Upande wa pili wa usalama wa Taifa ukoje?

Kweli kabisa Ndugu watu wanaongeaga tu bila hata facts, au Experience binafsi
Yuko jamaa tulikuwa nae Kazini, in the same Department almost kipind chote cha Rais awamu ya tatu, Tukaenda nae Kuongeza Elimu, awamu ya nne ya JK, Tumerudi Tukapiga Nae kazi Almost 3 Years; Ila Sikuamini wakati Mheshimiwa JPM alipokuwa anahitimisha yale mazoezi ya wanajeshi kwa njia ya Maji, nilimuona akiwa na Gwanda Anapewa mkono na Muheshimiwa Rais; Hapo ndipo nilipojua kuwa TPDF ni chombo cha juu sana kwa ulinzi kama unavyosema.
Kwakweli Ofisin tulishangaa sana, Binafsi sijawahi kumtilia shaka mpaka nilipomuona kwenye hiyo function.
USHAURI: Kama uko Taasi kubwa za Serikali kuwa makini sana na unacho-share na unachosema, inawezekana ukadhurika japo Indirectly.
Da
 
Hiyo kwa kiingereza yaitwa kuwa "discreet", yaani kuwa mwangalifu kwa kila uongeacho au kukifanya ili kuweza kulinda siri na heshima ya taasisi.

TISS ilivurugwa kwa miaka kadhaa pre JPM, pale walipoingia wale wasostahili na zoezi la uhakiki linafanyika.

Mchujo waendelea na wanatemwa wengi.
We
 
Kama uliingia TISS kwa kutoa rushwa au kutumia cheti cha mtu, basi tayari umefanya kosa kubwa sana kwani umevunja miiko inayopaswa kufuatwa wakti wa kuteua makuruta.

Sasa linapokuja suala la uhakiki ambalo linafanyika sasa, wengi wa vijana ambao waliingia kwa kuhonga au kwa kutumia majina makubwa wanapewa muda wa kujitafakari kisha kuondoka ndani ya idara hiyo bila kulipwa chochote.

Hivyo kama uliondolewa kwa sababu hizo hapo juu, basi negative side effects zitakuwa more devastating kuliko positive side effects.

Kuna mdada mmoja nilikuwa namfahamu kwa miaka mingi lakini sikudhani kama alikuwa akifanya kazi huko, ila hivi karibuni alikuja kwangu huku akilia sana.

Nilimuuliza kulikoni bibie, akasema ameambiwa kwamba aweza kustaafu kazi lakini hakutakuwa na malipo yoyote stahiki kama kiinua mgongo wala fedha za kusafiria kwasababu yeye alitumia vyeti vya mtu mwingine.

Fikiria mtu amepiga kazi miaka zaidi ya 30 kazini kwa cheti bandia yaani hakukuwa na uchunguzi mahiri kubaini mtumishi mtarajiwa yaani Vetting na matokeo yake huyu dada yangu ametumbukia shimoni.

Hivyo basi side effects zaweza kukupata ukiwa katika mazingiza hayo au mazingira mengine kama kustaafu ukiwa hukujenga nyumba, au ulikuwa unahanja na vimwana na hukuwa na akili ya future.

Lakini Positive side effects zingine zipo na ukipata nafasi tembelea eneo la Mbweni uone nyumba za maana zilizojengwa na wastaafu na hata wale ambao ndo umri wasogea.
aweza kustaafu kazi lakini hakutakuwa na malipo yoyote stahiki kama kiinua mgongo wala fedha za kusafiria kwasababu yeye alitumia vyeti vya mtu mwingine.




Hahahaha Yan hata 4 hana
 
Mkuu,hawa wa siku hizi hawako hivo. wapo wapo tu. nilikutana na mmojawapo mitaa fulani wakati ule wa vuguvugu la uchaguzi 2015, mdada hivi mwembamba kweli nafikiri hata kilo 50 hana. nikajiuliza, huyu anaweza kuni-arrest kweli? achilia mbali to eliminate the target..! I was puzzled
 
Kazi za kipuuzi sana hizo ,yaani ukahangaike na watu walio na kipato kisa wivu, angalia jinsi mwendazake alivyowatumia hao jamaa kuumiza wenzao kisa wivu. Kazi ambayo haiumizi watu haionei watu wivu na wala haina kusingiziana umbea na urogaji hiyo ndio kazi. Kiufupi fanya biashara zako kula hela yako usifuatilie maisha ya watu hapo umeyapatia
 
kuna shida usalamani kwetu for sure...binafsi najua kazi moja kubwa sana ya under covers ni last para za sms za mange kimambi "hide my ID" undercover yoyote akishajulikana basi ni useless he deserve to die....siku mpaka najishangaa yaani kuna siku niko bar napiga story na mshikaji huku tunakula bia story zikahitaji mawasiliano wakati tunabadilishana no ndo ikabidi nimulize jamaa anaitwa nani akaniambia we save.......usalama...nikapata kigugumizi kidogo nikamuuliza unasema??? akarudia tena Somebody usalama..dah na mimi nikasve the same name...baada ya muda ikabidi ni chunguze nikakuta kweli ni usalama...now najua hadi ofisini kwao...watumishi wao wote waliopo hapo ofisini...na jamaa mwaka jana kapanda cheo ndo alitangaza kila mahali na akafanya bonge la part.... binafsi nina kaconection kaujasusi bt idara nyingine low level kabisa ila methods and tactics remain the same ..so nadhani mwaka jana depo jipya liliingia uraiani kuna kadada kembamba kweli kalegevu haswa nako ni TISS yaan ni nanga mpaka basi...kila nyumba anayoishi haipiti mwezi anatambulika so anaamua kuhama...kahama kama nne alivyokuja kwangu na mimi nikamjua hata sikumficha siku moja nikamwambia wewe ni nanga usalama gani sasa wewe? alimind akataka hadi kulia jamani mim nimehama nyumba ngap sijui ilo nisijulikane lakinj naona hata siwezi nikamwambia ndo unanga wenyewe..... pia maboss wao wanawatumia vibaya sana kiasi kwamba inakua ngumu kuhide ID..
We mkorosho ww
 
Unaweza tumwa Ukafanye misheni flani Kubwa sanaa ambayo Inabdi iwee siriii... Unaweza maliza kiroho safii lakini akatumwa mtu ajee Kukumaliza na wew lakini hata ambiwa sababu ya kukua wew... NA HUWA HAWAJUANII WENGI WAOOOO...!!
Story za vijiwe vya kahawa


Unamjua LYATONGA AUGUSTINO MREMA
 
Mbona hawakuzuia wizi wa tembo,vifaru mpaka wameisha kabisa......makinikia tumeibiwa miaka 20 walikuwa wapi hawa TISS..... Kura zinaibwa huko ZEC na NEC,miswada mibovu bungeni ila bado watu mnawapa credit hao TISS wakati sioni la maana wanalolifanya kwenye ngazi ya kitaifa labda mngesema kusaka petty criminals ila wale moguls sioni hata wakibanwa na TISS ingawa ni mafia wa miaka mingi

TISS is overrated
 
Mna wa over rate sana. Eti hawajuliani kirahisi. Hamjakaa nao mtaa mmoja ndo maana hamuwajui. Wale ni rahisi kuwajua baadhi ya nyumba zao kubwaa afu huoni wakaaji .kuwaona mara chache .na hua wana gari zao na madereva kama taasisi tu za serikali zingine. Ila uvaaji wao ni kaunda tu mara nyingi
Uvaaji
 
Back
Top Bottom