UMEME WAKATIKA UWANJA WA TAIFA!!!Ngeleja jiuzulu

Status
Not open for further replies.
Iyo ni mpaka arusha alaf walvyo mafala waliuleta saa 12 na madakka meng,iv hi ni hujuma ama ni kukomoana kwa kutomchagua MKUU
 
Wachawi kuhusiana na suala la kukatika umeme leo uwanja wa Taifa ni:
  • Serikali-kwa kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la uhaba wa umeme kwa muda mrefu. Toka ahadi ya 2006 kwamba tatizo la umeme litakuwa historia, mpaka mwaka 2011 tunaambiwa rais na waziri sio mvua wala mawingu kwamba wanyeshe mabwawa yajae. Hawatuambii kama umeme unazalishwa kwa mvua na maji peke yake. Wanataja mvua, hawataji makaa ya mawe, gesi na IPTL ya mafuta mazito!
  • Tanesco, kwa kutowasiliana mapema na mamlaka ya Uwanja wa Taifa kuhusiana na ratiba ya kukata umeme. Walitakiwa watangulize maslahi ya nchi kwanza kwa kuhakikisha umeme unakatwa baaada ya sherehe kwisha. Hili limetupa taswira mbaya kama taifa, taifa linalozunguka kila siku kutafuta wawekezaji.
  • Uongozi wa Uwanja wa Taifa. Kila mechi inapopigwa taifa, kuna fungu linatengwa kwa ajili ya gharama za mechi na uwanja kwa ujumla. Niliye gizani nilidhani hizo pesa kweli zinatumika kuandaa mazingira mazuri ya mechi, kumbe ni za kulipana posho!
  • TFF/CECAFA. Hii ni aibu yao. Wana jukumu la kuhakikisha maandalizi ya mashindano yanaenda vizuri, ndo maana nchi mwenyeji hupewa nafasi ya kujiandaa mapema sana. Hakukuwa na sababu ya TFF/CECAFA kukubali mashindano yafanyike TZ wakati hakuna maandalizi ya kutosha. Hela za mapato mnapeleka wapi?
  • Wizara ya Michezo na Utamaduni. hii ndio wizara yenye jukumu la kuendeleza michezo TZ. Hata uwanja wa taifa upo chini yao. Kwa michuano mikubwa kama hii, ungetarajia hawa wanaporojo wahakikishe kila kitu kinaenda sawia, lakini wapi lakuvunda halina ubani. Unaendelezaje michezo kama hujali miundombinu ya michezo?
 
Taifa stars walipocheza na Moroco wimbo wa Taifa haukuimbwa kwa wakati muafaka,Rais wa TFF bwana Tenga kwa aibu akamtoa kafara msemaji wa wakatio huo FLORIAN KAIJAGE,waziri anayehusika kama kawaida ktk nchi ya wajinga akasema hajui chochote,leo sijui TENGA atasemaje maana KAIJAGE kama angekuwa kihelehele tungemsikia akisema mnaona watanzania,ni majungu na ujuha wa TFF!!Waziri anayehusika ameona hili tena SUPER SPORT WAMEJARIBU KUMVUA CHUPI HADHARANI.Mwisho niseme tu nimekasirika na hili tukio la leo laiti ningekuwa na BUNDUKI ningeshuti.
 
What is wrong with my beautiful black color? How come we don't seem to get anything right?
 
Wala tusiwalaumu Tanesco, lawama zote ziende kwa uongozi wa CCM chama tawala wao ndo leta sera mbovu hafai kuwa madarakani tena, watz haya masuala tusipokuwa makini hatutafika jamaa mwenyewe ndo kwanza anacheka na hana habari kabisaaa


WanaJf wenzangu ni wazi kwamba kilichotokea leo uwanja wa taifa ni aibu kubwa na fedheha kwa nchi yetu!! Kitendo cha Tanesco kukata umeme kwenye tukio kubwa kama la leo tena linaloshuhudiwa na ulimwengu mzima kupitia DSTV tena fainali ya kombe la kagame inadhihirisha wazi kua Tanesco wamedhamiria kuiabisha serikali na viongozi wetu na katika tukio la leo nazidi kuwapa hongera ksbb wao wanaonekana kuishinda serikali!!! sasa tuone hatua zitachukuliwaje na nani atawajibishwaa hapa!?
 
Kazi kwa Ngeleja aibu yako hii na ndugu yako January makamba

Mmh! Hawa ni viongozi vijana walioshindwa kutoa ushauri/soln ya umeme; Mkubwa wao anazungumzia kunyesha mvua Mtera wao wanamuangalia, au tuseme wanashindwa kumuelewesha kwamba; kuna other sources za energy like solar, wind, coal etc. Kama vijana viongozi ndio hawa; Sijui kama tunahaja yukuangalia ujana kama kigezo cha kuwa raisi.
 
Wana Yanga tuna haki ya kushtaki na kudai fidia maana sherehe yetu imeharibiwa. Sasa habari ni kukatika kwa umeme taifa, wala si kwamba Yanga ndo bingwa Kagame Cup. Halafu tulitaka Rais Kagame ahudhurie fainaili!!
 
Aibu si kukatika umeme tu pale Uwanja wa taifa.
Huwezi amini,
Vyoo vya VIP hakuna system ya maji inayofanya kazi, na hakuna hata maji ya dharura kama vile kwenye ndoo na kopo kama tulivyozoea! Hakuna toilet paper, hakuna wahudumu wa vyooni wakati wa mechi. Ninachoshangaa ni kwamba, hawa viongozi wetu wanajisaidia bila kunawa waendapo pale taifa? Kama ni hivyo ndivyo basi wanatembea na mavi! Na yeyote mwenye kutembea na mavi hawezi kufikiria positive, atafikiria mavi yake yaliyomganda!
 
uwanja wa Tanzania hauna generetor? Au hawana pesa ya kununulia mafuta? Ni tsh ngapi tuwape?
 
Iyo ni mpaka arusha alaf walvyo mafala waliuleta saa 12 na madakka meng,iv hi ni hujuma ama ni kukomoana kwa kutomchagua MKUU
 
Poleni sana sana Watanzania wenzangu .Hii ni aibu kubwa mno .Hakika wacha tusikie JK na wenzake watasema nini .Mie huku hata matangazo sikusikia nani kafungwa jamani ?
 
kibaya zaidi mechi ilikuwa inaonekana nchi nyingi za afrika hii ni aibu ya karne. kikwete ndio anapaswa kuwajibika maana alituambia tusimlaumu ngereja. Leo kaijage hayupo sijui watamkaba koo muhando, ngoja tusubiri.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom