kitendo cha Kikwete kutangaza makampuni 22 ambayo anadai kuwa ndiyo yamehusika na upotevu wa pesa BOT huku kwa makusudi kabisa akiacha kuzitaja kampuni za DeepGreen na Tangold. Cha kutia hasira tena ni kitendo cha ikulu kukataaa kuweka wazi report ya ukaguzi wa BOT iliyofanywa na E&Y kwa masingizio kwamba hiyo report inahusu mambo ya usalama wa taifa.

Huu usalama wa taifa kwa sasa umezidi. Tangold inahusiana moja kwa moja na usalama wa taifa. Jamaa wanahusishwa na wizi mkubwa sana kwa kupitia kampuni hewa. Hebu kumbuka hii iliyotolewa na Dr Slaa:



TANGOLD LIMITED

Kama Orodha ya Mafisadi inavyoonyesha, Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni inayomilikiwa na baadhi ya Mafisadi tuliowataja katika Orodha hiyo. Kuna utata mkubwa zaidi ambao umeigubika kampuni ya Tangold Ltd. Kwanza, licha ya nyaraka kuonyesha kwamba kampuni hiyo ilipewa hati ya kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006, nyaraka za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba Tangold Ltd. ilifungua akaunti ya shilingi Na. 011103024852 NBC Corporate Branch tarehe 1 Januari 2003. Kama ilivyokuwa kwa Deep Green Finance, siku ya Tangold Ltd. kufungua akaunti yake NBC ilikuwa ni Siku ya Mwaka Mpya na siku ya mapumziko kote nchini! Aidha taratibu za kibenki za ufunguaji wa akaunti za makampuni zinalazimu kampuni husika kuwasilisha benki nakala ya usajili wa kampuni, Katiba yake, leseni ya biashara na hati ya mlipa kodi ya TRA (TIN Registration Certificate) kabla ya kuruhusiwa kufungua akaunti. Swali la kujibiwa na NBC pamoja na Serikali ni je, ilikuwaje Tangold Ltd. iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti ya benki kabla hata haijaandikishwa nchini Mauritius achilia mbali kupata hati ya kutimiza masharti ya Tanzania?

Pili, kampuni ya Tangold Ltd. iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha yoyote ile kati ya tarehe 1 Januari 2003 hadi tarehe 1 Agosti 2005 ilipoanza kunyeshewa mvua ya neema ya mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania kutoka BOT! Mvua hiyo ni nje ya mvua ya dola za Marekani 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali na iliinyeshea Tangold Ltd. kama ifuatavyo:

a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 4,703,221,229.08 kwenda kwenye akaunti ya Tangold Ltd. Tarehe hii ni muhimu sana kwani ndiyo siku ambayo BOT ilifanya pia malipo ya kwanza kwa Deep Green Finance kama ilivyoelezewa katika Taarifa hii;

(b) Tarehe 2 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 244,428,386.15 kutoka akaunti yake hiyo kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Kama tuliyoelezea katika Taarifa hii, tarehe 1 Septemba 2005 Deep Green Finance ililipwa pia shilingi 2,083,255,881.60 na BOT;

(c) Tarehe 8 Oktoba 2005 shilingi za Tanzania 39,761,397.98 zilihamishiwa kwenye akaunti ya Tangold Ltd. kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(d) Tarehe 12 Oktoba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 1,690,500,000.00 kwenda Meremeta Limited;

(e) Tarehe 23 Novemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 555,300,048.00 kwenda Meremeta Ltd.;

(f) Tarehe 10 Desemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 100,940,489.71 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(g) Tarehe 12 Desemba 2005, siku mbili kabla ya Uchaguzi Mkuu, Tangold Ltd. ilihamisha shilingi za Tanzania 551,060,000.00 kwenda kwenye akaunti ya Meremeta Ltd

Baada ya hapo Tangold Ltd. haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi tarehe 6 Juni 2006 ilipohamisha shilingi za Tanzania 220,980,370.00 kwenda ‘TISS.' TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service ambalo ni jina la Kiingereza la Idara ya Usalama wa Taifa! Tangu tarehe hiyo hadi leo hii Tangold Ltd. haijaweka wala kutoa fedha nyingine yoyote katika akaunti hiyo. Kwa maana hiyo, katika kipindi cha miezi minne Tangold Ltd. iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi za Tanzania 4,742,982,627.06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd. ya jumla ya shilingi za Tanzania 3,363,531,259.67.

