Arusha mjini CCM twende na nani kwenye ubunge 2025?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,303
2025 iko pale kwenye kona je, wapiga kura wa Arusha mjini tumeshatafakari wa kwenda naye kwenye uchaguzi dhidi ya Godbless Lema. Huko CHADEMA inajulikana kuwa ni mgombea wao wa ubunge ni Lema. Mchakato wao wa kumpata mgombea ubunge huwa ni kiini macho tu. Tayari mgombea wao ni Lema na hata yeye kashathibitisha. Sisi CCM tunafuata sana katiba ya chama chetu kinavyotaka ndo maana hadi muda huu mgombea ubunge hajajulikana.

Mwaka 2020 kwenye kura za maoni walikwepo kina Mrisho Gambo, Philemon Mollel (Monaban) na Alberto Msando. Kwa hali ya kisiasa ilivyo hadi muda huu Gambo na Msando wako active kabisa kwenye siasa. Mbunge viti maalum Catherine Magige naye hayuko nyuma huku Meya wa Jiji Maxmillian naye akizidi kuchanja mbuga. Binafsi nitatoa ushirikiano kwa mgombea yeyote isipokuwa Gambo.
 
Back
Top Bottom