Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Kipindi cha kagera war Bernard membe jasusi mahiri alikuwa uganda kama muuza spea kwann jwtz wasingetumia watu wao wa MI ?

unajua kuwa MI inaundwa na wanajeshi watupu na unajua ugumu uliopo kutuma mwanajeshi wa nchi A kuingia nchi B ?

mossad ndio wanaodili saana na Iran kwann Israel wasitumie majasusi wa MI ?

unajua kuwa mkuu wa takukuru wa sasa pamoja na kuwa ni mwanajeshi wa jwtz lkn alikuwa ni muajiriwa wa tiss

Umejuaje kama JWTZ hawakua na majasusi wao wa MI?

Au mpaka waje kwenye vyombo vya habari kukuhadithia?

Acha ujinga
 
Ni rahisi sana Afisa kutoka JWTZ kwenda na kuwa DG TISS.. ila sio kipenyo kutoka TISS kwenda kuwa General ( CDF ) kulw JWTZ. Ndio utaelewa nani ni nani.. Sio rahisi nchi kupinduliwa na TISS ila JWTZ wana uwezo wa kupindua chi.. upo hapo Engineer ? Kila chombo kina umuhimu sana maana kwa ufanye kazi wa ushirikiano. Ila JWTZ ni senior
Kasome riwaya ya Mimi na rais.
 
Linaweza kuwa swali lisiloeleweka haraka, Labda nianze na simulizi kwanza

Mwaka 1979 Tanzania iliingia kwenye vita na Uganda maarufu kama vita ya KAGERA. Mwaka 1995 nilikutana na mzee Mkumbi(marehemu) mmoja wa watu ambao walikaribia kabisa kupigana vita hiyo. Miongoni mwa mambo aliyonisimulia ni kuwa yeye alirudia eneo la mwisho ambalo angetoka hapo ilikuwa ni moja kwa moja anaingia uwanja wa vita. Anasema alifurahi sana kwani akiwa kwenye eneo la mwisho ambalo daktari alikuwa anawapima afya ndipo alinusurika, kilichomnusuru ni kukutana na daktari ambaye alikuwa ndugu yake, akamuokoa kwa kueleza kuwa afya yake si mzuri.

Binafsi ingawa sikusema nilimshangaa sana huyu mzee kwa sababu alichokifurahia ni kukwepa majukumu yake ya msingi kama Mwanajeshi, hata huyo daktari kwangu bado hakuwa Mzalendo alitaka mtoto wa nani afe na wa nani abaki? Na hawa ndio wale ambao ni wengi wanaajiriwa kwenye majeshi yetu kwa njia za upendeleo lakini je tumeangalia nini athari yake?

Kuna hii idara maarufu ambayo wengi wanatamani kuajiriwa ambayo ni usalama wa Taifa, Licha ya mshahara na marupurupu yake upande wa pili wa idara hii ukoje(side effect yake ni ipi?) Kuna jamaa waliibuka kwa ahadi za kuajiri watu kwenye Idara hiyo ambapo walikuwa wanahongwa Mil 1 na kuendelea ili kuwapatia watu kazi kwenye Idara hiyo, Hivi ni kweli watu wanaoingia kwa mtindo huo watayaweza hayo majukumu? Au kazi yenyewe ni ile ya kupita kurekodi tu watu wanaomkosoa Rais kwenye vijiwe vya kahawa? Hakuna majukumu ambayo yanamtaka mtu kujitoa ambayo yanaweza kumfanya mtu akwepe kutimiza wajibu wake kama yule mzee aliyekwepa kwenda kupambana Uganda?

NAULIZA TU.
Swali zuri
 
Ni mbaya kuliko JWTZ @ TPDF kwani wapo kazini saa 24 kwa siku saba. Pia hamjui adui na anatakiwa amfahamu kiundani hasa. Hana adui maalum kwani yote yake mradi usalama wa taifa uwe salama. Tiss personnel are supposed to detect and eliminate in covert and/or clandestine way any threat to national security.

Huo ndio ubaya wa TISS. TPDF anasubiri tuvamiwe ndo aingie kazini.
Eti TPDF anasubiri tuvamiwe ndiyo aingie kazini 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣 Ila umesema kweli 😁😁😁😁
 
Ubaya mwingine ni unaweza kusacrifice maisha yako kwa mission ulio ifanikisha mwenyewe..pia wanamaisha magumu sana sababu inawachukua mda mrefu kuishi maisha ambayo sio halisi
Duh! Ila kazi ni kazi tu, kikubwa mkono uende kinywani.
 