Hebu angalia hapo mkondo wa pesa kutoka benki kuu kwenda Tangold na kuishia TISS.

What the f......k with this TISS, hawa ni kina nani na mbona hawaguswi?
 
Sometimes kuna kitu kinaitwa Covert Operations kwenye nchi jirani..
 
Na ifuatayo ni kwa nini Kikwete ameacha kwa makusudi kuitaja kampuni ya Deep Green (kumbuka tisheti za green za ccm) katika report yake. Hawa jamaa hata file lao limepotea BRELA:





DEEP GREEN FINANCE COMPANY LIMITED

Mnamo tarehe 18 Machi 2004 ilianzishwa kampuni iitwayo Deep Green Finance Co. Ltd. kwa madhumuni ya, pamoja na mengine, kufanya biashara kama ‘mabepari’ na wakopeshaji fedha! Kufuatana na taarifa za Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wakurugenzi wa Deep Green Finance walikuwa ni mabwana Mark Ross Weston wa New Zealand; Anton Taljaard wa Afrika Kusini; na Rudolph van Schalkwyk pia wa Afrika Kusini. Wote watatu ni wakazi wa Afrika Kusini na wanaelekea kuwa ni maafisa na/au wafanyakazi wa Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini. Kufuatana na taarifa za BRELA, wanahisa wa awali wa Deep Green Finance walikuwa ni mawakili Protase R.G. Ishengoma na Stella Ndikimi wa kampuni ya mawakili ya IMMMA Advocates; Nedbank Ltd., Nedbank Africa Investments Ltd. na SBM Nedcor Holdings Ltd. Tarehe 15 Aprili 2005 mawakili Ishengoma na Ndikimi walihamisha hisa zao kwa Nedbank Ltd. na Nedbank Africa Investments Ltd. IMMMA Advocates vile vile ni mawakili wa Tangold Ltd. ambayo imehusishwa na ufisadi tuliouelezea katika Orodha ya Mafisadi.

Taarifa za kibenki tulizonazo zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei 2004, Deep Green Finance ilifungua Akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam. Kitu cha kwanza cha kushangaza ni kwamba siku hiyo ilikuwa ni Sikukuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa siku ya mapumziko. Kitu cha pili cha kushangaza ni kwamba kampuni hii iliruhusiwa kufungua na kuendesha akaunti hiyo bila ya kuingiza wala kutoa fedha yoyote kwa zaidi ya mwaka mmoja kuanzia tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 31 Julai 2005. Kitu cha tatu cha kushangaza ni kwamba pamoja jina la Deep Green ‘Finance’ kuashiria kwamba kampuni hii ni taasisi ya kifedha, orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na BOT tarehe 21 Agosti 2007 haionyeshi kwamba kampuni hii imewahi kusajiliwa na BOT kama taasisi ya kifedha!

Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi minne kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka Wizara ya Fedha na/au BOT. Fedha hizo zilitolewa kwa utaratibu ufuatao:

(a) Tarehe 1 Agosti 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 241740, ilihamisha dola za Marekani 1,354,167.26 au shilingi za Tanzania 1,546,778,770.92 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo fedha hizo zote zilichukuliwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa utaratibu maalum wa haraka (special clearance) na kupelekwa mahali kusikojulikana na kwa madhumuni yasiyofahamika;

(b) Tarehe 1 Septemba 2005 BOT, kwa kutumia hundi Na. 015558, ilihamisha dola za Marekani 1,827,137.44 au shilingi za Tanzania 2,083,255,881.60 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku hiyo hiyo jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 zilichukuliwa kwa mara nyingine tena kwa kutumia utaratibu huo huo maalum wa haraka na kupelekwa kusikojulikana;

