ni wakati wa kubadilisha huu utaratibu wa kumpata meya kutoka huu mfumo wa kupigiwa kura na madiwani, iwe meya achaguliwe na wananchi sababu mfumo wa sasa umeweka maslahi ya chama mbele, pia huu mfumo si wa kidemokrasia kwasababu diwani analazimika kumpigia mtu wa chama chake hata kama ni mbovu
Nimejiuliza hili swali sina majibu ya uhakika.
CUF na CCM wamekuwa na Umoja usioelezeka kwenye masuala mbalimbali ya Utawala wa Taifa hili. Kimsingi maamuzi yao yamekuwa yakiwa kwenye Jihad kuu ya kupingana na CHADEMA kwa nguvu zote.
Sera za CHADEMA ziko tofauti sana na CUF na CCM. Kitendo cha Vyama hivi viwili CUF na CCM kuungana kwenye Maamuzi Muhimu ya kitaifa inaonyesha mkanganyiko mkubwa kwenye Demokrasia. Haijulikani bado kama CUF ni chama cha Upinzani au ni Chama Dada cha CCM. CUF imeungana na CCM kuipiga vita CHADEMA popote nwenye ngazi mbali mbali.
Nimejiuliza hivi haya wanayofanya ni kwa faida za nani?.
CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa amabzo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratiu zikoje.
Baada ya mgawanyo wa h/shauri ya jiji na kuwa na h/shauri ya jiji inayoundwa na jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la ilemela mwezi Julai mwaka huu mgawanyo wa madiwai ulikuwa hivi kwa nyamagana
Chadema -wa kata 5, viti ,maalum 2. mbunge mmoja, jumla wanakuwa 8
CCM - wa kata 6, viti maalum 1 jumla wanakuwa 7
Cuf - wa kata 1, viti maalum 1
Ilemela
Chadema -- wak kata 6, viti maalum 2 mbunge 1 jumla wanakuwa 9
CCM - wa kata 3, viti maalum 2 na mbunge 1 (wa viti maalum) jumla wanakuwa 6
CUF - MBUNGE WA viti maalum 1
Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 , aliyepungua Chadema akiwapigia CCM wanakuwa na kura 10 dhid ya 7 za Chadema.
Lakini pia CUF walishakubaliana na chadema kuungana mkono, kwa hiyo kwa kura 2 za CUF Chadema wangekuwa na kura 9, lakini inaonekana ama mwana Chadema mmoja kapigia CCM au CUF mmoja kapigia CCM na kufanya matokeo ya kuwa kuwa 11 kwa CCM dhidi ya nane za Chadema.
Hiyo ndiyo hali halisi ya jinsi mahesau ya kura yalivyochezwa, kama kuna uhalali katika mchakato huo au la ni suala la wataalamu wa masuala haya kutujuza.
Hayo yakiendelea uchaguzi wa Meya wa Ilemela meahirshwa katika mazingira tata, baada ya Mkurugeni kusoma Amri ya Mahakama iliyopewa tafsiri na mwanasheria wa jiji kuwa inakifanya kikao hicho kuahirishwa kwa kuwa Diwani wa Chadema Matata (pia alifukuzwa uanachama pamoja na wa igoma na anaendelea na udiwani kwa amri ya makahama) kuleta pia barua ya kutaka atambuliwe kaa mgombea.
Ukazuka ubishi kidogo juu ya hoja ya mgombea kuteuliwa na chama, mkurugenzi wa jiji akasema hiyo siyo sheria ni mwogozo, na kwa kuwa sheria na mwongozo zikigongana sheria ndiyo inatamalaki hatakia aingie katka mgogoro wa tafsiri ya sheria, akaahirisha kikao bila hata madiwani kujadili hoja hiyo.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa wa Chadema, pingamizi hilo lilikuwa linawarejeshea haki yao ya uanachama na hivyo kuendelea na udiwani wao, na kutaka matata asizuiliwe kuendelea na mchakato wa kuomba umeya, Kwa hiyo matata ameomba lakini hakuteuliwa na chama na mahakama haiwezi kuwalazmisha chama wateue mgombea kwa amri ya mahakama, anadhani ni uhuni tu na njama za kisiasa zimefanyika kuahirisha uchaguzi huo.
Nadhani kidogo piacha itaeleweka kwa wanjamvi juu ya nini hasa kimetokea.
SOURCE: Kamnada Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema
mkuu uko sawa kabisa. Tukubali kabisa kushindwa kwa chadema asilimia kubwa kunachangiwa na chedema wenyewe... Wakati ccm walienda kwa hesabu sisi tulienda kwa huruma kutoka cuf na kwa bahati itokee ccm.!
kinachonifurahisha cdm ni kuwa wewe km umechaguliwa kuwa kiongozi wa watu halafu unaleta mambo yanayokwenda kinyume na maadili ya chama, unapumzishwa. hiyo ndo nidhamu ya chama.
inatujengea uzoefu wa kutovumilia makosa ya mtu once tumechukua nchi uchaguzi ujao. hizi ni challenges na vyama makini vilivyojipanga kuchukua nchi, hukutana na vitu km hivi.
hii ndio tabu ya kumchukia mtu badala ya mfumo mtaendelea kuumia sana subirini 2015, kikwete anapita tu akija mnayempenda mtarudi CCM.
Mazingira ya wazi,ikiwa na maana kwamba kuna uwezekano wa kufahamu ni diwani yupi wa chadema(kama ni kweli) alimpigia mgombea wa ccm.mkuu nisaidie kura za wazi zinapigwa kwenye mazigira gani.?
kinachonifurahisha cdm ni kuwa wewe km umechaguliwa kuwa kiongozi wa watu halafu unaleta mambo yanayokwenda kinyume na maadili ya chama, unapumzishwa. hiyo ndo nidhamu ya chama.
inatujengea uzoefu wa kutovumilia makosa ya mtu once tumechukua nchi uchaguzi ujao. hizi ni challenges na vyama makini vilivyojipanga kuchukua nchi, hukutana na vitu km hivi.
wewe jamaa mbona mjinga sana?
Ujerumani kuna serikali ya mseto, uingereza kuna serikali ya mseto, israel kuna serikali ya mseto, ugiriki kuna serikali ya mseto, lebanon kuna serikali ya mseto, kenya na zimbabwe pia. Sasa unaona ajabu cuf na ccm kuunda serikali zanzibar?
Hebu wacha ushamba huo usikae vichakani kula panzi tu njoo utembee zanzibar uone watu walivyostaarabika ili upunguze fikra potofu.
Punguza ubinafsi, choyo na chuki na utambue tu kua ni sisi wananchi wa zanzibar kupitia njia ya kidemokrasi 64.3% tulipiga kura ya kukubali mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa. Na hata chadema kama wana ubavu wa kupata alau jimbo moja zanzibar nanyi mutashirikishwa. Lkn kwa sasa musitegemee huruma bila ya kufanya kazi.
hii ndio tabu ya kumchukia mtu badala ya mfumo mtaendelea kuumia sana subirini 2015, kikwete anapita tu akija mnayempenda mtarudi CCM.
Wewe ndi mshamba umekalia uzanziari wenu huko na Jussa wenu aliyewahi kusema mlipoteza jimbo kwa ajili lilikuwa na wakristo wengi
Acha sias zetu wabara tuzijadili huku huku bara nyie endeleeni na fungate salama