Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Huyo Mkurugenzi mbona ni mtu wa ajabu. Yaani anakubali moja kwa moja haki ya Diwani Chagulani kupiga kura (baada ya kurudishiwa udiwani na mahakama, lakini hapo hapo akakwama katika kumruhusu Diwani Matata kugombea, kwa kuwa hakuteuliwa na chama (Chadema). Kama ni hivyo basi hata yule Chagulani hakuwa na haki ya kuruhusiwa kupiga kura, kwani alirudi katika udiwani kwa nguvu ya mahakama, na si ya Chama (Chadema).
Naona mawakili wa Chadema wanaaonza kusafisha bongo zao na kupeleka mahakamani suala la uchaguzi huo wa kihuni. Mimi nadhani haki lazima itafutwe mahakamni, maana CCM imezidi mno na umafia katika chaguzi hizi.