Kwa utawala wa Magufuli na Samia, nimeamini TISS ni watu wa kawaida mnoo...

Tuwaheshimu JWTZ wanaolinda mipaka na kuwafanya viongozi hawa kujawa na kiburi...

Tunahitaji mageuzi makubwa mno kwenye taasisi hii
Kumbe na wewe upo humo? Fanyeni mageuzi sasa mpaka mtutangazie huku?
 
Kiinchi hiki ngwengwe tupu..
Lakini mnakijadili kuhusu usalama wa taifa utadhani kina uwezo wa kinyukilia yaani upupu mtupu.
hawa njaa kali wanalinda nini?
upuuzi mtupu tu, sanasana wanafuatafuata vijichama vya upinzani ambako hawana chochote yaani mnachosha kweli kupoteza muda kujadili utopolo kama huu
Hakuna usalama wa taifa wala nini, eti hawalali, wanalinda masaa 24, hebu acheni upuuzi
Vitambi vitupu vimejaa kwenye kaunda suti...
 
Kiinchi hiki ngwengwe tupu..
Lakini mnakijadili kuhusu usalama wa taifa utadhani kina uwezo wa kinyukilia yaani upupu mtupu.
hawa njaa kali wanalinda nini?
upuuzi mtupu tu, sanasana wanafuatafuata vijichama vya upinzani ambako hawana chochote yaani mnachosha kweli kupoteza muda kujadili utopolo kama huu
Hakuna usalama wa taifa wala nini, eti hawalali, wanalinda masaa 24, hebu acheni upuuzi
Vitambi vitupu vimejaa kwenye kaunda suti...
Watakutafuta
 
Ngoja nitafute kabisa Popcorns na Kinywaji baridi nikae nione jinsi ' Wajuvi ' wa haya mambo aliyoyaleta Mleta mada / uzi watakavyotiririka na kuserereka ili hata Mimi ' Ngumbaru ' niweze kujua a,b,c's za hii Taasisi ' Tishio ' ndani na nje ya Tanzania.
Mods huyu si mpige life ban tu 😝😝
 
Nina hakika Nina na uhakika kabisa yakuwa nitakacho kisema Leo nitarukiwa na kushukiwa kama mwewe na mijitu inayo itwa Usalama wa TAIFA na mawakala wao kimsingi Hali ya ufisadi katika TAIFA inazidi kuwa mbaya mbaya mbaya na watu wanao takiwa kuchunguza na kubaini upuuzi HUU wapo na wanalipwa mishahara mikubwa tu.

Tunaambiwa na mkaguzi halimasharu zetu kalibia mamlaka 188 zimetoa Bilioni 88 zimepotea Kwenye mikopo ya vikundi nataka niseme hakuna Halimashauri ambayo Haina vijana wetu wa Usalama wa TAIFA wapo na wanao uwezo wa kuchunguza kama fedha za umma zimepelekwa kwa vikundi kweli au ni hewa nasema hivi maana niliwai Kuta mfano wilaya ya mreba tu, mikopo zaidi ya milioni 60m ipo mikononi mwa vijana wawili na wake zao na hao vijana ni marafiki wakubwa wa hao vijana wetu wanapika wanakunywa pamoja na taarifa wanazo lakini wao wanaahindwa kulipoti ilo tu Kwa idara usika?

HUU wizi tunao ambiwa unajitokeza Nina Imani tunao.vijana wetu pendwa Kwenye mawizara na taasisi zetu je hao vijana walioko uko wanafanya kazi gani kama wanaahindwa kuripoti mambo kama hayo kabla hayajatokea?

Nilichokibaini ni kuwa vijana tunao ila changamoto je wanauwezo wa kuchunguza na kuhoji dhidi ya wizi huo unapotokea?

Yote haya lazima tukubaliane mfumo wa ajira wa vijana wa idara hii unachangamoto kubwa sana

Kitendo Cha kuajili watoto wa wakubwa, vijana wa umoja wa vijana wa ccm ambao wengi wao ni form four failure ni kosa kubwa sana tuna vijana ambao hawana uwezo mfumo ubadilidilishwe
 
Huwa kila siku tunasema, kama CCM itaendelea kukaa madarakani kwa shuruti, mifumo yetu ya utawala itaendelea kuwa mibovu. Kwa hapa tulipofika maana kansa ya athari ya utawala wa shuruti wa CCM imeshaenea nchi nzima, ni aidha yatokee machafuko tuanze upya, ama serekali ipinduliwe kuwe na kipindi cha mpito kuelekea uchaguzi mpya wa kidemokrasia ambao hautapendelea chama chochote kama ilivyo sasa.

