Richard mtao
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 209
- 236
Habari wana JF.
Naomba kuanza kwa kuzungumza machache sana ili tuelewane kutokana na mada hii.
Kumekuwa na mada mbalimbali zinazozungumzia maswala ya uzalendo, usalama wa taifa,maafisa usalama wa taiafa, majeshi na vyombo mbalimbali na kila mmoja amezungumzia kwa namna ya peke yake.
Leo mimi nazungumzia je ni kweli kwamba uzalendo unaweza kuwa chanzo cha usalama wa taifa? Sina maana ya kupotosha ama kutengeneza taharuki kwa namna yoyote ile, ninahitaji tujifunze na kuona mambo haya yanaoana kwa kiasi gani na yanaweza vipi kuchangia katika usalama wa taifa lolote duniani.
Nianze kwa kuelezea uzalendo/usalama wa taifa ni nini?
Uzalendo ni imani, hisia ya mtu kufanya jambo lolote ama kujitoa kwaajili ya taifa lake. Unaweza kujumuisha mambo mbalimbali yanayoashiria upendo na kuwakilisha nchi husika katika maeneo mbalimbali imiwemo lugha, alama,michezo na n.k.
Usalama wa Taifa ni ile hali ya nchi au taifa kuwa salama na ulinzi wa kutosha dhidi ya wanainchi, uchumi na taasisi zake zote. Vilevile usalama wa taifa unahusishwa na kutokuwepo kwa matukio ya kigaidi, uhaini, uhujumu, uhasi au mapinduzi yanayosababishwa na mambo mbalimbali.
Uzalendo unanafasi kubwa sana ya kuhakikisha nchi inakuwa salama sana, lakini hiyo itawezekana endapo serikali itashirikiana vyakutosha na jamii katika kuandaa kizazi ambacho kinamapenzi ya dhati na nchi yao, tukiachana na mifumo ya sasa iliyopo(elimu, afya, utawala na uongozi) ambayo kimsingi inasaidia katika kuandaa kizazi bora bado naona kuna haja ya serikali kufanya zaidi ili kuboresha mazingira hayo hasa ukizingatia nchi yetu inakua kila siku na kujifungulia fursa mpya za kiuchumi, kijamii na teknolojia. Na kama mnavyojua hakuna vitu ngumu kwasasa kama vita vya kiuchumi, afya, teknolojia. Hivyo ipo wazi pale taifa lolote linapopiga hatua kubwa basi maadui wanakuwa ni wengi sana kwa lengo la kuishusha au kuififisha kabisa kwenye ramani ya dunia.
Sasa kama huku ndiko tunakoenda( tunakua kiuchumi na kiteknolojia) je mifumo hii iliyopo sasa ambayo kimsingi imetusaidia sana je inaendana na kasi hii? Je wanainchi wangapi wenye uwezo wako tayari kufanya chochote kwajili ya nchi yao?
Nnachomaanisha ni kwamba kuna haja kubwa ya serikali kupitia wizara ama mamlaka husika kuwekeza na kuandaa mpango madhubuti wa muda mrefu utaowezesha jamii zetu kuandaa vizazi vinavyoelewa vinawajibu gani kuanzia katika ngazi za jamii hadi taifa, yaani kwa mfano watu kutotanguliza rasimali mbele kuliko kitu anachopaswa kufanya au mtu yoyote kutomuumiza mwenzie kwasababu zozote zile ambazo ziko nje ya sheria za nchi, ili tuweze kupata watu/viongozi/watumishi ambao sio wezi, sio wenye tamaa, sio wabadhirifu, sio viongozi wenye uchu wa madaraka.
Endapo serikali ikilifanikisha hili kutakuwa na faida nyingi sana zinazoweka uhakika wa usalama wa taifa,baadhi ya faida hizo ni pamoja na Kupungua au kuondokana kabisa kwa matukio ya kihalifu, ubadhirifu,uhujumu, ugaidi,uhaini,mapinduzi, uhasi,upinzani,machafuko,utoroshwaji wa rasilimali za nchi, vita, utakatishaji fedha, umaskini, magonjwa, njaa, ukame nakadharika.
Hivyo nahitimisha kwa kusema Uzalendo ndio msingi Mkuu wa usalama wa taifa. Kwakua unatoa fursa nyingi zinazoweza kulisaidia Taifa wakati wowote. Mfano endapo nchi itakuwa na wazalendo angalau kwa asilimia 90 maan yake nchi ina asilimia 90 za watu wanaoweza kufanya jambo lolote kwajili ya nchi na kama serikali ikihitaji wafanyakazi katika vyombo vya ulinzi na usalama au sekta nyingine yoyote maana yake ina uhakika wa kupaata idadi kubwa sana ya watumishi walio na uzalendo wa hali ya juu sana.
Uzi huu ni kwa maana ya kutaka kuamsha fikra mpya. Karibuni tujengane zaidi.