Hivi jimbo la Nyamagana jijini Mwanza lina mbunge kweli. Wakazi wa Kishiri wanateseka mno na barabara yao Mbovu sanaa

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Mar 8, 2019
366
1,376
Nchi hii ya Tanzania baada ya uchaguzi wa mwaka 2020 chini ya mwendazake majimbo yote yalikua chini ya CCM likiwemo hili la Nyamagana chini ya uongozi wa Stanslaus Mabula.

Huyu mbunge sijui kama yupo hapa Mwanza. Barabara nyingi za jimbo lake hasa maeneo ya pembeni ambayo kimsingi ndio yana watu wengi na wapiga kura wengi ni mbovu vibaya mno.

Barabara ya kutoka IGOMA kwenda KISHIRI inatia kichefuchefu kwa kweli.

Barabara ni mbovu, mashimo mwanzo mwisho. Utembee kwa daladala kero, bajaji kero, private car kero na kuna mbunge analipwa zaidi ya milioni 12 kwa mwezi na kuna mfuko wa jimbo.

Kishiri wamesahaulika na huyu Mabula na CCM yake. Na jinsi viongozi wa CCM walivyo wanafiki watajifanya wanachonga barabara na kuwajali wananchi miaka hii ya uchaguzi 2024/2025.

Mbunge na CCM yako mjitafakari barabara ya Kishiri mbovu mno ichongwe na kumwaga hata kifusi huku wanaishi wapiga kura wenu wengi tu na sisi wafanya biashara tunaitumia hii barabara ila imekua kero kwetu.

Mwananchi hapa wa Ilemela- Buswelu kwa Angelina Mabula.
 
Kwenye hiyo barabara sasa hivi Kuna mkandarasi Mchina anajenga barabara kutoka Buhongwa hadi Igoma kwa kiwango cha lami.

Na ikifika Kishiri itagawanyika njia mbili. Moja itapita njia ya sasa ya Kishiri kwenda Igoma na nyingine itatoka Kishiri kupitia jirani na Shule ya Sekondari Igoma kwenda Sabasaba hadi kukutana na Barabara ya Musoma maeneo ya Nyamhongolo.

Barabara itakuwa two -way na taa zaidi ya 470! Pia Mh. Stanslas (sio Stanslaus) Mabula amewajengea watoto wa Kishiri na Bujingwa Shule ya Sekondari ya kisasa kabisa na ambayo itafunguliwa mapema mwezi ujao. Tumpe maua yake Mh. Mbunge wetu MH. STANSLAS MABULA!👏👏👏👏!!!!
 
Back
Top Bottom