Maandalizi ya maandamano ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mkoani Mwanza yamefikia asilimia 90 huku miongoni mwa waliothibitisha kushiriki ni mwanasiasa mkongwe, Dk Wilbrod Slaa.
Taarifa hiyo imetolewa jana Jumanne Februari 13, 2024 na Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad, wakati viongozi wa kamati ya maandalizi ya maandamano hayo walipotembelea na kukagua uwanja wa Furahisha wilayani Ilemela jijini hapa, yanapotarajiwa kuhitimishwa.
Dk Slaa alipozungumza na Mwananchi Digital lililotaka kujua kama kweli atashiriki maandamano hayo amesema, “ni kweli nitashiriki na nitakuwepo.”
Katibu wa Chadema Kanda ya Victoria, Zacharia Obad amesema “Tutatumia maandamano hayo kuomboleza kifo cha (Edward) Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama na kiongozi ndani ya chama chetu, pia alikuwa kiongozi wa umma alipokuwa Waziri Mkuu nchini,” amesema Obad.
Amewataka wafuasi wa Chadema na wasiokuwa wafuasi kujitokeza kwa wingi kushinikiza matakwa hayo mawili ambayo ni ugumu wa maisha na Serikali kusikiliza maoni ya wananchi kuhusu miswada mitatu ya Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na ya vyama vya siasa iliyokwisha pitishwa na Bunge.
Source - Mwananchi