Hiyo sababu ya kuahirisha uchaguzi wa ilemela ndiyo itakayowaumbua CCM na Mkurugenzi wao. Mkurugenzi kakubali kwamba Diwani Matata hana chama, basi ilikuwaje alimkubali Chagulani kushiriki kupiga kura? Kwa nini asitumie kigezo hicho hicho cha alichomkatalia Matata?
Ikumbukwe kwamba katika chaguzi sifa zote mbili lazima zizingatiwe - sifa ya kupiga kura na sifa ya kupigiwa kura. Huwezi kuikubali moja na nyingine ukaikataa.
Lakini wataalamu wa sheria wafafanue hili, na naomba wachangiaji wajikite katika subject hii tu.
Nawasilisha.
Yes, wachangiaji wajikite katika point hhi. Kuna ukinzani mkubwa wa maamuzi ya Mkurugenzi hapa.
Huyo diwani aliehamishwa toka tar 14, je sheria zinaruhusu diwani viti maalumu kuhama toka kata moja kwenda nyinine,? Na kama hairuhusiwi kwa nini chadema wakubali kushiriki uchaguzi wenye mamluki.? Na huyo diwani wa mahakama ni haki yake kupeleka kura upande wowote ule maana yuko huru hivyo ni makosa kuhusisha na kushindwa kwa chadema....ni ajabu nyingine kwa chadema kuungana na cuf kwenye umeya wakati bungeni waliwakatalia kuunda kambi moja rasmi ya upinzani.. Hivyo kutegemea kura za cuf ilikua sawa na kucheza kamali..kwa kukubali kufukuza madiwani ambao ndio kura zako rasmi ilikua sawa na kukubali kupoteza kiti cha umeya.!
Usikurupuke kuuliza maswali kwa jabza...Hebu soma vizuri ndo utaijua hiyo hesabu ikoje mkuuHebu weka hesabu zako sawa aisee , umesema nyamagana ccm walikuwa 7, then wakahamisha viti maalum 1 kutoka ilemela kuja nyamagana, kwa maana hiyo jumla Yao hapa ni 8, ww hiyo hesabu ya 9 umenipata wapi, au hesabu ya mchina hiyo? Fafanua
mkuu huo ukinzani wa sheria chadema hawakuuona kabla ya kushiriki uchaguzi.??
Haya nenda chooni ukapunguze hilo zigo...Nilikuwa nasubiria kwa hamu tangia asubuhi post za wana cdm kuanza kujitetea baada yakupigwa dafrau hili la uchaguzi wa ccm , sasa ndio zinakuja. Na nashangaa mleta mada hii hajui kuwa meya ni wa Jiji la mwanza, ilemela ni manispaa itachagua mwenyekiti wa manispaa na sio meya. Cdm kubalini kushindwa uchemfu mmeufanya wenyewe na maamuzi ya kamati kuu yasiyo zingatia maslahi ya wana mwanza kwa kuwafukuza madiwani walio chaguliwa na wananchi, madhara yame mmeyaona.
CCM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!
Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 ,
SOURCE: Kamnada Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema
Lol! CCM uharamia kila mahali! jamani CCM hivi hamwezi kabisa kugombea bila haya mambo yenu ya kisanii tu, kwa kuwa mna nguvu za dola?
Katika Katiba mpya tunatala mameya na wenyeviti wa halmashauri wachaguliwe na wapiga kura direct, na siyo madiwani wachache ambao ni rahisi kwa maharamia wa CCM kuwaghilibu kwa pesa.
Soirry, huijui Chadema inasimamia nini! yaani madiwani mafisadi waachiwe tu eti kwa sababu itakosesha CDM umeya? Hayo mambo yenu ya CCM mkae nayo nyie wenyewe -- yaani mambo ya kulea mafisadi. na ndiyo maana mnaporomoka kwa kasi katika umma.
Una-mix madesa mkuu.
CCM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!