(c) Tarehe 8 Septemba 2005 Tangold Ltd. ilihamisha dola za Marekani 100,256.62 au shilingi za Tanzania 114,611,746.80 kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Itakumbukwa kwamba Tangold Ltd. ni kampuni ya kigeni iliyoandikishwa nchini Mauritius tarehe 5 Aprili 2005 na kupewa Cheti cha Kutimiza masharti ya Tanzania tarehe 20 Februari 2006. Hata hivyo, mawaziri kadhaa wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameendelea kudai kuwa kampuni hiyo inamilikiwa kwa asilimia mia moja na Serikali ya Tanzania. Wakurugenzi wa Tangold Ltd. ni Gavana Daudi Balali, Waziri wa Miundombinu Andrew Chenge, Katibu Mkuu (Fedha) Gray Mgonja, Katibu Mkuu (Maji) Patrick Rutabanzibwa na Katibu Mkuu (Ofisi ya Waziri Mkuu) Vincent Mrisho. Kufuatana na barua ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa BOT ya tarehe 21 Desemba 2006, Tangold Ltd. ililipwa na BOT dola za Marekani 13,736,628.73 kwa kupitia akaunti isiyojulikana ya Nedbank Ltd. ya Afrika Kusini na kwa madhumuni yasiyojulikana;

(d) Tarehe 16 Septemba 2005 jumla ya shilingi 129,000,000.00 zilitolewa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance na kuwekwa kwenye akaunti ya muda maalum (FDR);

(e) Tarehe 3 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 2,083,333,333.33 za Wizara ya Fedha zililipwa kwa utaratibu maalum wa haraka kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Inaelekea fedha hizo zililipwa kabla BOT haijaingiza fedha yoyote kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwa vile tarehe 4 Oktoba 2005 BOT ilihamisha dola za Marekani 1,789,075.89 au shilingi 2,083,891,765.35 kwenda kwenye akaunti hiyo;

(f) Tarehe 8 Oktoba 2005 jumla ya shilingi 39,761,397.98 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda Tangold Ltd.;

(g) Tarehe 31 Oktoba 2005 jumla ya shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 fedha za Wizara ya Fedha zilihamishiwa kwenye akaunti ya Deep Green Finance;

(h) Tarehe 2 Novemba 2005 dola za Marekani 1,821,095.57 au shilingi za Tanzania 2,083,653,279.68 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(i) Tarehe 30 Novemba 2005 BOT ilihamisha shilingi za Tanzania 2,083,333,333.33 zikiwa fedha za Wizara ya Fedha kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Siku moja baadaye, dola za Marekani 1,817,199.52 au shilingi za Tanzania 2,184,610,383.04 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(j) Tarehe 10 Desemba 2005 shilingi 100,940,489.71 zilihamishwa kutoka Tangold Ltd. kwenda kwenye akaunti ya Deep Green Finance. Hii ilikuwa ni siku nne tu kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Desemba 14, 2005 kufanyika nchini kote;

(k) Tarehe 19 Desemba 2005, siku tano baada ya Uchaguzi Mkuu kufanyika, dola za Marekani 88,722.17 au shilingi za Tanzania 104,755,554.09 zilihamishwa kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance kwenda kusikojulikana;

(l) Tarehe 9 Februari 2006 shilingi 3,836,800.00 zilihamishwa kwenda akaunti ya mawakili wa Deep Green Finance, IMMMA Advocates, iliyoko benki ya Standard Chartered. Haijulikani kama fedha hizi zilikuwa ni kwa ajili ya malipo ya mawakili hao au la;

(m) Malipo ya mwisho kutoka kwenye akaunti ya Deep Green Finance yalifanywa tarehe 22 Novemba 2006 ambapo jumla ya shilingi 14,465,000.00 zilihamishiwa katika akaunti isiyojulikana ya benki ya Standard Chartered na kwa matumizi yasiyojulikana;

Kutokana na rekodi za kibenki zilizoonyeshwa hapo juu, jumla ya shilingi 10,484,005.39 ziliingizwa katika akaunti ya Deep Green Finance katika kipindi cha miezi minne tu kati ya tarehe 1 Agosti na 10 Desemba 2005. Hiki kilikuwa ni kipindi cha mchakato na/au kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 14 Desemba 2005. Aidha, kuanzia tarehe 11 Desemba 2005 hakuna fedha yoyote iliyoingizwa katika akaunti hiyo hadi tarehe 27 Februari 2007 kampuni hiyo ilipovunjwa ‘kwa hiari’ ya wanahisa wake. Ni muhimu kurudia kwamba, kwa ushahidi huu wa nyaraka za kibenki, kampuni ya Deep Green Finance haikuwa na hata senti moja kabla ya tarehe 1 Agosti 2005 na wala haikupokea hata thumni mara baada ya tarehe 10 Desemba 2005 na mara baada ya Uchaguzi Mkuu.

