Taifa lisilo kuwa na Umeme wa uhakika ni Taifa liloamua kuwa masikini

Lidafo

JF-Expert Member
Sep 26, 2019
551
747
Habari wanajamvi!
Kwa muda sasa tatizo la umeme linazidi kumea na hakuna matumaini ya huu mgao kuisha, Najaribu kujiuliza kama Mtanzania hivi serikali imeshindwa kabisa kumaliza tatizo la mgao wa umeme?

Sina haja ya kuelezea Faida za nishati hii muhumu kwa maendeleo ya nchi hilo kila mtu anafahamu sasa kama tutashindwa kudhibiti uzalishaji wa umeme ambao ndio nishati muhimu katika kukuza uchumi vipi tutaweza kukua Kiuchumi wakati umeme wenyewe tu umetushinda?

Itoshe kusema tu taifa ambalo limeshindwa kuwa na umeme wa uhakika ni taifa ambalo limeamua kuung`ang`ania umaskinini na kuukumbatia kabisa na halina future ya kujikomboa kama taifa, Bali maendeleo yatabaki kwa mtu binafsi ila sio kama taifa.

Wakati tatizo hili limeanza zilitoka kauli za Kisiasa kuwa shida maji machache sasa hivi mvua ni za kutosha mbona bado shida ipo?

Miradi kila siku haiishi sasa kwa hali ilivyo watu wakisema kwamba kuna upigaji na biashara zinaendelea nyuma ya huu mgao na serikali imeshindwa kuwadhibiti watakuwa wanakosea?

Kwasabu serikali imewapa watu sababu ya kusema ili tuache kusema udhaifu huu serikali itufanyie jambo moja tu.. UMEME UWE WA UHAKIKA!

Miaka michache nyuma at least umeme ulikuwa wa uhakika na bei za kuusambaza zilikuwa nafuu sana lakini miaka michache mbele Umeme ukawa ni wa kuungaunga na bei za usambazaji kuongezeka yaani tunafanya kazi ya kupiga hatua 7 mbele alafu tunarudi hatua 14 nyuma what a shame!

Vinginevyo tatizo hili la umeme huenda lipo Kisiasa Zaidi yaani Create the problem then solve it, To gain popularity and truth from society ukizingatia tunaelekea 2025 au kuna watu wanaihujumu serikali ya awamu hii ili iwonekane ni mbovu mbele ya raia ukizingatia tunaelekea 2025 au Ni upigaji ambao hata wakubwa huko juu wanafaidika nao na wameamua kutupuuza wananchi au yote kwa pamoja yanawezekana.

Mwisho ni seme kuwa Kuachia tatizo lizidi kuwa kubwa ni kutengeneza chuki kwa jamii dhidi ya serikali yao na itafika kipindi hakuna atakaeweza kuvumilia tena.
 
Twiga yupo kazini

OIG3.QISWYcLuJJlkIdwh.jpeg
 
Mlisema January makamba ndio tatizo
Sasa hayupo kwenye umeme tatizo bado lipo
Tatizo la umeme halisababishwi na mtu mmoja mkuu, Kuna kikundi cha watu ambacho inahitaji ujasiri kukivunja chote, In short ni chain kubwa kwenye wizara kubwa kama ya nishati na shirika kubwa kama TANESCO ni ngumu kwa mtu mmoja kufanya hujuma hivyo ni chain flan hivi ambayo hata ukimuondoa mmoja wengine wanaendeleza hujuma
 
Kinyerezi phase 1,2,3+JNHP itatosha kabisa kumaliza tatizo la umeme.shida itakayobaki ni hujuma.
Hata hilo bwawa halitasaidia maana linategemea mvua

Siamini kama bwawa la "stigler gorge" litamaliza tatizo la mgao wa umeme nchini
 
Habari wanajamvi!
Kwa muda sasa tatizo la umeme linazidi kumea na hakuna matumaini ya huu mgao kuisha, Najaribu kujiuliza kama Mtanzania hivi serikali imeshindwa kabisa kumaliza tatizo la mgao wa umeme?

Sina haja ya kuelezea Faida za nishati hii muhumu kwa maendeleo ya nchi hilo kila mtu anafahamu sasa kama tutashindwa kudhibiti uzalishaji wa umeme ambao ndio nishati muhimu katika kukuza uchumi vipi tutaweza kukua Kiuchumi wakati umeme wenyewe tu umetushinda?

