Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza...

Duuuu cdm mshaniharibia week end yangu...naianza vibayaaaaaa, dawa ni kumlimboka tu huyo mkurugenzi wa mza! Hivi viongozi wetu mlipowatimua hao madiwani hamkujua kuna uchaguzi wa umeya?
 
Hiyo sababu ya kuahirisha uchaguzi wa ilemela ndiyo itakayowaumbua CCM na Mkurugenzi wao. Mkurugenzi kakubali kwamba Diwani Matata hana chama, basi ilikuwaje alimkubali Chagulani kushiriki kupiga kura? Kwa nini asitumie kigezo hicho hicho cha alichomkatalia Matata?

Ikumbukwe kwamba katika chaguzi sifa zote mbili lazima zizingatiwe - sifa ya kupiga kura na sifa ya kupigiwa kura. Huwezi kuikubali moja na nyingine ukaikataa.

Lakini wataalamu wa sheria wafafanue hili, na naomba wachangiaji wajikite katika subject hii tu.


Nawasilisha.

Yes, wachangiaji wajikite katika point hhi. Kuna ukinzani mkubwa wa maamuzi ya Mkurugenzi hapa.
 
Huyo diwani aliehamishwa toka tar 14, je sheria zinaruhusu diwani viti maalumu kuhama toka kata moja kwenda nyinine,? Na kama hairuhusiwi kwa nini chadema wakubali kushiriki uchaguzi wenye mamluki.? Na huyo diwani wa mahakama ni haki yake kupeleka kura upande wowote ule maana yuko huru hivyo ni makosa kuhusisha na kushindwa kwa chadema....ni ajabu nyingine kwa chadema kuungana na cuf kwenye umeya wakati bungeni waliwakatalia kuunda kambi moja rasmi ya upinzani.. Hivyo kutegemea kura za cuf ilikua sawa na kucheza kamali..kwa kukubali kufukuza madiwani ambao ndio kura zako rasmi ilikua sawa na kukubali kupoteza kiti cha umeya.!
 
Huyo diwani aliehamishwa toka tar 14, je sheria zinaruhusu diwani viti maalumu kuhama toka kata moja kwenda nyinine,? Na kama hairuhusiwi kwa nini chadema wakubali kushiriki uchaguzi wenye mamluki.? Na huyo diwani wa mahakama ni haki yake kupeleka kura upande wowote ule maana yuko huru hivyo ni makosa kuhusisha na kushindwa kwa chadema....ni ajabu nyingine kwa chadema kuungana na cuf kwenye umeya wakati bungeni waliwakatalia kuunda kambi moja rasmi ya upinzani.. Hivyo kutegemea kura za cuf ilikua sawa na kucheza kamali..kwa kukubali kufukuza madiwani ambao ndio kura zako rasmi ilikua sawa na kukubali kupoteza kiti cha umeya.!

Soirry, huijui Chadema inasimamia nini! yaani madiwani mafisadi waachiwe tu eti kwa sababu itakosesha CDM umeya? Hayo mambo yenu ya CCM mkae nayo nyie wenyewe -- yaani mambo ya kulea mafisadi. na ndiyo maana mnaporomoka kwa kasi katika umma.
 
Hebu weka hesabu zako sawa aisee , umesema nyamagana ccm walikuwa 7, then wakahamisha viti maalum 1 kutoka ilemela kuja nyamagana, kwa maana hiyo jumla Yao hapa ni 8, ww hiyo hesabu ya 9 umenipata wapi, au hesabu ya mchina hiyo? Fafanua
Usikurupuke kuuliza maswali kwa jabza...Hebu soma vizuri ndo utaijua hiyo hesabu ikoje mkuu
 
mkuu huo ukinzani wa sheria chadema hawakuuona kabla ya kushiriki uchaguzi.??

CDM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!
 
Nilikuwa nasubiria kwa hamu tangia asubuhi post za wana cdm kuanza kujitetea baada yakupigwa dafrau hili la uchaguzi wa ccm , sasa ndio zinakuja. Na nashangaa mleta mada hii hajui kuwa meya ni wa Jiji la mwanza, ilemela ni manispaa itachagua mwenyekiti wa manispaa na sio meya. Cdm kubalini kushindwa uchemfu mmeufanya wenyewe na maamuzi ya kamati kuu yasiyo zingatia maslahi ya wana mwanza kwa kuwafukuza madiwani walio chaguliwa na wananchi, madhara yame mmeyaona.
Haya nenda chooni ukapunguze hilo zigo...
 