Vinginevyo hao usalama wa taifa wataendelea kupatikana kwa mchongo ili kulinda huu mfumo wa wizi wa chama cha mapinduzi. Nilishangaa sana uchaguzi wa 2020 idara ya usalama kufuata maelekezo ya rais aliyekuwa madarakani ya kuchezea uchaguzi kwa kiwango cha kutisha. Ikifika mahali ukaona idara ya usalama wa taifa inafuata matakwa binafsi ya kiongozi aliyeko madarakani, ujue hapo hakuna idara ya usalama tena, bali genge hatari la usalama wa taifa. Kwao hao usalama wa taifa wako kuhakikisha CCM haitoki madarakani, kwani ajira zao zinatokana na CCM kuwepo madarakani, na sio uwezo wao wa kazi.
 
Wanasema ipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya ccm, sijui kama ni kweli...
Na pia vijana wanaofanyiwa recruitment na idara Wana personal relationship na high profile figures wa hii nchi.. just vidokezo TU na mwana mmoja kanipa.

Hilo liko wazi, usalama huu wa taifa uko kulingana na utashi wa watawala walioko madarakani. Na hili limechangiwa na katiba inayomfanya rais kuwa mungu mtu. Ukiangalia ni taasisi iliyoundwa kulingana na mitazamo ya rais aliyekuwa madarakani wakati wa kutungwa kwa hiyo sheria.

Kutokana na udhaifu wa muundo wake, rais anaweza kuagiza wafanye chochote atakacho iwe ni kwa maslahi yake binafsi, au ya chama chake, na sio lazima iwe kwa maslahi ya taifa na watafanya. Tazama hiyo idara ya usalama wa taifa, huwa inafanya kazi kulingana na utashi wa rais anayekuwa madarakani, na sio sheria zitakavyo.
 
Nina hakika Nina na uhakika kabisa yakuwa nitakacho kisema Leo nitarukiwa na kushukiwa kama mwewe na mijitu inayo itwa Usalama wa TAIFA na mawakala wao kimsingi Hali ya ufisadi katika TAIFA inazidi kuwa mbaya mbaya mbaya na watu wanao takiwa kuchunguza na kubaini upuuzi HUU wapo na wanalipwa mishahara mikubwa tu.

Tunaambiwa na mkaguzi halimasharu zetu kalibia mamlaka 188 zimetoa Bilioni 88 zimepotea Kwenye mikopo ya vikundi nataka niseme hakuna Halimashauri ambayo Haina vijana wetu wa Usalama wa TAIFA wapo na wanao uwezo wa kuchunguza kama fedha za umma zimepelekwa Kwa vikundi kweli au ni hewa nasema hivi maana niliwai Kuta mfano wilaya ya mreba tu, mikopo zaidi ya milioni 60m ipo mikononi mwa vijana wawili na wake zao na hao vijana ni marafiki wakubwa wa hao vijana wetu wanapika wanakunywa pamoja na taarifa wanazo lakini wao wanaahindwa kulipoti ilo tu Kwa idara usika?
HUU wizi tunao ambiwa unajitokeza Nina Imani tunao.vijana wetu pendwa Kwenye mawizara na taasisi zetu je hao vijana walioko uko wanafanya kazi gani kama wanaahindwa kuripoti mambo kama hayo kabla hayajatokea?
Nilichokibaini ni kuwa vijana tunao ila changamoto je wanauwezo wa kuchunguza na kuhoji dhidi ya wizi huo unapotokea?
Yote haya lazima tukubaliane mfumo wa ajira wa vijana wa idara hii unachangamoto kubwa sana

Kitendo Cha kuajili watoto wa wakubwa,vijana wa umoja wa vijana wa ccm ambao wengi wao ni form four failure ni kosa kubwa sana tuna vijana ambao hawana uwezo mfumo ubadilidilishwe

Very true

Pale bandarini wamejaa tiss kila kona but wizi ndio kila siku
 
Back
Top Bottom