Itoshe kusema tu taifa ambalo limeshindwa kuwa na umeme wa uhakika ni taifa ambalo limeamua kuung`ang`ania umaskinini na kuukumbatia kabisa na halina future ya kujikomboa kama taifa, Bali maendeleo yatabaki kwa mtu binafsi ila sio kama taifa.

Wakati tatizo hili limeanza zilitoka kauli za Kisiasa kuwa shida maji machache sasa hivi mvua ni za kutosha mbona bado shida ipo?

Miradi kila siku haiishi sasa kwa hali ilivyo watu wakisema kwamba kuna upigaji na biashara zinaendelea nyuma ya huu mgao na serikali imeshindwa kuwadhibiti watakuwa wanakosea?

Kwasabu serikali imewapa watu sababu ya kusema ili tuache kusema udhaifu huu serikali itufanyie jambo moja tu.. UMEME UWE WA UHAKIKA!

Miaka michache nyuma at least umeme ulikuwa wa uhakika na bei za kuusambaza zilikuwa nafuu sana lakini miaka michache mbele Umeme ukawa ni wa kuungaunga na bei za usambazaji kuongezeka yaani tunafanya kazi ya kupiga hatua 7 mbele alafu tunarudi hatua 14 nyuma what a shame!

Vinginevyo tatizo hili la umeme huenda lipo Kisiasa Zaidi yaani Create the problem then solve it, To gain popularity and truth from society ukizingatia tunaelekea 2025 au kuna watu wanaihujumu serikali ya awamu hii ili iwonekane ni mbovu mbele ya raia ukizingatia tunaelekea 2025 au Ni upigaji ambao hata wakubwa huko juu wanafaidika nao na wameamua kutupuuza wananchi au yote kwa pamoja yanawezekana.

Mwisho ni seme kuwa Kuachia tatizo lizidi kuwa kubwa ni kutengeneza chuki kwa jamii dhidi ya serikali yao na itafika kipindi hakuna atakaeweza kuvumilia tena.

Siamini kama bwawa la "stigler gorge" litamaliza tatizo la mgao wa umeme nchini

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Hivi kijiji kama kina vibaka wengi na wanakijiji hawataki kuchukuwa hatua kuwaondoa unadhani wataisha? Tatizo la Tanzania ni wananchi! Wako wako tu wanakimbizana na mpira na wasanii. Hawataki kushinikiza viongozi kubadilika.
Mkuu hili la wananchi kutokuwa na uchungu ni kweli kabisa, Lakini litafika mwisho wake.
Tukumbuke kuwa jamii huwa na tabia ya kupitia transition mbalimbali tulikuwa kwenye kipindi cha ujinga mkubwa lakini kikapita sasa tupo kwenye ujinga wa wastani mambo kama kubet yamekuja kushika kasi sana itafika kipindi yatakuwa ya kawaida sana na jamii itakuwa busy na mambo mengine sasa serikali isiombe jamii iwe Bize na kuwawajibisha viongozi.
 
Nchi inakila kitu ila maskini Dah! Muwekezaji Gani awekeze kiwanda kikubwa mazingira haya. Priority mbovu!
Yaani inatia hasira sanaa vipaumbele vya serikali havieleweki.
Yaani unahamasisha vijana wajiajiri wakati umeme tu ni shida.
Haya raia kajikongoja na ka- saloon chake bado umeme umemkatia.
 
Na ndiyo maana mpaka leo kuanza kwa ile treni ya mwendokasi kunazidi tu kupigwa sarakasi.
Yaani ile Re-forming ya Rais Samia ilitakiwa ifanye kazi kwenye mambo ya muhimu kama haya in a positive way.
Lakini kwa hali ilivyo sasa ni kama nchi haina mwanga wala maono kila kitu tafrani.
 
Mkuu hili la wananchi kutokuwa na uchungu ni kweli kabisa, Lakini litafika mwisho wake.
Tukumbuke kuwa jamii huwa na tabia ya kupitia transition mbalimbali tulikuwa kwenye kipindi cha ujinga mkubwa lakini kikapita sasa tupo kwenye ujinga wa wastani mambo kama kubet yamekuja kushika kasi sana itafika kipindi yatakuwa ya kawaida sana na jamii itakuwa busy na mambo mengine sasa serikali isiombe jamii iwe Bize na kuwawajibisha viongozi.
Maneno yako ni kweli kabisa. Mkuu hata mimi nina uhakika mambo hayawezi kuwa namna hii siku zote. Ukiangalia idadi ya vijana wanaomaliza std 7, form 4 na 6, na vyuo ni kubwa sana. Huwa nasema watakavyofikia utu uzima itakuwaje!
 
Back
Top Bottom