CCM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!

Umemjibu vizuri kabisa! Kwa mfanio unapodai malipo fulani, unaweza kupokea kile utakachopewa halafu unaenda mahakamani iwapo hujaridhika! CCM mnashangaza kweli kweli.
 
Yanamwisho haya!Nani alitegemea uelewa huu wawatanzania tena kwahara namna hii japo sio wote!Nakwambia wanasiasa wajipange vizuri kisera nautekelezaji 2015!Kama wanabisha wajikumbushe zomezomea yahapa karibuni mkoa huohuo!!
 
Kidogo nimefunguka! Ila kuna kitu bado kinanitatiza sana!
Na ngoja ntarudi baadae na nitasema tu!
Kwani hili la ccm sasa inanitatiza sana!
 
hata hivyo ccm wangeshinda. sababu ccm walitakiwa wawe na kula 10 dhidi ya 9 wa chadema. je huyo diwani wa Ilemela asingekuja chadema wangeshinda?. bila shaka wangelingana kura ambapo mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi ingemlazimu kupiga kura na angeipigia ccm bila shaka. Tukubali tu kwamba chadema tumeshindwa. Tujipange upya kimafia zaidi. mia
 

Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 ,
SOURCE: Kamnada Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema

Nifafanulie hapa mkuu,
Ilemela na Nyamagana zote ziko ndani ya Mwanza,
So any movement within these districts will not affect the entire total number of madiwani within Mwanza, au ikoje hii?
Mtu akitoka ilemela akahamia Nyamagana itaathiri vipi jumla ya madiwani wa Mwanza?
Ufafanuzi please!!
 
Naomba kuuliza jamani ikiwa Chama Kinakuwa na Madiwani wengi lakini Umeya umechukuliwa na chama chenye madiwani wachache je hicho chama kilichochukua umeya kinanufaika na nini wakati inawezekana katika maamuzi kikapata pingamizi kutoka upande wa pili?
 
Lol! CCM uharamia kila mahali! jamani CCM hivi hamwezi kabisa kugombea bila haya mambo yenu ya kisanii tu, kwa kuwa mna nguvu za dola?

Katika Katiba mpya tunatala mameya na wenyeviti wa halmashauri wachaguliwe na wapiga kura direct, na siyo madiwani wachache ambao ni rahisi kwa maharamia wa CCM kuwaghilibu kwa pesa.

Duh! na hilo likitokea sijui CCM wataambulia mameya na wenyeviti wangapi. Labda nape aweza kutupa mwanga!
 
Soirry, huijui Chadema inasimamia nini! yaani madiwani mafisadi waachiwe tu eti kwa sababu itakosesha CDM umeya? Hayo mambo yenu ya CCM mkae nayo nyie wenyewe -- yaani mambo ya kulea mafisadi. na ndiyo maana mnaporomoka kwa kasi katika umma.

sasa kama chadema wanakuza demokrasia, kwa nini mlalamike kushindwa wakati baadhi ya kura mmejipunguzia wenyewe kwa kutimua madiwani....mimi naamini sababu ilikua moja tu... "Chadema tumeshindwa uchaguzi sababu ya mgogoro na baadhi ya madiwani wetu" hizo zingine mbwembwe tu.
 

CCM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!
Una-mix madesa mkuu.
CCM au CDM?
Mwanzo umeanza vibaya, but ukamalizia poa.
 
Nimejiuliza hili swali sina majibu ya uhakika.
CUF na CCM wamekuwa na Umoja usioelezeka kwenye masuala mbalimbali ya Utawala wa Taifa hili. Kimsingi maamuzi yao yamekuwa yakiwa kwenye Jihad kuu ya kupingana na CHADEMA kwa nguvu zote.
Sera za CHADEMA ziko tofauti sana na CUF na CCM. Kitendo cha Vyama hivi viwili CUF na CCM kuungana kwenye Maamuzi Muhimu ya kitaifa inaonyesha mkanganyiko mkubwa kwenye Demokrasia. Haijulikani bado kama CUF ni chama cha Upinzani au ni Chama Dada cha CCM. CUF imeungana na CCM kuipiga vita CHADEMA popote nwenye ngazi mbali mbali.

Nimejiuliza hivi haya wanayofanya ni kwa faida za nani?.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom