Ubora wa vyuo vikuu duniani: Oxford chaongoza duniani, Cape Town chaongoza bara la Afrika

Profesa anatoka katika chuo anasema Deni la Taifa sio mzigo kwa Taifa unategemea nini hapo...ni bora upate degree moja Stellenbosch kuliko phd za bongo ni sanaa tuu ilo mimi nalijua kitambo...
 
Chuo kikuu cha Dar ni sehemu ya uso wa Tanzania. Badala ya kutetea kwamba kiko sawa inabidi tujifunze toka Makerere na Nairobi ili tuimarishe UDSM.

A new approach is needed. Utawala mpya wa Rais Magufuli na Professor Ndalichako uangalie UDSM kwa umakini. It will not be enough to throw more money at the problem. We need to find out the root of the problem and work out a comprehensive solution.
 
Chuo kikuu cha Dar ni sehemu ya uso wa Tanzania. Badala ya kutetea kwamba kiko sawa inabidi tujifunze toka Makerere na Nairobi ili tuimarishe UDSM.

A new approach is needed. Utawala mpya wa Rais Magufuli na Professor Ndalichako uangalie UDSM kwa umakini. It will not be enough to throw more money at the problem. We need to find out the root of the problem and work out a comprehensive solution.
Tatizo mnapenda sana kusifiwa na kujisifia ilo ndio tatizo
 
CHUO kikongwe zaidi katika ulimwengu wa nchi zinazozungumza Kiingereza na kilichotoa viongozi mashuhuri nchini Uingereza cha Oxford, kwa mara ya kwanza kimeongoza katika orodha ya vyuo vikuu duniani, lakini Makamu Mkuu wa chuo hicho ameonya kwamba Brexit inaweza kuharibu mategemeo yake ya muda mrefu.

Chuo hicho cha Oxford kimepiku chuo kilichokuwa kikiongoza orodha hiyo kwa miaka mitano iliyopita, cha California Institute of Technology, ambacho kimeshika nafasi ya pili. Pia orodha hiyo imeshuhudia vyuo vikuu vya China vikipanda kwa haraka zaidi katika orodha hiyo ya vyuo vikuu bora duniani.

Oxford, walikosoma mawaziri wakuu wane kati ya sita waliopita wa nchi hiyo, kimepiku chuo cha Marekani baada ya bajeti yake ya utafiti kuongezeka kufikia paundi bilioni 1.4 ($1.83bn), wakati matokeo ya utafiti wake ukiongezeka, anasema Phil Baty, mhariri wa orodha hiyo.

Lakini Baty anasema kujitoa kwa Uingereza kutoka katika Jumuiya ya Ulaya “ni hatari kubwa kwa mafanikio yetu” kwa kufanya kuwa vigumu zaidi kuwavutia wanataaluma wa juu zaidi na kuwaweka katika miradi ya utafiti.

Brexit inahatari ya kuwaondoa wanafunzi, wafanyakazi na fedha, Makamu Mkuu wa Oxford, Profesa Louise Richardson, aliiambia redio ya BBC.

Richardson alisema kuwa vyuo vikuu vingine vimeongeza jitihada zake katika kuchukua asilimia 17 ya wafanyakazi wake ambao ni wananchi wa Jumuiya ya Ulaya, na ambao hadhi yao katika Uingereza haiwezi kuhakikiwa baada ya kura ya Juni 23.

“Vipo vyuo vikuu vingi duniani ambavyo vitafurahi kuwa nao na vimekuwa vikijaribu kuwafuata ili kuwachukua na kuwauliza kama wanaweza kujiunga na vyuo vyao badala ya kuendelea kubaki,” alisema.

Serikali pia imeshindwa kutoa uhakika kama itafidia kiasi cha paundi milioni 67 kwa mwaka ambazo chuo hicho kimekuwa kikipokea kutoka kwa Baraza la Utafiti la Ulaya ambazo hutumika kufanya kazi za utafiti, alisema.

“Kusema ukweli, tuna wasiwasi juu ya hilo.”

Wakati Oxford, University of Cambridge na London’s Imperial College vya Uingereza vikiwa ndani ya vyuo kumi bora duniani pamoja na chuo kikuu cha ETH Zurich, orodha hiyo imetawaliwa na vyuo vikuu vya kutoka nchini Marekani.

Chuo Kikuu cha Stanford cha Marekani kimeshika nafasi ya tatu, wakati Massachusetts Institute of Technology, MIT kikishika nafasi ya tano, Havard nafasi ya sita, Princeton saba na Chuo Kikuu cha California, Berkeley na Chuo Kikuu cha Chicago vikifungana katika nafasi ya kumi. Vyote hivi vinatokea nchini Marekani.

