UDSM kimenuka sasa hivi, Kikwete na Kawambwa Wataficha wapi nyuso zao?

pesa na kufanya dhifa ya taifa na mashoga wanayo

Hebu tuondolee ujinga hapa na elimu yako ya Malampaka. Wewe unadhani hata hyo dhifa isingekuwepo hiyo hela ndo ingepelekwa huko UDSM? Mbona unashindwa kutofautisha majukumu ya taasisi za utawala? Kwa hiyo kesho utasema hata chai inayonywewa Ikulu wangepewa wanafunzi. Matatizo hayatatuliwi kwa njia isiyo endelevu na ya jazba kama yako!
 
Kwa kweli taifa limebaki jina kutokana na walio na madaraka kuendesha kama vile sisi ni wanyama, nataka kusema wananchi tuinuke na kuwa majasiri ktk kutetea haki na kukataa uongozi uliopo.Tumechoka kusikia vilio vya wanafuzi, walimu, madaktari, wafanyabiashara, wafanyakazi na wakukulima kwa ujumla wake.Mungu atusaidie
 
More updates wakuu....................niko hapa vijana wanatoa hoja kuwa kwanini wasipewe hela ilihali rais anazurura ulimwengu mzima kutoka anga moja mpaka nchi nyingine, inavyoonekana serikali haina majibu kabisa , naona wanausalama wanajaa hapa , HAKUNA HAKI NASEMA HAKUNA HAKI , HAO WANANIFATA NA MIMI NAPIGWA WAKUU, KIKWETE TOKAAAAAAAAAAAAAA, TUACHIE NCHI YETU TOKA

we jasiri. Unapost ndani ya kichapo. We jasiri
 
naikubali sana hiki chuo.
na siku zote nitakikubaliiiiiiiiiiiiiiiiiiii
zidumu imani za wana udsm wenye kujua kudai haki zao, salamu kwa wote wana udsm waliopita waliopo na watakoendelea kuwapo ikiwa watakuwa na imani ya namna hii.
 
Na hapo watasema ni CHADEMA? kwa matendo yao haya ndio yanayo jenga chuki kubwa kwa wanafunzi na vijana then wanasema eti CDM wanafanyiwa uchochezi kumbe serikali na chama chao ndio root ya kila kitu
 
aisee!!!!!!! fantastic avatra, lakini hebu turdi na nyuma, ivi ni mtu tu akijiskia kuongea kwa manufaa yake anaongea tuuuuu au ni mipango ya serikari, na kama ni ya serikari basi .com, hadi wanafunzi?!!! afu eti uwape wa mwaka wa kwanza unataka kupunguza wasomi ili nchi ui.com vzr! hiyo sera tumeistukia coz kwa nini umpe wa mwaka wa pili umnyime wa mwaka wa kwanza wakati siku zote mwazo ndio mgumu? au ndo ile msemo 'alienacho anaongezewa na asienacho ananyang'anywa hata na alichonacho?
 
Kuna washawasha check chini hapo ipo nyuma ya rev square inawasubilia

DSC06409.JPG
I can bet on my life wewe ni mtoto wa fisadi!
 
in the name of peace tunaonewa tunakandamizwa na tukitaka kuhoji, kudai, kuwawajibisha watu fulani,fulani tunaambiwa tutavuruga amani ujinga mtupu kama mabaya yasemwe yawekwe wazi serikali ikishindwa kuwawajibisha,kutekeleza ni jukumu letu kwa namna yoyote tunayoona inafaa kufanya tufanye.eti tushindwe kufanya mambo ya msingi kisa tutavuruga amani hii ni psychological lie watu wanapandikizwa tuamke watanzania
 
halafu sasa yamekuwa mambo ya kufurahisha wao wavuruge mambo watu wakireact wanasema chadema wamewatuma, wakati mwingine wala si chadema watu wamechoshwa na namna nchi inavyoendeshwa
hii ndio miaka 50 ya uhuru na vurugu ziwe zinasemwa kuwa zimeongezeka sio kutoa mafact ambayo mengine hayana hata uhalisia
 
Tayari mambo yamechafuka katika chuo kikuu cha Dar es salaam na mpaka muda huu vijana wako Revolution square na wametangaza mgomo kwa kile wanachodai ni kwa mwaka wa kwanza kunyimwa mikopo, sasa hii ni aibu, je JK na Kawambwa wataficha wapi nyuso zao?
kweli nimeamin udsm ni watetezi wetu. maana kuna watoto wa maskin kibao tumeshndwa kwnda chuo kisa uzembe wa viongozi; nataman ningekuwapo dsm ningeliunga japo mm nimepata sua. wanachuo wengne amkeni tudai haki zetu mcbaki kulalamika na kuomba wazasaidie tena kumbkeni wao walisomeshwa bureee. enyi mliopata mikopo msigeuke kuni ya akiba kuwahcheka waliokosa, kama hayajawakta nyie yatawkta watoto wenu. tuamke vyuo vyote tz
 
Hebu tuondolee ujinga hapa na elimu yako ya Malampaka. Wewe unadhani hata hyo dhifa isingekuwepo hiyo hela ndo ingepelekwa huko UDSM? Mbona unashindwa kutofautisha majukumu ya taasisi za utawala? Kwa hiyo kesho utasema hata chai inayonywewa Ikulu wangepewa wanafunzi. Matatizo hayatatuliwi kwa njia isiyo endelevu na ya jazba kama yako!

Kama nchi imefilisika kuna haja gani ya watu wengine kunywa chai ya serikali wakati watu wanakufa njaa. Wangetumia mishahara yao kujilisha ungeshangaa hata mialiko ya futari za mwezi wa Ramadhani usingeisikia.
 
halafu sasa yamekuwa mambo ya kufurahisha wao wavuruge mambo watu wakireact wanasema chadema wamewatuma, wakati mwingine wala si chadema watu wamechoshwa na namna nchi inavyoendeshwa
hii ndio miaka 50 ya uhuru na vurugu ziwe zinasemwa kuwa zimeongezeka sio kutoa mafact ambayo mengine hayana hata uhalisia

Usiseme mafact sema madata!
 
Back
Top Bottom