Kwa taarifa za sasa hivi, inafahamika kwamba faili la Deep Green Finance lililotakiwa kuwa BRELA limetoweka. Tuna kila sababu ya kuamini kwamba hii ilikuwa ni kampuni hewa (shell company) iliyoundwa kwa ajili tu ya kupitishia fedha za umma kutoka Benki Kuu kwenda kusikojulikana wakati wa Uchaguzi Mkuu wa 2005. Ndio maana kampuni hiyo haikuwa na fedha zozote benki kutokea tarehe 1 Mei 2004 hadi tarehe 1 Agosti 2005, wiki tatu kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu. Na ndio maana mabilioni iliyolipwa na Benki Kuu yalilipwa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na mara baada ya Uchaguzi Mkuu kupita malipo hayo ya fedha za umma yalikoma.


Kikwete sisi haya tutazidi kuyaweka kwenye magazeti ya Tanzania mpaka utakapoamua kuzitaja hizi kampuni mbili na kuhakikisha kuwa hawa wanashughulikiwa. Hawa jamaa wa DeepGreen ambao wewe unahusika zaidi na pesa zao zilizotumika kukuweka ikulu lazima wajulikane wazi.

Kwa vile sio kila afisa usalama wa taifa na fisadi, inabidi hao watu wa TISS ambao wana uhusiano na Tangold pia wawekwe wazi hapa kwa sababu halali mtu mpaka kieleweke na wale afisa usalama wa taifa ambao ni safi wasichafuliwe na wachoyo na walafi wachache walioko huko TISS.
 
Hiyo ilikuwa ni pesa ya kununulia kanga, kofia na t-shirt za kijani; pamoja na kulipia pilau nyingi kule kwa akina Rostam (Igunga).

Mataifa ya nje na wafadhiri itabidi watuokoe na janga hili; kwani wakikohoa tu hawa wakubwa tunajua mambo yatarekebika kidogo hapo 2010. Bila hivyo, inaelekea sisi wananchi hatuna njia na uwezo wa kuwaadabisha hawa wahujumu. Sisi hatuna nguvu za kuwashinda hawa; jamani tusaidieni wakubwa.
 
Sometimes kuna kitu kinaitwa Covert Operations kwenye nchi jirani..

Icadon:
Kuanzia tarehe mosi Aug. hadi Desemba 2005 kulikuwa na janga gani katika nchi jirani lililosababisha matumizi hao?
 
Ahh Nimechoka sasa, Nitasema haya na litakalokuwa liwe:

Hawa jamaa wa usalama wa taifa (TISS) wamezidi sana na inabidi tuanze kuwashikia bango nao. Niliwapa breki kidogo maana ile hofu ya agents kunitafuta na kuitafuta familia yangu ilikuwa inanisumbua lakini sasa gloves are off. Nitaanza kuweka vitu vyenu hapa nyie wezi na mafisadi wa usalama wa taifa na lolote mnalotaka kufanya mfanye tu. Ni mimi na JF against nyie:

Katika unafiki wa hali ya juu, Raisi Kikwete juzi ametangaza kumfuta kazi Balali (ambaye alishatangaza kujiuzulu) na kutoa amri ya kuendelea kufanya uchunguzi wa BOT. Cha kutia hasira ni kitendo cha Kikwete kutangaza makampuni 22 ambayo anadai kuwa ndiyo yamehusika na upotevu wa pesa BOT huku kwa makusudi kabisa akiacha kuzitaja kampuni za DeepGreen na Tangold. Cha kutia hasira tena ni kitendo cha ikulu kukataaa kuweka wazi report ya ukaguzi wa BOT iliyofanywa na E&Y kwa masingizio kwamba hiyo report inahusu mambo ya usalama wa taifa.

Huu usalama wa taifa kwa sasa umezidi. Tangold inahusiana moja kwa moja na usalama wa taifa. Jamaa wanahusishwa na wizi mkubwa sana kwa kupitia kampuni hewa. Hebu kumbuka hii iliyotolewa na Dr Slaa:



Hebu angalia hapo mkondo wa pesa kutoka benki kuu kwenda Tangold na kuishia TISS.

What the f......k with this TISS, hawa ni kina nani na mbona hawaguswi?
ha ha haaaaa ha, Jee huijuwi system ni nini?
 
ha ha haaaaa ha, Jee huijuwi system ni nini?

Niambie ndugu yangu maana kila mtu kulingana na alichosomea shuleni ana tafsiri yake tofauti ya neno system. Wanauchumi wana tafsiri tofauti ya system na ile ya madakitari.