Cambridge cha Uingereza kimeshika nafasi ya nne, wakati Imperial College kikiwa cha nane na ETH Zurich nafasi ya 9.

Chuo Kikuu cha St. Andrews cha Scotland na Chuo Kikuu cha Sheffield vimeporomoka kutoka vyuo vikuu 100 bora duniani.

Katika Ulaya, nchi za Ujerumani na Uholanzi zimeshika nafasi ya tatu na nne, ambapo Ujerumani ina vyo vipatavyo 41 katika vyo vikuu 200 bora na Uholanzi ikiwa na vyuo vikuu 13 katika orodha hiyo.

Nchi za Ulaya Kusini kama Hispania na Italia hazijafanya vizuri kutokana na uhaba wa fedha na matatizo katika kuwapata wafanyakazi bora, Baty alisema.
Kwa upana zaidi, orodha inaonyesha taasisi katika bara ya Asia zimepiga hatua, kukiwa na vyuo viwili kutoka barani humo – Chinese University of Hong Kong na Korea Advanced Intitute of Science and Technology – vikiwa ndani ya vyuo 100 bora na vingine vinne vikiingia katika vyuo bora 200.

Peking University kimepanda hadi nafasi ya 29 kutoka 42, na Tsinghua kikishika nafasi ya 35, kutoka nafasi ya 47 ya mwaka 2015.

Vyuo vya Asia vinapanda, alisema Baty, wakati serikali ya China ikiingiza mabilioni ya dola katika vyuo vyake wakati huo huo, nchi za magharibi zikikabiliwa na uhaba ya bajeti.


Chanzo:
Raia Mwema
 
natofautiana sana na Mzee LOWASA lakini kwenye maono yake ya elimu kuhusu taifa hili nampongeza sana. kama juzi alisema wazi yeye angeanza na walimu
Kwanini asisitize kuanza na walimu wakati jpm yeye kaanza na madawati na sizani kama anawaza maslahi bora ya Mwl
kwa nn nchi inashindwa kuwa angalia walimu sababu elimu bora inaanzia chini hapo ndo tutaweza kudumu
Elimu si suala la kuwa bure au kulipiwa. Elimu inahitaji investment...
 
Ungekuwa una elimunzuri ungefahamu kuwa orodha ya vyou vikuu bora duniani hutolewa na taasisi nyingi tu sio hao 'times' peke yao. Kabla hujafikia conclusion ungetafuta orodha ya taasisi nyingine pia na pengine ungetambua vigezo vyao ni vipi. Usiwe kama wengine wanasema eti wahitimu hawajui kiingereza. Kuna wataalamu huko Japan hata maneno kumi ya kiingereza hana lakini hatari hao, usipime.Kufikiri na kufanya 'analysis' kuna hitaji weledi na sio papara kama hivi. Harvard, Stanford na Yale nivya ngapi katika hiyo list yenu?
Wewe ndio huenda huelewi, leave those others, kwanini katika rating ya times tusiwepo? Usiwe diehard , kubali madhaifu ili ujirekebishe,
Halafu sidhani kama wewe ni msomi unaefananisha graduate wa udsm aliesomea kwa kingereza toka form one akasoma chuo ambapo language of instruction ni English na mtaalam wa Japan ambaye hajawahi soma kwa kingereza hata hatua moja katika elimu yake,
Jiongeze mkuu!
 
View attachment 406119Mkuu tatizo ni kubwa kuliko unavyolifikiria. Usilaumu mwanafunzi.

Tazama hilo tangazo limetoka ofisi ya DVC-ARC. Halafu ujiulize mwanafunzi atakuwa katika hali gani.
Asee, nimelisoma hadi aibu. Siasa mbaya sana. Wasomi wa chuo hiki hawawezi kuleta mabadiliko kama watu wana-cancel ratiba ya kusoma eti wamsikilize Rais. Huruma
 
Mbona wengi mmeulizia UDSM?.

Nawaza tu hapa
Ni kwa sababu ndio chuo kikuu cha kwanza, chuo kilichojengwa na watanzania, chenye miundombinu bora kuliko vyuo vyote vya uma kwa gharama za watanzania, kwaiyo, kina jukumu la kuiwakilisha nchi katika medani za kimataifa, (Responsibility)
Kwa maana hiyo, udsm owe us so many things,
Udsm inapofanya vibaya inatutia aibu kama Taifa.

inaonekana UDSM kina wanyima usingizi sana
 
Udsm ndiyo wenye ngebe sana... Haya hata 30 bora (poor Africa) hawamo!!! Teheteheheee..... Udsm...
 
Mtu anamaliza PHD-UDSM, hajui kingereza, then mnataka kiingie top 30???-I'm not suprised.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Back
Top Bottom