Tafsiri yako ni ipi?
 
Katika vitu ambavyo viliondoa credibility ya Slaa na mafisadi wa ngono wenzake kwenye donor community, kwa wasomi na wafanyabiashara ni kutangaza kwenye hiyo dossier kwamba neno TISS kwenye transactions walizoona maana yake ni Tanzania Intelligence and Security Service. Hata teller pale Mwanga Community Bank atakwamba TISS kwenye banking jargon manake ni Tanzania Inter-bank Services System. Usalama wa taifa is so incompetent lakini sio kwenye kiwango cha kuandika TISS kwenye transactions, labda wataandika Kagoda Agriculture.

Halafu mpenzi, unajikuza sana kutangaza vita na usalama wa taifa kwasababu they are incompetent as to know kwamba upo Ohio. Na pili who the f are you to deserve their attention?
 
MwK:
Huenda ni 'system' ya kuwakomoa wananchi, na kuwaneemesha wakubwa; ndivyo ninavyoielewa hiyo 'system' inavyotumiwa humu.
 
Katika vitu ambavyo viliondoa credibility ya Slaa na mafisadi wa ngono wenzake kwenye donor community, kwa wasomi na wafanyabiashara ni kutangaza kwenye hiyo dossier kwamba neno TISS kwenye transactions walizoona maana yake ni Tanzania Intelligence and Security Service. Hata teller pale Mwanga Community Bank atakwamba TISS kwenye banking jargon manake ni Tanzania Inter-bank Services System. Usalama wa taifa is so incompetent lakini sio kwenye kiwango cha kuandika TISS kwenye transactions, labda wataandika Kagoda Agriculture.

Halafu mpenzi, unajikuza sana kutangaza vita na usalama wa taifa kwasababu they are incompetent as to know kwamba upo Ohio. Na pili who the f are you to deserve their attention?

Ufisadi wa usalama wa taifa umewafanya kuwa mambumbumbu hata wasijue kuwa TISS inawahusu wao na kuitumia kila sehemu kwa vile walivyozoea. Fisadi mwingine wa ccm ameitafsiri hiyo TISS ambayo wewe unaiita Tanzania Inter-bank Service system kama Tanzania Internal Surveillance system.

Hii ni game ya maneno na so far kila mtu anaweza kuwaka lake kufunika TISS. Kuhusu attention na usalama wa taifa labda nikuulize wewe wa Ohio utueleze kilichotokea kwako miaka ile ulipokuwa mtawa katika kanisa la katoliki la boston
 
atakwamba TISS kwenye banking jargon manake ni Tanzania Inter-bank Services System. Usalama wa taifa is so incompetent lakini sio kwenye kiwango cha kuandika TISS kwenye transactions, labda wataandika Kagoda Agriculture.


kwa tafsiri yako.

asante wewewe mchaga kwa kutupa habari za Mwanga,Pili asante pia kwa kutambua Kagoda ni kampuni ya kujinufaisha wkwa watu wa usalama wa viongozi.Tatu nashukuru bado unajiita fisadi wakati unafahamu ufisadi ni dhambi.Nne toa hoja sababu hoja ujibiwa kwa hoja,Tano tunakupenda kwasababu itafika wakati utaeleza ukweli wote kuhus ufisadi.
 
Hold on a minute.. yawezekana Balali alipomuambia mama Meghji kuwa zilikuwa ni sababu za "Usalama" alikuwa anajua anachozungumzia? Mtu mkubwa kama yeye kuja na sababu ya "usalama" kati ya sababu zote duniani..
 
Haya sasa:
TISS - Tanzania Intelligence and Security Service;
AU
TISS - Tanzana Inter-bank Services System

Dr Slaa atueleze alikuwa na maana ipi. Inter-bank service ambayo haikuwa na jina la benki husika, alama ambayo laa na wenzake wasingeweza kuitambua?

Halafu ni kwa vipi hizo TISS z Meremeta na DeepGreen na wenzake ziwe nyakati hizo hasa Aug. hadi Dec.? Ni udadisi tu, mimi sina majibu wala ufahamu.
 
Duh hizi aibu za mchana mwanawane! inaelekea wakati tunasheherekea hizi public holidays mafisadi wanakuwa na ngoma wanazocheza gizani.

By the way wana JF msimind, ni majina tu yanafanana, sina hisa huko deep green!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom